Inawezekana Hatumuelewi Rais Dkt. Magufuli

Inawezekana Hatumuelewi Rais Dkt. Magufuli

Game changer kwa siasa za Tanzania tulizozoea.Aliposema malumbano ya siasa ni hadi 2020, mwanzoni hatukumuelewa ila sasa anaeleweka kabisa.mikutano ya kisisasa isipopewa baraka na jeshi la polisi ni haramu,hata kama ni ya kamati tu.
Aliposema serikali inahamia Dodoma kabla ya 2020 hatukumuelewa lakini sasa tunamuelewa serikali itaanza kuhamia hapo baada tu ya shughuli za Bunge la mwezi huu.
Serikali yake ilipoamua kutotangaza live mijadara ya Bunge ,wapo watu waliona kama tatizo la muda,ila sasa tunamuelewa.
Aliposema pesa za serikali zinahifadhiwa kwenye benki ya biashara badala ya Benki kuu wapo waliona kama ni issue ndogo sasa anaeleweka vizuri hali ya benki za biashara wamestisha mikopo kwani hawana fedha.
Aliposema nchi ya viwanda hawakumuelewa sasa ni lazima wanafunzi wote wa sekondari kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne kusoma masomo ya sayansi.
Aliposema atamtumbua yeyote asie endana na kasi yake,wapo waliona kama tisha toto,ila sasa wanamuelewa kama gwiji wa kutumbua majibu.
Aliposema hajisikii kutembelea nchi za nje ili kubana matumizi walifikiri ni msaha ila sasa anaeleweka.
Na tutakapo ona pesa zinahamia kwa wanaofanya kazi bado hatutamwelewa tutadhani tupo ndotoni...tatizo ni kuiona Tanzania kupitia kuta nne za nyumba unayotoka hasa zile zenye access to umeme na maji...huku majority wakiwa hawana milo miwili...eti uchumi imara my foot!

Uchumi imara kwa wakusanya kodi na kuzitumia bila kujali haki za msingi za kila mtanzania...Mh. Rais Mungu na malaika wake wakuzunguke usijekubali fellowship ya hao miungu watu...utageuka kuwa jiwe la chumvi...Mungu huyu ni wa upendo aliyemuumba mnyinge ndiye aliyeumba na yule alijipa haki na kuzirasimisha bila kujali kuwa zina mdhalilisha binadamu mwenzake...ukisimama katika haki Mungu hatakuacha uaibike atakufundisha kutoka na kuingia vyema katikati ya watu aliokupa kuwaongoza...

Kwa wanadamu Mungu huongea kwa ishara lakini kwa rafiki zake hujadiliana nao...ninauhakika wa asiliamia zaidi ya 100 kuwa uchumi wa nchi itaimarika kwakiasi ambacho mataifa wataulizana imekuaje....kama ulivyopatikana ndivyo itakavyokuwa hata kwa yaliyobaki kuhusu welfare...
 
Amani iwe kwenu!

Nimejaribu kutafakari kidogo juu ya kauli kadhaa za rais wetu akiwa katika baadhi ya ziara na kubaini kitu..
1. Inawezekana kauli tata za mh. ni za makusudi na zinalengo la kubadili sura nzima ya siasa tulizozoea..Hii nikiwa na maana kwamba wakati tukiwa bize kujadili kauli tata hizo teyari yeye anapata mwanya wa kufanya mambo ya msingi ambayo anatarajia kuyafanya!Ni kama unaweka nyama na wakati huo huo unampigia mluzi mbwa..lazima aweweseke!
kwakweli hapa nakataa, huwezi kubadili sura ya siasa kwa kutamka na kupandisha bei za bidhaa!(huo ni mfano tu) madhara ya kauli zake yanaende nje kabisa ya uwanja wa siasa, pengine hata yeye hushangaa yatokanayo baada ya kuonge.


2.Kauli zake nyingi pia zina vichekesho na mikwara mingi..Hii mikwara inaweza kuwa na lengo la kuwaweka sawa watendaji au watu waovu!Kwa jinsi navyoona haya yote anayafanya makusudi kwa kuamini kwamba meseji zinafika na watu wanamsikiliza neno kwa neno!
nikweli anasikilizwa neno kwa neno, japo kauli zake zina vichekesho kauli nyingine tena zikikinzana na "sera" za selekali yake, kwamba ninyi fyatueni watoto mimi nitasomesha! kisha waziri wake wa afya anaona kosa hilo na kulisahihisha, maahana aliona ukinzani wa jumbe hizi mbili. eti ange iambiaje jamii ifuate uzazi wa mpango? mahana ni kitu kinacho simamiwa na wizara yake.

3.Kwa kuzingatia kuwa watanzania na wanasiasa ni watu wa porojo na propaganda basi naona anacheza kama pele kwenye hili na wanasiasa wengi hawajamstukia!Vyama vya upinzania visipokuwa makini vitabaki kujadili hotuba zake badala ya kujikita kwenye main agenda za vyama vyao..
moja wapo ya kauli zake tata ni kuwazuia hao wana siasa kufanya siasa hadi 2020!, sasa wanajikitaje kwenye ajenda za vyama vyao wakati wamepigwa marufuku kufanya mikutano ya ndani na nje?

4.Pia muheshimiwa kuna wakati kwenye hotuba mambo ya sirini huyaweka wazi wazi..Nahisi anafanya makusudi kuwa hata wale wanaofanya maovu na kusitiriwa kisiasa basi kuna siku watawekwa hadharani..amefanya watu wa deal na wala rushwa kubwa kuwa waangalifu maana kuna siku wanaweza kusemwa hadharani..Miaka ya nyuma hatukuzoea hii na tunaona kama wanadhalilishwa..
hapa yawezekana ukawa sahihi, ila sijaelewa kama kuwaweka wazi ulimahanisha kuwa taja tu wakati wa hotuba au kuiacha sheria ichukue mkondo wake?. kama ni kuwataja tu hiyo haitoshi na haisaidii chochote, yahani fisadi aone aibu?.........


5.Tukumbuke rais wetu ni msomi wa Phd na si bure lazima huwa anajitafakari baada ya hotuba zake lakini pamoja na hilo bado wimbi la kauli tata linaendelea na bila shaka ni makusudi kwa lengo maalum kwa kuzingatia aina za siasa tulizozoea..Yaani huwa anapiga pale pale tunapoona amekosea au atakosea na mbaya zaidi huwa haachi kurudia pale anapoona watu wamekwazika!
ndiyo ni msomi, hapa naona busara na hekima vinaitaaaaaaaaaaaa!!!!!!!!!!!!!.....huwa hana lengo lililo fichama zaidi ya hilo lililo bebwa kwenye kauli husika. hapa naamini kuwa yatokanayo na kauli zake hata yeye huwa ana yashangaa(rejea mfano wa sukari na bei zake elekezi).....si kila msomi ana busara na hekima na waweza kuwa na hekima na busara bila kuwa msomi.

Kitu ninachokiona ni kuwa rais anataka kututoa kwenye aina za siasa tulizozoea,yaani analeta a new era of politics!Wito wangu kwa viongozi wa upinzani na wanaharakati kama kweli mnataka kuisaidia hii nchi mjikite kwenye ajenda zenu na si hotuba zake kwa vipande hasa vyenye utata!Atawapoteza na wakati huo huo yeye anaendelea kuchanja mbuga kisiasa na kwenye ajenda zake..In short I can call him as a game changer and a smart president..
ni kweli anatupeleka kwenye new era of politics zenye sura ya mfumo wa chama kimoja wakati nadhria nzima na sheria vikisema mfumo tofauti kabisa!, kwa wana harakati nao wajiandae kwenye harakati zao machungu na mazito vina wasubiri kwenye awamu hii kwa hatuna tafsiri inayo fanana ya neno UCHOCHEZI!.
TATIZO LA VIONGOZI WETU, HUPATA BUSARA BAADA YA KUTOKA MADARAKANI- by, JENERALI ULIMWENGU.
 
Ame: ... viongozi wa wapinzani wengi wao wakubali kuwa wengine wapo implicated katika mambo fulani fulani ambayo kama kweli wanadhamira ya kujenga taifa lenye high social capital wangeachia nafasi zao kwakujiuzulu ili wale ambao hawajawa tainted wapate moral authority ya kunyooshea kidole waliopo kwenye madaraka...

... ndiyo maana viongozi waliopo madarakani wanapata nguvu ya kufanya chochote kwakua hakuna mwenye moral authority ya kuwanyooshea kidole miongoni mwa waliopo mbele kukosoa

Asante kwa kuelimisha wanaJF hali halisi ya sasa kisiasa, kijamii na kiuchumi inavyodorora kwa sababu ya kiwango kisichoridhisha cha uwajibikaji kimaadili na kijamii (moral and social responsibility).

Mifano ipo mingi ya mimomonyoko ya maadili na kutowajibika kijamii. Inayotia fora na kutia kinyaa ni aina ya maneno yanayotumiwa hadharani, bungeni, mikutanoni, nk hasa na wanasiasa na viongozi. Hata humu JF unasoma bandiko za wachangiaji au waleta mada unajiuliza hayo yameandikwa na mtu mzima au punguani! ATI UHURU WA KUTOA MAWAZO!!!

Nimenukuu mambo mawili tu, kwa yale uliyonijibu, ili kuamsha mjadala kuhusu anayewajibika kujenga "moral and social responsibility"!

Kwa muda mrefu tumefanya makosa makubwa kuacha suala la "moral responsibility" kujengwa na Taaisisi za dini. Sikuona ajabu CHADEMA kuahirisha utekelezaji wa Tamko la UKUTA au Wabunge kushiriki shughuli za Bunge ati viongozi wa dini ndo wamewashauri kufanya hivyo!

Tumefanya makosa pia Katiba yetu kuegemea katika kulinda "social responsibilities" kwa kutunga sheria na kanuni 'siyo' kulinda na kukuza bali kutoa adhabu kwa wasiowajibika kijamii (socially irresponsible).

Anachofanya Rais ni kusisitiza uwajibikaji kimaadili (akikemea mienendo miovu km kiongozi kumsusia kiongozi mwenzake mkono wa salamu, kususia karibisho mbalimbali, nk) na kijamii (akitoa maagizo ya kiutawala km kuwakamata na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria wanaotishia uvunjifu wa amani kwa njia ya aina yoyote).

Ili kumsaidia Rais kutekeleza wajibu wake, kwa dhamana aliyopewa na Wananchi, ili isionekane ni mbabe, dikteta au kuvunja Katiba, ni muhimu kuinganisha "moral and social responsibility" kwenye Katiba Ya JMT.

WanaJF ni mawazo yangu kupanua hoja ya Ame.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Amani iwe kwenu!

Nimejaribu kutafakari kidogo juu ya kauli kadhaa za rais wetu akiwa katika baadhi ya ziara na kubaini kitu..
1. Inawezekana kauli tata za mh. ni za makusudi na zinalengo la kubadili sura nzima ya siasa tulizozoea..Hii nikiwa na maana kwamba wakati tukiwa bize kujadili kauli tata hizo teyari yeye anapata mwanya wa kufanya mambo ya msingi ambayo anatarajia kuyafanya!Ni kama unaweka nyama na wakati huo huo unampigia mluzi mbwa..lazima aweweseke!

2.Kauli zake nyingi pia zina vichekesho na mikwara mingi..Hii mikwara inaweza kuwa na lengo la kuwaweka sawa watendaji au watu waovu!Kwa jinsi navyoona haya yote anayafanya makusudi kwa kuamini kwamba meseji zinafika na watu wanamsikiliza neno kwa neno!

3.Kwa kuzingatia kuwa watanzania na wanasiasa ni watu wa porojo na propaganda basi naona anacheza kama pele kwenye hili na wanasiasa wengi hawajamstukia!Vyama vya upinzania visipokuwa makini vitabaki kujadili hotuba zake badala ya kujikita kwenye main agenda za vyama vyao..

4.Pia muheshimiwa kuna wakati kwenye hotuba mambo ya sirini huyaweka wazi wazi..Nahisi anafanya makusudi kuwa hata wale wanaofanya maovu na kusitiriwa kisiasa basi kuna siku watawekwa hadharani..amefanya watu wa deal na wala rushwa kubwa kuwa waangalifu maana kuna siku wanaweza kusemwa hadharani..Miaka ya nyuma hatukuzoea hii na tunaona kama wanadhalilishwa..

5.Tukumbuke rais wetu ni msomi wa Phd na si bure lazima huwa anajitafakari baada ya hotuba zake lakini pamoja na hilo bado wimbi la kauli tata linaendelea na bila shaka ni makusudi kwa lengo maalum kwa kuzingatia aina za siasa tulizozoea..Yaani huwa anapiga pale pale tunapoona amekosea au atakosea na mbaya zaidi huwa haachi kurudia pale anapoona watu wamekwazika!

Kitu ninachokiona ni kuwa rais anataka kututoa kwenye aina za siasa tulizozoea,yaani analeta a new era of politics!Wito wangu kwa viongozi wa upinzani na wanaharakati kama kweli mnataka kuisaidia hii nchi mjikite kwenye ajenda zenu na si hotuba zake kwa vipande hasa vyenye utata!Atawapoteza na wakati huo huo yeye anaendelea kuchanja mbuga kisiasa na kwenye ajenda zake..In short I can call him as a game changer and a smart president..
sawa mkuu,ngoja tuone yatokanayo.
 
Ni ngumu sana kufahya evalutaion au impact ya uongozi kwa kipindi cha mwaka..Lakini kuna baadhi ya vitu vimmeshafanywa na naamini soon serikali itwaeleza wananchi wake..

Baada ya miaka mitano mtasema hivi hivi kwamba ni ngumu kwa kipindi hiki kifupi kufanya tathmini ya uchumi wa viwanda.
 
Back
Top Bottom