Uchaguzi 2020 Inawezekanaje miundo mbinu iliyojengwa na pesa za watanzania wote, ionekane kuwa imejengwa na CCM pekee?

Turufu kubwa inayotumiwa na wanaCCM, ili Rais Magufuli apewe tena miaka mingine 5 ya kutawala nchi hii, ni kuwa Rais huyo amejenga reli ya SGR, amejenga mafly overs, amejenga mabarabara ya lami, anajenga bwawa la umeme katika mto wa Rufiji

Nimekuwa nikijiuliza ni kwanini juhudi zinazofanywa na watanzania wote, bila kujali itikadi zetu za kisiasa, sifa zote achukue mtu mmoja, ambaye ni Mwenyekiti wa CCM, ambaye pia ndiye Rais wetu Magufuli?

Kwa kuwa siyo siri tena, kuwa turufu kubwa wanayotumia wanaccm kuelekea uchaguzi mkuu mwishoni mwa mwaka huu, ni ujenzi wa miundo mbinu mbalimbali inayoendelea nchini, utadhani kuwa pesa ya kugharimia miundo mbinu hiyo, anatoa toka mifukoni mwake, yeye Rais Magufuli!

Hata serikali ya makaburu wa Afrika Kusini, walijenga miundo mbinu ambayo ndiyo inayongoza kwa ubora wake humu barani Afrika. Hata hivyo wananchi wa nchi hiyo, waliamua kumchagua mzalendo mweusi, Shujaa Nelson Mandela kuwa Rais wao na kuwapiga chini makaburu weupe ambao ndiyo waliokuwa wakijidai kuwa miundo mbinu hiyo imejengwa na wao.

Vile vile inajulikana kuwa pesa yote ya walipa kodi wa nchi hii, ya wanaccm na wanaChadema, zinakusanywa kwa pamoja na kuwekwa kwenye Hazina ya Taifa na ndiyo hizo zinazojenga, hiyo miundo mbinu, ambayo wanaccm "wanajimwambafai" kuwa wamejenga wao!

Wakati tunaelekea kwenye uchaguzi mkuu mwishoni mwa mwaka huu ni lazima watanzania tusikubali kulaghaiwa kwa hizo propaganda nyepesi kuwa eti miundo mbinu yote nchi hii imejengwa na wanaccm!

Hebu tusikilize sera za kila mgombea na wananchi tuchague kiongozi ambaye tunaamini ndiye atakayetuvusha kama Taifa, katika umoja wetu na kudumisha utulivu wa nchi hii.

Tusichague kiongozi ambaye tunamuona dhahiri kuwa analibomoa kwa kasi kubwa Taifa hili umoja wetu na kuleta chuki ndani ya jamii ya watanzania.

Mungu ibariki Tanzania.
Magufuli na CCM yake ndio wamepewa ridhaa na dhamana ya kukusanya kodi na kusimamia rasili mali zetu wewe kapuku panya mpunga kauze chai huna unalojua zaidi ya kutujazidia server zetu hapa JF.
 
TUKIACHA USHABIKI WA KISIASA
Kiongozi wa juu wa Chama aliyeko madarakani kipindi flani, NDIYE anaweza kusukuma mambo yatendeke na kwa kiasi gani
Mf: China miaka yoote iliongozwa na maraisi wazuri tu ILA alipo ingia Mao Tse Tung (mwaka 1945) ndiye aliyeleta mabadiliko makubwa ya Uchumi yanayoifanya china itishie Dunia Nzima
Tanzania kwa mfano imewaliwa na Maraisi wengi; ila Alipo ingia huyu amesukuma maendeleo kwa kiasi kikubwa naweza kusema zaidi ya mara mbili ya walio pita.
Sisemi kuwa waliopita hawajafanya kitu: Iko hivi, Raisi mmoja anaweza kujenga shule 35, mwingine ajenge 200. au mwingine anaweza kujenga Hospitali (vituo vya afya 50: Mwingine ajengine aingie ajenge 250; na miundo mbinu nk
Hivyo yule aliyeweza kusimamia na kupunguza ubadhirifu hivyo kutekeleza miradi mingi kwa kipindi chake; ndio hujivunia chama chake na sio hapa TZ ni utaratibu wa DUNIA NZIMA
Duu Mparee2 umesoma kitabu gani hicho. Hebu tuambie kabla ya Mao Tse Tung Rais wa China alikuwa nani?
 
Shida ni kwamba sisi wanainchi wenyewe tunapenda sana mfumo wa kudanganywa na kupewa ahadi. Hatuna tofauti na mwanamke ambaye anapenda kupewa ahadi ya vitu vikubwa ndipo atoe gemu kisha akiona hakuna anachopata anaanza lalamika na kusubiria apewe tena ahadi mpya tena na kuendelea kutombwa maisha yake yote ile hali anaona anapigwa chenga.

Kimsingi sisi ndio tunawataka hawa wanasiasa kutuuzia ahadi hewa na pia kutudanganya kuwa wao ndio chanzo cha mafanikio yetu...... Kumbe huu ni uongo.

Sasa leo wabunge wakienda bungeni wanafanya siasa za vyama vyao muda wao ukiisha wanakuja kutuomba ridhaa, ridhaa ya nini sasa?! Maana unatakiwa umuombe ridhaa mtu unaemtumikia, sasa wewe unatumikia chama, why unaomba ridhaa kwangu mimi raia.

Hii ni sawa na mtu umeachiwa mali nyingi sana kisha umteuwe mtu akushikie na kukusaidia namna sahihi ya kuzitumia halafu yeye anakuwa busy kukuzitumia kufanya maisha yake ila napohitaji kuthibitisha nyaraka za umiliki wa mali au akitakiwa kutoa uthibitisho wa aina yoyote anakuja kwako mbio kukuomba na kutumia hela zinazotokana na mali yako kukurubuni umpe uthibitisho akautumie kuendelea kutumia mali yako upuuzi mtupu.

Sasa kimsingi raia ndio mnalea haya majanga na sio CCM wala sijuj nini, na hata hawa chadema mkiwapa ridhaa msitegemee jipya lolote kwasababu wataendeleza michezo ile ile ya chama ila kwa style nyingine.
 
Kinachoonekana ni utekelezwaji wa ilani ya CCM,

CCM inasimamia serikali,ili unapofika tena Uchaguzi kama hivi iwaambie wananchi ilichotekeleza na itakachotekeleza tena kama wakipewa ridhaa.

Hivyo tulia CCM ing'are.
 
lebabu11
Tunachoona hakijakaa sawa, ni kwa huyu Rais tuliyenaye kujiona kuwa apewe sifa yeye pekee, kwa kutengeneza miundo mbinu hiyo, wakati ni kodi za wananchi wote, bila kujali itikadi zetu za kisiasa, ndiyo tuliotengeneza miundo mbinu hiyo
Watu wa ajabu sana, kwa nini mnamsifia lisu kwamba ndio tumainio lenu pekee! So CDM waliobakia wote ni wababaishaji? Kama hivyo sivyo, kwa nini cdm wote msiwape sifa za kuwa tumaini?
 
Hivyo vyote vinajengwa kwa kodi zetu sote na wala siyo hisani ya CCM. Hata daraja LA Kigamboni ambalo limejengwa kwa fedha za NSSF halafu hawa kwa ulofa wao watasema wamejenga wao.Hawa jamaa mshipa wa aibu hawanaga.
Tunahitaji Sera za kumkomboa Mtanzania katika Lindi LA umaskini,maradhi na ujinga ambavyo ni maadui wa asili.
Tusifanye makosa,CDM kupitia Mh.Lissu anatosha.
Gellangi
Umenena ukweli mtupu kwa asilimia 100
 
Mtu mpumbavu hudhani upumbavu ni ushajaa. Mtu mwenye akili timamu huwezi kumsifia mkoloni kisa alijenga shule. Huna tofauti na binti anayepigwa mimba kisa ananunuliwa chips.
Nyie vigoli wa shule ya msingi waziri kuelewa kisa, hamjachezwa unyago. Umeshindea kusoma na kuelewa nilichokiandika sasa utawezaje kujua kama aliyekuoa ni mmeo au kaka yako.
 
Nyie vigoli wa shule ya msingi waziri kuelewa kisa, hamjachezwa unyago. Umeshindea kusoma na kuelewa nilichokiandika sasa utawezaje kujua kama aliyekuoa ni mmeo au kaka yako.
Huna akili mpuuzi wewe umeandika nini cha maana hapo zaidi ya kukariri upuuzi wa Lissu? Eti hata mkoloni alijenga reli,shule na hospital
Hujui kuwa mkoloni alijenga shule kwa ajili ya wazungu na watu wachache kama watoto wa machifu? Hujui kuw alijenga reli ili asifirishe malighafi kwenda ulaya? Alijenga hospital ili atibu wafanyakazi waliomzalishia ili apate malighafi.
Alijeng kwa manufaa ya Tanzania? Huna akili,endelea kukariri upuuzi wa vibaraka wa mabeberu.
 
Back
Top Bottom