Zomba,Uliona CUF walifanya fujo? walichoma moto magari? walivunja maduka ya watu?
Zomba,
CUF kama CHADEMA Waliamriwa wasiandamane!na wao wakasema ni haki yao kuandamana. Na polisi walijaribu kuyazuia ila walizidiwa maarifa tu.
Na hao CHADEMA walishatembea kilomita 2 bila ya fujo au uvunjifu wa amani yoyote..hapa ni wazi polisi ndio walichochea fujo. Wangeyaacha yakamalizikia na mkutane wake hakuna ambaye angeumia, wacha kuuawa. Na hao wageni wenu wangefurahi kuona TZ kweli ni nchi ya amani na kidemokrasia.
Hakuna mantiki yoyote kwa wana siasa walio mahiri kulazimisha maandamano yafanyike wakati kuna wageni, tena wawekezaji muhimu ambao hakuna nchi katika hii dunia yetu ya sasa isiotaka wawepo au watembelee kwao.
Hivi unasema nini wewe? Roho mbaya, chuki binafsi ni nini, kwa sababu gani na kwa nani?
Sent from my ZTE-BLADE using Tapatalk
You might have skipped brainagra treatment regime! Acha ujinga wako
Nani amekuambia ni lazima kutii polisi hata kama wanafanya uhalifu? Unaishi dunia gani wewe?
Sent from my ZTE-BLADE using Tapatalk
Yote hiyo, ni kwa sababu tu, ya chuki zao binafsi walizozijenga baada ya kuangushwa vibaya kwenye uchaguzi uliopita.
Demokrasi ni kuingia mitaani na kuanza fujo? Demokrasia ni kukaidi amri ya jeshi la polisi?
Kama mngekuwa mnaijuwa demokrasia msingeyafanya yote hayo. Kwa kipi kikubwa kilichowafanya muingie mitaani na kusababisha umwagikaji wa damu? kama si roho mbaya na fitna na uzabizabina?
Je Serikali yako ya CCM walikutangazia kama kuna wageni Arusha? na je kuna Newspaper yoyote iliyoandika huo ujio? Au CCM walitaka kuwachakachua hao wageni baadae wawaibie kwa kuwaandikishia mikataba mibovu!!!!!!!Hizo ndio sababu ambazo hazipingiki, kulikuwa kuna umuhimu gani wa kufanya maandamano wakati kuna wageni? tena ni wawekezaji muhimu? kama si kuwatisha?