Intelligent Quotient

Cushite

JF-Expert Member
Sep 29, 2013
2,858
3,543
UPO KUNDI GANI? ******************
Leo naomba nitoe darasa dogo ambalo pengine linaweza kuwa geni kwa wengine... Lakini wale walionisoma katika Kitabu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi hawatalishangaa darasa hili bali watapokea madini mapya tu akilini mwao.

Katika maisha ya kuhangaika na kujikokota kusaka maarifa ya ulimwengu, nikiwa nimeketi na laptop tu shambani kwangu Mbutu Kigamboni, Novemba 2016, nilihitimu katika chuo kikuu Huria Uingereza maarufu kama The Open University, katika shahada ya Forensic Pschology, mkufunzi wangu alikuwa ni Mr Keith Zimmerman, hii ilikuwa ni baada ya 2015 kumaliza masomo ngazi ya cheti katika chuo cha International Institute of Certified Forensic Investigation Professionals Inc USA. (IICFIP) (tawi la Nairob).

Ninakumbuka Mr Zimmerman alinipatia kitabu kinachoitwa MURDER INVESTIGATION MANUAL (2006): "Produced on behalf of the Association of Chief Police Officers by the National Centre for Policing Excellence". Kitabu hiki kiliniongoza kufanya mtihani wa mwisho na kuhitimu vema ambapo nilipata nafasi ya kuendelea katika chuo cha Distance Learning Centre UK ambako ninaendelea mpaka sasa...

Kitabu hicho kilinifunza mengi, ambayo leo naomba niyatumie kujenga mada na darasa huru katika makala hii ambayo ni mbegu. Si katika kujikweza wala kukukwaza bali katika kukusaidia wewe rafiki yangu kuutambua ulimwengu na walimwengu wake.

Ujasusi ni hatua ya juu ya shughuli za kipelelezi... Yani ni sawa na mwanajeshi kufikia ukomandoo (field marshal) ambapo sasa hakutakuwa na mafunzo zaidi ya kuyarejelea yaleyale uliyojifunza kama sehemu ya kujiweka sawa.

Hatua za awali kwa mtu anayejifunza ujasusi ni mafunzo ya upelelezi ya kawaida, yaani wote mtatumia msingi mmoja wa mafunzo hayo, sawa kabisa na polisi au mtu yoyote anayeweza kujifunza miiko na taratibu za upelelezi.... Sheria kuu (principles) za upelelezi wowote ule ni NNE tu,
1. Tukio,
2. Hisia (suspect),
3. Kuhoji hisia,
4. Advanced

Hayo manne ndio msingi wa shuguli za kipelelezi duniani kote, yaani mtu yeyote anayesema anafanya upelelezi wa jambo lolote lazima azingatie hayo. Hivyo ukienda kuuliza mwenendo wa upelelezi wake lazima ukute mtiririko huo...

Ujasusi hushughulika zaidi na mambo ya juu (Advanced) kama yalivyo katika mtiririko wa misingi na taratibu za upelelezi, Huku kwenye ku advance upelelezi kuna mnyumbuliko mkubwa sana ambako ndiko ulimwengu wa watu na vile vya ulimwengu huu ndiko viliko.

Unapofika ngazi ya shahada ya kwanza hadi uzamivu ya kusoma ujasusi kwa sehemu kubwa utasoma watu na yawazungukayo, utasoma uwezo wa kumtafsiri binadamu kwa kila nyanja na hasa kupitia milango yake mitano ya fahamu, huku ujasusu huongeza mlango mwingine wa sita.

Binadamu utamtafsiri katika mambo muhimu ya kiusalama tu, ili kuzuia madhara yaletwayo na binadamu huyu kwa wengine (crimes). Hapa ninamaana sasa unaweza kujikita kutambua na kung'amua mauaji (mfano jaribio la mauaji ya Lissu), ugaidi, wizi, ufisadi nk. Kwa ujumla hapa ni makosa ya jinai yote. Ujasusi upo katika kubaini viashiria vya tukio (kabla ya tukio), kuzuia tukio, tukio lenyewe, baada ya tukio, na kusaidia kubaini ukweli baada ya tukio.

Sasa ili ufunzwe ujasusi wa aina hiyo, moja ya somo huwa ni kuwatambua binadamu na makundi yao na namna bora ya kuyakabili makundi haya ya binadamu bila kuleta madhara kwako na katika jamiii kwa ujumla.

Nidhahiri, binadamu kama walivyo viumbe wengine, hutofautiana kwa mambo mengi. Kwa kushindwa kutambua tofauti zilizopo baina yao, binadamu wamekuwa ni viumbe wanaoongoza kwa migogoro. Kwa kuzingatia hilo, Wakufunzi katika vyuo bora vya Ujasusi wanalazimika kuwafunza maafisa ujasusi wanaosomea mambo haya kwa weledi wa hali ya juu sana.

Binadamu wanagawanywa katika makundi makuu mawili kulingana na uwezo wao wa kufikiri na kuchanganua mambo. Makundi hayo mawili yamegawanyika mara mbili na kutengeneza makundi makuu manne kama ifuatavyo:

1.Introvant- Hili ni kundi linalojumuisha binadamu wenye uwezo mkubwa kiakili na wanaotafakari mambo kwa kina. Binadamu wanaopatikana katika kundi hili hutofautiana kwa kiasi kikubwa na wengine kutokana na uwezo wao wa akili (). Kwa lugha nyepesi Hawa ndio wanaoongoza ulimwengu na mielekeo yake.

Kundi hili nalo limegawanyika katika makundi makuu mawili ambayo ni:

A. Melancolin:

Binadamu katika kundi hili ni wenye upeo mkubwa wa kuvumbua mambo ya kitaalam yanayohitaji akili nyingi na wana uelewa mpana kwenye masomo ya Sayansi na Hesabu. Licha ya uimara huo katika akili zao, binadamu wa kundi hili wana hisia zinazogusika na kuchokozeka kirahisi. Kundi hili maranyingi ndilo huwekwa kwenye vitengo vya kuchakata taarifu zote za kijasusi kutoka vyanzo malimbali vya mashirika au idara husika.. Na pia hukaa katika vitengo maalumu vya maamuzi ya mwelekeo wa nchi au taasisi, au shirika.

Wanawake ni wepesi wa kulia pale wanapokerwa hata na jambo dogo. Wana upendo wa dhati lakini wanapotendwa hata kwa jambo dogo, huumia sana kihisia. Wana huruma sana na hawapendi kuona wengine wakionewa. Wana aibu sana wawapo mbele ya watu wengi na ni watunzaji wazuri wa siri. Hawa hutumika mara nyingi katika ujasusi hasa kwenye misheni za kijasusi zinazoitwa honey trup ambapo anaweza kupandikizwa mahali akaolewa, akazaa na kukaa hata miaka kumi na tano katika ndoa, na siku ikifika anatekeleza misheni kilaini na kutokomea.

B. Fragmetic

Hili ni kundi la binadamu ambao wana uelewa mpana, wana uwezo wa kuchanganua mambo kwa kina na kujenga hoja lakini hawawazidi binadamu wa kundi la kwanza (Melancolin). Wana hisia ngumu, siyo waoga na wanajijali wao kuliko watu wengine. Hawa maranyingi huchaguliwa na kuwekwa kwenye vitengo maalumu viitwavyo special oparesheni, maaranyingi wale sirial Killer na special assasinators hutolewa katika vitengo hivi, hawa ni watu maalumu sana, lakini huongozwa na Melancolin katika utendaji wao.

Ni wabishi na hupenda kutumia mifano na takwimu katika ubishi wao. Hawayapi mapenzi kipaumbele katika maisha yao na wengi huishi ‘single’ kwa muda mrefu. Wanajiamini sana hata kwa mambo ambayo hawayajui. Wengi hupenda kuchunguza na kufuatilia maisha ya wengine na wanafaa kwa kazi za ushushushu.

2. Extrovants: Hili ni kundi kuu la pili linaloundwa na binadamu wenye uwezo wa kawaida wa kiakili. Uwezo wao wa kuchanganua mambo ni wa kawaida, hawajishughulishi kujua mambo yasiyo na manufaa na ni wepesi wa kuridhika hata kwa mafanikio madogo. Kundi hili nalo limegawanyika katika makundi makuu mawili:

A. Sanguine-

Kundi hili linaundwa na binadamu wenye uwezo wa kawaida wa kiakili, kufikiri na kuchanganua mambo (wakati mwingine huwa na uelewa mdogo). Ni wacheshi, wanapenda sifa, wanapenda kusikilizwa kuliko kuwasikiliza wenzao na hupenda kuwa wazungumzaji wakuu kwenye kila jambo hata kama hawana ufahamu nalo. Ni wagumu wa kutunza siri.

Hawapendi kujifunza mambo mapya na hata wakifundishwa husahau haraka. Wanapenda sana kuonekana kwa watu kwa kila jambo wanalolifanya hata kama ni dogo. Si waaminifu katika mapenzi na siyo ajabu kuwakuta wakiwa na wapenzi wengi kwa wakati mmoja.

B. Colerick-

Kundi hili linaundwa na binadamu wenye sifa zinazokinzana na kundi la Melancolin. Wana uelewa mdogo katika kila jambo na wengi hukatisha masomo yao kutokana kuwa na vichwa vizito. Ni wakali, wakatili na wana wivu kwa mafanikio ya watu wengine.

Tofauti zote zinaanzia kwenye asili ya kila kundi. Kundi la kwanza (Intovents), asili yake ni kusikiliza na kuufuata msukumo wa nguvu kutoka ndani bila kutegemea mazingira ya nje wakati kundi la pili (Extrovents) husikiliza na kufuata msukumo wa nje ya miili yao. Hisia zao hutegemea mazingira ya nje kuliko ya ndani.

Binadamu wanaopatikana katika kundi kuu la kwanza liitwalo Introvents, ni "wakimya" sana, wanaona aibu kuzungumza mbele ya binadamu wengi ingawa wanapenda kufanya mambo kwa vitendo. Wanaelewa zaidi kwa vitendo na hawaamini kwa urahisi kile wanachokisikia bila kuona vitendo.

Binadamu wanaopatikana katika kundi la pili ni kinyume chake. Extrovents wanapenda sana kuzungumza na kubishana mbele ya wengine hata kama hawana uhakika juu ya kile wanachokibishia. Ni wepesi wa kuamini maneno ya wengine bila kutafakari kwa kina na hupotoshwa kirahisi. Ni wagumu wa kuonesha vitendo juu ya yale wanayoyasema.

Binadamu wanaopatikana katika kundi la kwanza, Introvents ni "wavumilivu" katika mipango ya muda mrefu na hawaoni hasara kulifuatilia jambo moja hata kwa kipindi kirefu. Hawajali linaumiza kichwa kwa kiasi gani ilimradi wafanikiwe. Mara nyingi wanapenda kufanya kazi peke yao na kuwaonesha wengine matokeo.

Kundi la pili ni kinyume chake. Extrovents wanapenda sana kazi nyepesi nyepesi zisizoumiza kichwa na zinazokamilika haraka. Hawapendi kazi ngumu zinazochukua muda mrefu kukamilika na hulka hii inawaweka mbali na mafanikio ya muda mrefu. Wanapenda kufanya mambo katika jumuiya kuficha udhaifu wao na wanapofanikiwa hata kwa kiasi kidogo, hujisifu sana.

Katika nchi zilizoendelea na kustaarabika, Melancolin walio katika vitengo nyeti vya nchi viitwavyo wafanya maamuzi (decision makers) ndio wanaochagua nani awe kiongozi wa nchi toka miongoni mwa vyama vya siasa na ndio wanaweza kumuondoa kwakutumia secrets codes kiongozi wa nchi anayetweza taifa. Lakini hili linategemea sana aina ya muundo wa vitengo hivi, kama vimeathiriwa na siasa za vyama basi vitengo hivi hujikuta vikitumikishwa kwa maslahi ya wanasiasa badala ya kulitumikia taifa kwa maslahi ya taifa.

Na Yericko Nyerere
 
Hiyo hapo juu nimeitoa facebook ilivyo bila editing wanajamvi. wataalam wa hili watusaidie ukweli na hata mifano hai ikiwezekana.
 
inaendelea au ndo mwisho..? kama ni mwisho hujatutendea haki!!
 
Kuna jamaa aliwahi kuichambua hii kitu pale Wapo radio miaka michache iliyopita. Hawa jamaa wapo pale mwenge stand ya bus.
 
Kuna ukweli asee, nina swali hizi ni inborn traits au...najee inawezekana kushift from 1 type to another (hapa naomba nimtolee mfano E. Snowden)
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom