information security law

mja

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
310
64
Hello JF,
does Tanzania have any legislation governing information security, and if person caught breaching network and steal information what are the consequences?

is there any cyber law, at large?
Regards,

mja
 
Ipo sheria inaitwa Electronic and Postal Communication Act ya mwaka 2010
Hata hivyo sheria hiyo inamapungufu mengi ambayo tume ya kurekebisha sheria
inayafanyia kazi na hivi karibuni yataletwa mabadiliko au sheria/muswada wa sheria mpya bungeni.
Mfano wa mapungufu hayo ni kutokuwepo kwa tafsiri ya Cyber Crime, hakuna chombo kilichopewa
mamlaka ya kupeleleza makosa hayo, utaratibu wa kukusanya ushahidi toka makampuni ya mawasiliano
haupo bayana, kulinda haki ya faragha za wateja siyo bayana, na pia haisemi endapo kampuni ya mawasiliano
ikishindwa au kukataa kutoa taarifa kwa wapelelezi nini kitatokea, haielezi ni muda gani ambao makampuni ya mawasiliano
yanapaswa kutunza taarifa za wateja wao, na pia mara wanapotakiwa kutoa taarifa hizo wazitoe ndani ya kipindi gani
tangu walipopokea request hivyo wakati mwingine makampuni hayo yamekuwa ni kikwazo katika kupambana na cyber
crimes. Aidha sheria hiyo haijaeleza kama kesi za cyber zinabanwa na utaratibu wa siku 60 kabla ya kuanza kusikilizwa.

Aidha utaratibu wa internet cafe haujaainishwa namna ambavyo ikatokea mtu/watu wakaitumia cafe vibaya itakuwaje.
labda hapo wangelazimishwa kuweka cctv camera itakayoweka kumbukumbu ya watu wanaoingia cafe.
 
sheria iliyopo inamapungufu mengi kama cyber crime na matumizi ya cafe ambayo serikali inayafanyia kazi kupitia tume ya kurekebisha sheria.
ki ukweli panahitajika sheria thabiti itakayopambana na makosa mbalimbali ya mawasiliano
 
Back
Top Bottom