India: Mwanaume abeba mwili wa mkewe Km 12

India: Mwanaume abeba mwili wa mkewe Km 12

Mimi mwanadamu ni nini hata nijidai?Kwani mimi nilieumbwa kwa mwili wa nyama na pumzi ya msaada ni nani hata nilewe madaraka?
Mimi ni msafiri,Mpita njia na mpangaji katika Ulimwengu huu uliojaaa dhiki na taabu.

Nina nini mimi?Eti nina jeshi na pesa?Hapana...Hivyo vyote havitanizuia kufa na kuoza na kuliwa na funza.
Nina magari na nyumba za kifahari kushinda wenzangu?Hapana...Hata moja sitazikwa nayo,Yote na ufahari wake nitaziacha nyuma.

Sasa mimi ni nani eti??Mimi si kitu,mimi si lolote...Nijapopita katikati ya majeshi yanayonitii na watu wanaoniogopa...bado mimi si lolote!!Mimi ni fukara na masikini wa mwili na roho.. kiburi na majivuno ya ubinadamu yananidanganya.

Mimi ni mavumbi,katika mavumbi nimetoka,na mavumbini nitarudi....Nitaoza kwa kuliwa na funza...Kilo kilicho changu katika mwili huu wa nyama ktapukutika...Utabaki unywele tu katika shimo la kaburi ili kutimiza hesabu mbele za yeye aliye mkuu kuliko wote.

Thamani yangu si lolote...Nisijivune,Nisijigambe,Nisinyanyase,Nisihusudu vilivyo vya ulimwengu na kuyaacha maisha yasiyo na kikomo.Eee Mungu unirehemu...Kwa kuwa mimi ni mdhambi.
Umeongezea uchungu asee!
 
Binadamu buana, huyo aliepiga picha hii yeye alishindwaje kumsaidia? Aliona kupiga picha ni jambo la maana zaidi kuliko kumsaidia?? Na hapo panaonekana ni wilayani kabisa ameshindwaje hata kumkodishia Boda boda? Au alimpiga picha kwanza ndio akamsaidia?
Vyovyote vile ilivyokuwa, ila mpiga picha alitenda jambo la maana kutuletea picha halisi ya tukio ili tuelewe vema nafasi na nafsi za wanadamu hapa duniani.
 
Duu hyo picha yenye mtoto akilia ndo inachoma zaidi. Mbaya zaidi kwa mbaali anaonekana mtu mwingine yupo na hamsini zake tu!
 
Watu wengi wamekuwa na interest na tukio la kutembea km 12 na mwili lakini sioni wengi wakiuliza hizo km 48 zilizobaki nani aliubeba mwili kufika kijijini kwao.Habari kama hii ingekuwa nzuri kama tungeambiwa mwishowe ilikuwaje?Aliamua kuuhifadhi hapo km 12 badala ya kwake km 60?au kuna watu wenye mioyo ya utu walimwona na kumsaidia?
 
Mbona jamaa kaandika hapo alisaidiwa usafiri wa gari mpaka nyumbani kwao baada ya watu kumuonea huruma.
 
Hhmm.. Inasikitisha, binadam tuna roho mbaya, hata wa kumsaidia alikosekana..

Halaf hao viongozi wa serikali ni wanafiki.. Wakubali tu walimnyima gari, mtu anatoaje mwili wa maiti hospital pasina taarifa, wanamaanisha kaiba.. Basi wamshtak.. Wakubali tu kuwa wamekosea shenz zao..
 
HV INAKUWAJE NCHI ILE NI TAJIRI SANA INAKUWA MM SIELEWI KABIS
Tatizo sio utajiri, tatizo roho m..ya, kama wao wanafanyiana hivyo mtu baki atafanywa nini? Tukisema tunaambiwa tuna gubu muyaone wenyewe. Nasema ingekuwa Tanzania asingefika mbali hata kama hawamjui wangemchangia ili apate usafiri au wangemuomba shughuli za mazishi zifanywe pale na msiba apeleke nyumbani. Angalia watu wanamshangaa badala ya kumsaidia, hii ndio nchi yangu naipenda sana, tuna upendo wa dhati na kuhurumiana pia, wao ukiwa masikini wanakudharua na kukuona wa nini.
 
India kuna umasikini wa kutisha
hu wa kwetu afadhali mara 1000

kuna watoto wanazaliwa barabarani tu
hadi wanakuwa watu wazima hawajawahi kuishi ndani ya nyumba
Na umasikini wao unachangiwa na ubaguzi yaani kama ulizaliwa katika familia ya kutumwa wewe ni wa kutumwa tuu. Nafikiri hili ndio linachangia umasikini wao.
 
Kweli hili picha la kihindi, kama walimpokea hapo hospital mgonjwa iweje wamruhusu aondoke na maiti, si kuna askari wa hapo hospital, kibali cha kutoka na maiti alipata wapi ? Hiyo hospital isikwepe lawama kabisa
Utetezi wao hauna maana kabisa
 
Binadamu buana, huyo aliepiga picha hii yeye alishindwaje kumsaidia? Aliona kupiga picha ni jambo la maana zaidi kuliko kumsaidia?? Na hapo panaonekana ni wilayani kabisa ameshindwaje hata kumkodishia Boda boda? Au alimpiga picha kwanza ndio akamsaidia?
Mpwa ubaguzi wa india uache tu. Hata kama anauwezo lakini ukiwa daraja la chini utasaidiwa na masikini wenzako tuu sasa kama hakuna masikini karibu ndio hivyo tena.
 
India wana ubaguzi pia inaitwa caste system wanaamini kuna aina ya watu wana 'laana' hawawasaidii wanawatenga...

Hilo la ubaguzi limechangia sana baadhi ya makundi katika jamii ya India kuwa masikini. Wale wanaoitwa untouchables hata fursa ya elimu kwa muda mrefu walikuwa hawapati. Pamoja na kwamba serikali kupitia katiba, ilipiga marufuku ubaguzi na kuweka utaratibu wa fursa kwa makundi yote kupitia mfumo wa quota, bado jamii nyingi zinatambua mfumo wa ubaguzi na itachukua karne nyingi sana kuutokomeza kabisa.
 
Dah huyu jamaa ni jasiri sana. Ina maana huyu bwana hana hata marafiki? Yaani msiba ni wake peke yake?

Nimeumia sana...

Ndugu huko India ni zaidi ya ujuavyo. Maskini anabaguliwa na kunyanyaswa kuliko sehemu yoyote duniani
 
Kweli hili picha la kihindi, kama walimpokea hapo hospital mgonjwa iweje wamruhusu aondoke na maiti, si kuna askari wa hapo hospital, kibali cha kutoka na maiti alipata wapi ? Hiyo hospital isikwepe lawama kabisa

Walikanusha na kudai kuwa huyo jamaa alibeba mwili wa mkewe pasina kuutaarifu uongozi wa hospitali
 
Back
Top Bottom