Inonga anaondoka Simba mwishoni wa msimu huu 2024

Pole sana mtani, huu mwaka mbali duuuh, huku timu mbovu, kule wachezaji wanataka kusema, pale umepigwa FA yaani mtani huna raha kabisa mwaka huu.
 
Simba haina shida kuachia mchezaji wala huwez skia lawama, ugomvi, wala kutupiwa majini kama wale Walozi wa Kule kwenye mafuriko ya Vinyesi vya Jiji. Ameondoka Mickoson, Okwi, Chama, Sakho, Costa Nyumba, Bwallya nk lkn Mnyama kaenda Champions League mara 5 na wale walozi na kubania wachezaji kakaa miaka 87 ndio kafika Robo Fainali ya Vilabu Barani Afrika.

Timu hii hii mbovu ndio Bingwa na Ngao ya Hisani
Unaumwa bawasili sio bure Kisinda yupo RS Berkane wapo nusu fainali federation, Mukoko yupo nusu fainali na Mazembe, Msuva haina haja ya kueleza , Feisal anapambania kiatu, Saido yupo hapo kwenu nani kawaloga hao? nitajie wachezaji 5 waliofanikiwa baada ya kutoka 5imba
 
Uzuri Simba hatunaga bifu na wachezaji wakimaliza wanaondoka kwa amani au wanauzwa,au kutolewa kwa mkopo kwa amani bila kelele...sio huko ubuntu botho ..weee
Halogwi wala nini Simba wanajua kuachwa. Hakuna atakaemshobokea ili baadae ije kuwa bifu. Afuate utaratibu aende.
 
Beki wa Simba Enoch Inonga anatarajia kuondoka Simba baada ya msimu kumalizika.

Japo Inonga ana mkataba mpaka 2025 ila ameomba kuondoka na ameshaanza mazungumzo na club yake wamuachie.

Pia beki wa kati Che Malone nae anataka kuondoka sababu hafurahii kuwepo Simba.

Za ndani zinasema Simba wanataka kumchukua naodha wa Yanga Bakari Mwamnyeto ambae mkataba wake unaisha Yanga hivi karibuni na bado hajasaini mkataba mpya.
ok sawa
 
Kimsingi Inonga hana faida yeyote akiwa Simba, hujituma akiwa national team...
Hii kauli nimeisikia wanasimba wengi wakiisema ila nadhani ina kasoro. Kwa maoni yangu national team wamejua madhaifu ya Inonga na wamemuelekeza jinsi ya kucheza ili yasiidhuru timu kitu ambacho Simba hakijafanyika.

Kwa mfano, Inonga siyo mzuri katika kupiga pasi ndefu, yaani 95% ya pasi zake ndefu nyingi zinapotea na nyingi kati ya hizo unajiuliza aliona nini hadi anazipiga maana mpira unaenda mahali ambapo hakuna mchezaji mwenzake. Inawezekana ana mapungufu ya macho kuona mbali. Kwa pungufu hili ukiangalia alivyocheza AFCON, Inonga alikuwa hapigi pasi ndefu, na mara nyingi walikuwa hata hawamchezeshi mpira. Kazi yake ilikuwa kukaba na kuzuia, akipata mpira anaachia kwa mtu wake wa karibu anarudi kwenye jukumu lake la msingi, uchezaji tofauti na ule akiwa Simba.
 
Kwa hali hii Yanga atakuwa bingwa kwa miaka mingi sana. Maana wapinzani kila mwaka watakuwa wako busy kujenga tu kikosi chao, huku wakiendelea kujipa matumaini kupitia yule msemaji mwenye damu ya Kinjekitile Ngwale, mwilini mwake.
Subiri shoo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom