India kutunga sheria kubana zaidi mitandao ya kijamii baada ya kutunishiana misuli na Twitter

Sam Gidori

Senior Member
Sep 7, 2020
165
414
Baada ya msuguano baina ya serikali na mtandao wa Twitter kufuatia maandamano ya wanaharakati wanaotaka mageuzi ya kilimo kuhusu kuondolewa kwa maudhui yanayodaiwa kupotosha na kuhatarisha usalama wa taifa, serikali ya India sasa inatunga mswada utakaolazimisha mitandao ya kijamii kukubaliana na amri ya serikali kuondoa maudhui na kusaidia uchunguzi.

Muswada huo uliopewa jina Intermediary Guidelines and Digital Media Ethics Code unakuja wakati ambapo mataifa mengi duniani yanajaribu njia mbalimbali za kuwajibisha mitandao ya kijamii kwa maudhui yanayochapishwa na watumiaji wa mitandao hiyo.

Muswada huo, ambao ukipitishwa kuwa sheria utekelezaji wake utasimamiwa na vyombo vya dola, unayataka makampuni ya mawasiliano kuondoa maudhui yanayoonekana kupotosha ndani ya saa 36 baada ya waraka wa serikali unaotaka maudhui kuondolewa kutolewa huku pia ukiyataka makampuni ya mawasiliano kusaidia uchunguzi wa makosa ya kimtandao ndani ya saa 72 baada ya kutolewa amri ya kuhitaji kuchunguzwa. Ikiwa chapisho la mtandao litaripotiwa kuhusisha ngono, kampuni ya mawasiliano italazimika kuliondoa chapisho hilo ndani ya saa 24 baada ya kupokea malalamiko.

Zaidi, muswada huo unayataka makampuni ya mawasiliano kuwateua maafisa watakaokuwa wakisimamia malalamiko na kushirikiana na vyombo vya dola kusaidia uchunguzi pale utakapohitajika, na lazima wawe raia wakazi wa India.

Muswada huo utakapopitishwa utahusisha majukwaa mengine ya kidigitali, ikiwa ni pamoja na vyombo vya habari vya mtandaoni (online media).

Muswada huo pia unawataka wachapishaji wa maudhui mtandaoni kuzingatia mgawanyiko wa kidini na kitamaduni na kuwa makini na maudhui yanayoonesha msimamo, imani au matendo ya jamii au dini fulani.

Wakati bado muswada huo haujapitishwa kuwa sheria, polisi katika jimbo la Uttar Pradesh walimweka kizuizini Mkurugenzi wa mtandao wa Amazon kwa zaidi ya saa nne siku ya Jumanne kwa madai kuwa filamu ya Tandav yenye mrengo wa kisiasa imewaumiza waumini wa baadhi ya madhehebu na imesababisha ghadhabu kwa baadhi ya watu.
 
Social madia imekamata hatamu ya dunia.
Tawal nyingi zinaona kua ni uchawi unaotia doa tawala zao.
Kumbe tawala za zamani zilitawala vizuri kutokana na ufinyu wa nyanja za kupashana habari pia kueneza habari.
 
Social madia imekamata hatamu ya dunia.
Tawal nyingi zinaona kua ni uchawi unaotia doa tawala zao.
Kumbe tawala za zamani zilitawala vizuri kutokana na ufinyu wa nyanja za kupashana habari pia kueneza habari.
Katizame documentary inaitwa "Social Dilema",hata US sasa wanadiscuss jinsi ya kuilimit hii mitandao sababu fake news zimekuwa nyingi na vilevile vijana wamekuwa addicted sana na hii mitandao,imwafanya kuwa wazembe,hawana interaction na wenzao nk.

Humo ktk documentary wanaongea na ma-expert upande wa computer programming walio wahi kufanya kazi Facebook,Insta,Twitter,google nk.

Huyu jamaa Tim Kendall
yzky7jb7an8uf66y6wcr.jpeg

alikuwa anafanya kazi Facebook kama Director of Monetization,alisema kama mitandao isipo dhibitiwa inaweza kuna siku ikasababisha Civil War,sababu fake news zimekuwa nyingi sana.
 
Back
Top Bottom