UINGEREZA imeiweka India katika orodha nyekundu, red list, ya vikwazo vya safari. Rais wa Uingereza peke yao ndio watakaoruhusiwa kuingia kutoka India. Zuio hilo linaanza kesho Ijumaa. April 23, 2021.
Hii ni baada ya mfumuko mpya wa maambukizi na vifo vya COVID-19 nchini India unaoifanya nchi hiyo kuwa kiunga hatari cha ugonjwa huo duniani, new hotspot. Covid-19 ya India kwa sasa inasambazwa na kimelea kipya cha kutisha zaidi chenye mabadiliko mapya mawili vya vinasaba, double mutant.
Marekani nayo imewaasa raia wake kutokwenda India maana hali ni hatari hata kama wamepata chanjo.
Hapa kwetu Tanzania safari za popote ikiwemo India zinaendelea kama kawaida. Tunachofanya ni kupima jotoridi la wasafiri mara wafikapo, kitu ambacho kimeonekana hakiaminiki sehemu nyingi duniani hususan kwa wasafiri wa India. Nchi za Canada, Hong Kong, na nyinginezo zimelalamika kwamba asilimia kubwa ya wasafiri wanaofika kwenye airport zao hukutwa na maambukizi ya Covid-19 wanatokea India, na wanakuwa wamebeba nyaraka kutoka kwao zinazoonyesha hawana maambukizi hayo. Mashirika ya ndege ya India pia yameshutumiwa kwa kusafirisha watu walioathirika na Covid-19
Chanzo:
UK India Travel Advice
India Daily
Center for Disease Control
Sisi tusiopima hatujui kiwango cha maambukizi kikoje hatujui mlipuko mpya wala wa zamani ukoje, sasa hapo tunaanzaje kuzuia hao wahindi kwa kigezo cha huo mlipuko mpya?
India wana double mutation na triple mutation variants.Zote zinasambaa kwa speed na zina madhara makubwa,hiyo double inaathiri sana watoto na hiyo triple Inaweza kukuendesha hata kama umepata chanjo.
Huu ugonjwa kama series na hii double mutation wanadai ishafika UK.
India wana double mutation na triple mutation variants.Zote zinasambaa kwa speed na zina madhara makubwa,hiyo double inaathiri sana watoto na hiyo triple Inaweza kukuendesha hata kama umepata chanjo.
Huu ugonjwa kama series na hii double mutation wanadai ishafika UK.