Inawezekana hii ikawa ni kweli? Soma | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Inawezekana hii ikawa ni kweli? Soma

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Tiba, Oct 18, 2010.

 1. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #1
  Oct 18, 2010
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,511
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145

  HALI NI TETE
  IOKOE NCHI YAKO KUTOKA KWENYE UTAWALA BANDIA

  Habari za uhakika tulizozipata masaa machache yaliyopita ni kwamba JK ameingia mkataba na nchi moja kubwa ili shirika la ujasusi la nchi hiyo liweze kumsaidia kupata ushindi kwa wizi bila kuhatarisha amani nchini. Hii ni baada ya balozi wa nchi hiyo kubwa kumpa ripoti ya kijasusi inayoonyesha kuwa bila usaidizi wa nchi hiyo nchi ni lazima itaingia kwenye vita ndani ya Mwezi Novemba.

  Katika ripoti ya shirika hilo la kijasusi imeonyesha kwamba Taasisi ya kijasusi ya Tanzania ama 'idara ya usalama' ukiondoa mkuu wake OR hawana mapenzi kabisa na JK japo kuna wenye mapenzi na CCM. Ripoti hiyo pia imeonyesha kuwa ndani ya vyombo vya usalama na ulinzi ikiwemo JWTZ wana chuki kubwa na JK na wanamdharau kutokana na namna alivyoendesha nchi kwa miaka 5 iliyopita.

  Ripoti pia inaonyesha kuwa wanamtandao wa 2005 tayari wanaendesha kwa siri kubwa mchakato wa kijasusi utakaomfanya JK apate 'suprise' kwa kujikuta ameshindwa kabisa kiti cha urais japo mikakati yote ya kuchakachua matokeo imeonekana kufanikiwa. Hili ni kundi lililokuwa nyuma ya uanzishwaji wa CCJ kwa usiri na kwa kujificha.

  Ripoti imemtaja EL ambaye majuzi alisifiwa na JK na kutambulishwa kwa wapiga kura huko kaskazini mwa Tanzania kuwa ni mmoja kati ya viongozi wa mkakati huu na ambaye tayari amejiandaa kuhakikisha hata jimboni kwake tu ni yeye peke yake anayepita kwa kushinda kiti cha ubunge lakini JK katu hapiti.

  Yako mambo mengi kwenye ripoti hiyo ambayo yalimfanya JK ashindwe kutoa jibu mara baada ya kukabidhiwa ripoti ya mwisho ya REDET na mwanamke mmoja BK wa REDET ambapo hii ilikuwa mara ya pili, kwani mara ya kwanza ilionyesha kuwa JK anaongoza kwa asilimia 81.3 na ndipo baada ya kuangalia upepo akawarudishia ili wairekebishe kwani Dk.alionekana kupata asilimia 6.8 tu jambo lililomfanya JK ang'ake 'wewe unataka kuniharibia wewe, ukimpa asilimia sita si itaonekana uongo wa wazi, kabadilisheni haraka'

  Safari hii ilipoletwa alikuwa tayari ameshachanganywa na ripoti ya shirika lile la ujasusi na hivyo baada ya kumgandisha kwa muda mrefu mama huyo ambaye inasemekana ni girlfriend wake wa muda mrefu na ameshaahidiwa ukatibu mkuu wa wizara ya elimu, JK alimwambia tu 'haya kaitoeni' bila kuiangalia kiundani.

  Habari zinasema kuwa nchi hiyo kubwa ina uchu mkubwa wa madini yetu ya Uranium na haiko tayari kuona nchi nyingine yeyote inayakamata. Hivyo tayari wamekwisha sambaza NGO zao sehemu kubwa ya Tanzania wakijifanya kushughulikia HIV, kumbe wanafanya ujasusi kuhusu rasilimali zetu. Hawa ni magaidi ambao hupenda kuita nchi nyingine magaidi huku wakiwaibia rasilimali zao.

  Hivi sasa wameleta na wanaendelea kuleta majasusi wa shirika lao japo wana utaifa wa nchi mbalimbali kama waangalizi wa kimataifa wa uchaguzi huu ikiwa ni moja kati ya mkakati wa shirika hilo la ujasusi kuhakikisha linatimiza makubaliano ya mkataba, yaani kazi imeanza. Hivyo hata uchaguzi uchakachuliwe mpaka mtoto mchanga mwenyewe aone waziwazi kuwa umechakachuliwa bado waangalizi hao watasema ulikuwa huru na wa haki.

  Hivi sasa shughuli za saidia JK ashinde zimeanza pole pole kuchukuliwa na shirika hilo kutoka kwa mtandao mpya wa JK unaoongozwa na RK, na shughuli za kampeni zinazoongozwa na AK. 'we are taking over from here gentlemen' wanasema majasusi hao.

  Katika mitambo yetu tumenasa mazungumzo ya ndani ya shirika hilo la ujasusi na inavyoonekana lengo kubwa siyo Uranium peke yake bali ni kufanya undumilakuwili(double crossing) kwa kusaidia JK halafu mlango wa nyuma maadui zake ili kuliingiza taifa hili kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe. Inasemekana kuwa nchi hiyo imefanya ujasusi wa kutosha wa kiuchumi na kugundua kuwa nchi yao itafaidika sana kama Tanzania ikiwa vitani kuliko hali ikiwa ya amani. Wanahitaji Uranium lakini baadaye wanataka waipate kwa njia za panya, halafu wauze silaha na mengineyo.

  Nchi hii kubwa inaamini kuwa hakuna biashara inayolipa duniani kama vita. Lakini hawakubali asilani vita kwenye ardhi yao.

  Mtaji wao mkubwa kutokana na habari za uhakika kutokwa kwa mmoja wa makatibu wa kwanza wa ubalozi huo ni kwa uchakachuaji wa matokeo.

  WATANZANIA TUAMKE, JWTZ, TISS NA WENGINEO KUMBE SIYO WALINZI KWENYE UCHAGUZI HUU BALI NDIO WATAKAO TUMIWA NA NCHI HII KUBWA KULETA MACHAFUKO NCHINI. HAITAKUWA VITA KATI YA WANANCHI NA WANANCHI, ITAKUWA VITA KATI YA JWTZ A NA JWTZ B LAKINI WATAKAOUMIA NI WANANCHI WA TANZANIA KWA FAIDA YA WAGENI.

  KAMA UNAIPENDA NCHI HII, ZUIA UCHAKACHUAJI WA MATOKEO AMBAO UMESHAANZA KWA MATOKEO YA TAFITI ZA KISHENZI. VINGINEVYO MUDA SI MREFU........ TANZANIA PIA TUTAITWA NCHI YA KIGAIDI, HUKU JAMAA WAKIBEBA URANIUM, TANZANITE, DHAHABU, ALMASI, WANYAMA WETU, HALAFU HAWATOKI NG'O WAKIDAI KULINDA AMANI MPAKA WAMALIZE KABISA KWA FAIDA YA NCHI ZAO.

  JAMANI EBU TUKUBALI MABADILIKO, TUKUBALI SAUTI YA UMMA, VINGINEVYO TUTAJUTA.


  IOKOE NCHI YAKO KUTOKA KWENYE UTAWALA BANDIA

  TAARIFA HII NI KUTOKA NDANI YA TISS, UPANDE WA WALE WALIOCHOSHWA NA UTAWALA WA JK NA WAFUASI WAKE “CONSERVATIVE HOI POLLOI”
  My Take:

  Nimeipata hii habari kutoka kwa rafiki yangu through email. Sina uhakika na kinachosemwa kama ni kweli, lakini kwetu hapa Bongo kila kitu kinawezekana. Hivi kweli JK anaweza kufikia hatua hii? Tujadili!!! Inasemekana source yake ni TISS kama inavyosomeka hapo juu.
   
 2. Mlachake

  Mlachake JF-Expert Member

  #2
  Oct 18, 2010
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 2,919
  Likes Received: 608
  Trophy Points: 280
  Hivi na wangapi walishasoma post huku wakabaki speechless?
  Hii habari imeniacha speechless.
  yaani siwezi kusema ni uongo wala ni kweli, ila inatisha kama movie.
   
 3. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #3
  Oct 18, 2010
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,840
  Likes Received: 471
  Trophy Points: 180
  Tulishajadili kwa kirefu sana.Ipotezee
   
 4. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #4
  Oct 18, 2010
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,921
  Likes Received: 454
  Trophy Points: 180
  kama ilishaandikwa hii thread vile.......au hii ni nyingine
   
 5. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #5
  Oct 18, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,914
  Likes Received: 214
  Trophy Points: 160
  Hiyo nchi kubwa inayotajwa mbona kama naijua vile?
  Na huo mkakati wao wa kutupiganisha mbona haujawekwa wazi ili tujiepushe nao pindi tuonapo dalili zake?
  Kuhusu Kikwete kukubali hilo jambo sintoshangaa hasa tukizingatia kuwa kwa sasa hana imani hata na watu wake wengi wa karibu..

  Binafsi hii habari bado haijaniingia akilini ingawa sintoipuuza pia!
  Asante mkuu.
   
 6. sblandes

  sblandes JF-Expert Member

  #6
  Oct 18, 2010
  Joined: Apr 25, 2010
  Messages: 2,448
  Likes Received: 781
  Trophy Points: 280
  Mkuu hii habari inaweza ikawa ina ukweli lakini inaweza kuwa imetiwa chumvi.
  Dalili za baadhi ya vigogo wa chama kuwa kimya na kutoshiriki kwenye kampeini inatia shaka kama wanamuunga mkono.
  Maslahi ya hiyo nchi kubwa kuhusu madini ya Uranium, hilo linawezekana hiyo nchi kubwa haina uhakika wa kufaidika na uchimbaji wa madini hayo ikiwa atashinda kiongozi mwingine asiye JK inawezekana msimamo wa Dr Slaa haujaeleweka.
  Hiyo nchi kubwa imekuwa kipenzi cha Raisi JK tokea akiwa waziri wa nchi za nje hivyo wanamuelewa vizuri sana.
  Kitendo cha JK kutoa ahadi nyingi bila bleki inawezekana ana kitu anachojua yeye toka kwa hilo taifa kubwa.
  Kitendo cha yule kiongozi raisi maarufu kwa hotuba toka hilo taifa kubwa kumsifu JK majuzi ni dalili tosha kama kuna kitu nyuma yake.
  Maslahi ya taifa kubwa yanaonekana yako hatarini hivyo wanatafuta nchi tiifu lakini yenye amani na inayopakana na nchi nyingi kuweka jeshi la nchi kubwa hiyo ili kulinda na kuongeza ushawishi wa taifa hilo kusini mwa jangwa la sahara hilo nina uhakika nalo.
  Mambo ya kijasusi yanaendana na maslahi ya hilo taifa kubwa lakini kupiganisha majeshi yetu hilo ni hatari sioni kama hilo JK anawezakulikubali.
   
 7. Joss

  Joss JF-Expert Member

  #7
  Oct 18, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 729
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Kama hii habari ni ya ukweli na TISS wanaifahamu,basi ni muda muafaka wa kuwa wazalendo for the sake of innocent people,you know what you have to do to save lives of millions,that's why you are the secret agents a.k.a National security agents a.k.a intelligence agents,be intelligent now more than ever,you have the right to question and disobey bad orders for the sake of millions of lives.
  Be the heroes now,History will never forget you,I will never forget you,Tanzanians will never forget you !!!!!!
   
 8. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #8
  Oct 18, 2010
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  mh,kila kikicha natamani nisiwepo tanzania.
  hizi movie nazo soma na kuijenga kichwani zina umiza kweli kweli,....
   
 9. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #9
  Oct 18, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
 10. Mdau

  Mdau JF-Expert Member

  #10
  Oct 18, 2010
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,771
  Likes Received: 252
  Trophy Points: 180
  Sitashangaa, historia ipo upande wa hii story POSITIVELY............Marekani ndio utaratibu wake huu,na maandalizi kafanya tangu siku nyingi sana...
   
 11. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #11
  Oct 18, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Hinaonekana kabisa kuwa ni habari ya kupikwa!
   
 12. Deodat

  Deodat JF-Expert Member

  #12
  Oct 18, 2010
  Joined: Sep 18, 2008
  Messages: 1,279
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  Wewe unamwamini sana muungwana eeh? kile kichwa si kizima, chochote anaweza kuamua.
   
 13. WABUSH

  WABUSH JF-Expert Member

  #13
  Oct 18, 2010
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 285
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Thanks wachangiaji, bado sina hoja naona kama kunachakachua but is a food for thought! Habari ni habari tutaifanyia kazi
   
 14. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #14
  Oct 18, 2010
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,846
  Likes Received: 11,965
  Trophy Points: 280
  Kwanza habari yenyewe siiamini inaonekana kama ya kutunga vile, ila kama JK ana mpango huo naomba akamuulize Savimbi alivyofanywa na mabwana zake baada ya madini ya shaba kupungua alitupwa kama mbwa mitaani.
   
 15. P

  Paul S.S Verified User

  #15
  Oct 18, 2010
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Crap. uchochezi mtupu
   
 16. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #16
  Oct 18, 2010
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Tumeambiwa tusitumie neno "Crap" Nitakuchongea kwa mods ufungiwe mpaka wiki mbili baada ya uchaguzi.
   
 17. P

  Paul S.S Verified User

  #17
  Oct 18, 2010
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  mkuu huu ni uchochezi wa siasa. hata hivyo crap inaruhusiwa kama utatoa maelezo kama nilivifanya
   
 18. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #18
  Oct 19, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,748
  Likes Received: 415,867
  Trophy Points: 280
  La kuvunda halikosi ubani
   
Loading...