Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,720
- 215,773
John na Rose walikuwa majirani na walisoma shule moja nchini Kenya, walipendana sana na uhusiano wao ulihama kutoka kwenye urafiki na kuwa mapenzi. Waliahidiana kufunga ndoa, walimaliza shule darasa la nane, kutoka na hali ya familia zao wote wawili hawakuweza kuendelea na masomo.
John alipata kazi ya ulinzi katika moja ya hoteli za jiji la Nairobi, na walianza mipango ya kufunga ndoa, waliishi kwa amani na kufanikiwa kupata watoto, lakini ukali wa maisha uliongezeka, huduma za watoto na udogo wa kipato cha John. Rose alianza kulima bustani za watu na kupanda maua, ujira aliopata ulisaidia mahitaji ya shule kwa watoto lakini maisha yalikuwa bado magumu.
Kule kazini kwa John, watalii wengi hufikia pale, na mara nyingi wanamuachia John vi zawadi wanapoondoka. John ni mcheshi, pia anapenda kuwa nadhifu. Kuna siku alifika mtalii raia wa Ujerumani mwanamke, yule mama alikutana na John alimuuliza sehemu sehemu ambazo wenzake waliofika Kenya kabla walimwambia ni vizuri kuziona, John alitoa ushirikiano mzuri sana.
John ilibidi awe anamaliza shift yake asubuhi, anakwenda nyumbani kupumzika kidogo then anarudi kukutana na mama Mjerumani. Anamtembeza na wakirudi jioni John anaunganisha kazini. Baada ya mazoea, yule mama akaanza kumpenda John, alimuuliza kama ameoa? Yule mama alimueleza jinsi alivyo lonely huko kwao Ujerumani, hata ameamua kuja holiday mwenyewe.
John alimwambia mama hajaoa ila anamlea mke wa kaka yake ambae ni marehemu na watoto wanne. John alirudi nyumbani akaweka manyanga mezani mbele ya Rose, Rose alijua hii ni break through ya matatizo yetu, walikubaliana, John na mzungu walifunga ndoa. Baada ya kukamilisha utaratibu wa safari, mama alitangulia John akiomba apewe muda wa kuiacha familia ya marehemu kaka yake vizuri.
John aliingia Ujerumani, wakaanza maisha, lakini mara nyingi alikuwa na huzuni, mama alimuuliza nini kinaleta msongo wa mawazo? John alijibu elimu ya watoto wa kaka, walikubaliana watoto wote waende Ujerumani kwa masomo ya university. John alimueleza mke wa kizungu kuwa nyumba anayoishi mke wa kaka si nzuri, basi walijenga ghorofa.
Ili kulinda famila ya kaka, walikubaliana kila mwaka watakwenda Kenya holiday, wanafikia hotelini, si ile ambayo John alifanya kazi, la. Walishafika nyumbani na mke mzungu, lakini mara nyingi John anakwenda kushinda na familia na kurudi hotelini usiku.
Rose ameacha kulima bustani za watu, sasahivi yeye anaita vibarua wamtengezee garden yake.