Mkuu hujasomeka vizuri. Na-assume unamaanisha imegoma ku-connect kwa kutumia software ya Join Air. Tatizo hili lilinitokea hivi karibuni niliponunua modem ya voda. Fuata maelekezo yafuatayo: install software inayokuja na modem, lengo hapa ni kuinstall drivers za hiyo modem. Hatua inayofuata ni ku-unistall hiyo software. Then, install software ya Join Air na uanze kuitumia.Kuna mchezo Voda wamefanya kwenye ile software inayokuja na modem. Usitegemee Join Air ita-connect kama ile software yao inayokuja na modem haujai-unistall.