Inawezekana kisheria??

Kana-Ka-Nsungu

JF-Expert Member
Oct 4, 2007
2,257
353
Naomba mnisaidie wanasheria. Kuna uwezekano gani wa kutumia sheria ili kuwabana warithi wenzako wa mali ili wasifanye maamuzi juu ya vile mlivyorithi bila ya kukushirikisha? Kwa mfano- kama ni gari, nyumba au shamba, wasiwe na uwezo wa kuuza bila ya wewe kuhusishwa?
 
Mzee, jaribu kuwa very specific na aina ya umiliki ambao hzo mali za urithi zimetolewa kwenu, Je mmamiliki kwa pamoja kwa tafsiri ya kisheria kwamba kila mmoja wenu ana miliki kwa jina lake mali hiyo hiyo (Joint tenantsbayo ukifa na lako limekufa ) au kila mmoja wenu ana sehemu ya share yake katika hizo mali (tenants in common - unaweza kurithisha).

Wakati mwingine inawezekana urithi ukatokewa kwa nyumba ambayo kila mtoto amepewa chumba chake au kwa nyumba ambayo watoto zaidi ya mmoja wamerithishwa nyumba pasipo kutaja yupi, kipi vivyo hivyo kwa shamba, yawezekana kila moja akawa na heka zake katika shamba hilo hilo moja au mkamilikishwa wote kwa pamoja pasipo mchanganuo!.
 
Lets say ni nyumba ambayo hati ya umiliki bado ina jina la babu na hadi usawa huu tumebaki wajukuu tu na ndio tunajaribu kuzidiana kete.
 
Back
Top Bottom