International friendly: Tanzania (Taifa Stars) vs Ivory Coast (Les Éléphants)-Updates

i1382_a.bmp


midomo ya watu wengine ni nuksi tupu....
 
wachezaji wa kibongo wanapenda sifa kama hizi na sio kucheza mpira...​
Tena wachezai wetu hawana nidhamu.Mafanikio kidogo ,kichwa kinavimba halafu mnamlaumu kocha.Hovyooo,mnafikiri mafanikio yanakuja mara moja tu kufumba na kufumbua.
 
Taifa Stars hii hii ambayo imeshindwa ata kuchukua Challenge Cup? Labda tubadirishe kocha na sio huyu kilaza tuliye naye sasa hivi.

Sawa nakubaliana na wewe kwamaba walishindwa kuchukua Kombe la challenge,lkn Maximo amejitahidi kadiri anavyoweza.

Tatizo ni wachezaji wetu ambao wako tofauti sana na akina Drogba,Toure na wengineo kwa sababu walikoanzia ni mbali zaidi ya wachezaji wetu sema kuna kitu kinaitwa 'MSINGI WA MPIRA',nakumbuka Mziray kwenye kipindi cha Kipima Joto aliwahi kusema kwamba wachezaji wa Tanzania hawana msingi wa mpira tofauti na wachezaji wa mataifa mengine ya Kiafrika ambao wanafundishwa malezi ya kimpira toka udogoni/utotoni na ndo maana ukubwani wanaona matunda yao.

Maximo hata akienda Rwanda na Rwanda ikifanikiwa kufika Finali za Kombe la Dunia tuseme la mwaka 2014,tatizo liko wapi kati yetu sisi au Maximo?

Mpira unahitaji uvumilivu,uzalendo,kujituma,kuipenda timu au klabu,maarifa,ukomavu wa kisaikolojia,afya na malezi bora ya kimpira,uongozi bora wenye ushirikiano wa hali ya juu na mchango kutoka Serikalini na kutoka kwa wadau mbalimbali.Kwa haya tuitafika mbali.

Mungu Ibariki Tanzania!
 
Back
Top Bottom