India: Mwanaume abeba mwili wa mkewe Km 12

India: Mwanaume abeba mwili wa mkewe Km 12

Na hilo jimbo ni mojawapo ya majimbo yenye umaskini wa kutupa mkuu.
Hata Tanzania kuna sehemu zenye umasikini wa kutupwa. Tatizo India ni la kiubaguzi. Watu vijijini huwa wanafia hospitali na kubebwa ba wabakijiji kwa kutumia kitanda maalaumu. Serikali huwa haitoi magari kwa ajili ya kubeba maiti. Na kama mgonjwa wako ana deni ni lazima ulipe ndio uruhusiwe kuchukua maiti yako.
 
Walikanusha na kudai kuwa huyo jamaa alibeba mwili wa mkewe pasina kuutaarifu uongozi wa hospitali
Wacha uwe na mait muhimbil usiibebe nenda tu na gar uone kama utatoka nayo....waache uongo jaman
 
Mimi mwanadamu ni nini hata nijidai?Kwani mimi nilieumbwa kwa mwili wa nyama na pumzi ya msaada ni nani hata nilewe madaraka?
Mimi ni msafiri,Mpita njia na mpangaji katika Ulimwengu huu uliojaaa dhiki na taabu.

Nina nini mimi?Eti nina jeshi na pesa?Hapana...Hivyo vyote havitanizuia kufa na kuoza na kuliwa na funza.
Nina magari na nyumba za kifahari kushinda wenzangu?Hapana...Hata moja sitazikwa nayo,Yote na ufahari wake nitaziacha nyuma.

Sasa mimi ni nani eti??Mimi si kitu,mimi si lolote...Nijapopita katikati ya majeshi yanayonitii na watu wanaoniogopa...bado mimi si lolote!!Mimi ni fukara na masikini wa mwili na roho.. kiburi na majivuno ya ubinadamu yananidanganya.

Mimi ni mavumbi,katika mavumbi nimetoka,na mavumbini nitarudi....Nitaoza kwa kuliwa na funza...Kilo kilicho changu katika mwili huu wa nyama ktapukutika...Utabaki unywele tu katika shimo la kaburi ili kutimiza hesabu mbele za yeye aliye mkuu kuliko wote.

Thamani yangu si lolote...Nisijivune,Nisijigambe,Nisinyanyase,Nisihusudu vilivyo vya ulimwengu na kuyaacha maisha yasiyo na kikomo.Eee Mungu unirehemu...Kwa kuwa mimi ni mdhambi.
Maneno mazito hayo mkuu
 
Sisi ni maskini lakini sio maskini wa roho Kama India, hapo si mjini kabisa wanawezaje kumpita mwenzao hivyo dah!!! Ee mungu tunusuru, Bora tukose hizo Mali kuliko kupata na kuwa na roho Kama hawa jamaa
 
Kweli india kuna makaudhu watu watu walikuwa wanawaza kumpiga picha tu bila kumpa msaada wowote.
 
Back
Top Bottom