Inawezekana CAG alisema wabunge wa CCM pekee ndio dhaifu ila waupinzani sio dhaifu.....

Iliwekwa poll japa jukwaani na kabla haijaondolewa waliosema bunge ni dhaifu ilikuwa 100%
 
Kama mulikwepa kupigia kura ya referundum ya maoni ya katiba mpya na kuendelea kukumbatia katiba ya mwaka 1977 iliyotungwa kwa mfumo wa chama kimoja inayotoa madaraka makubwa kwa muhimili mmoja wa Executive ku overpower mihimili mingine.Basi haya ndio matokeo
 
Na Lusekelo Mwandemange.

Kwanza nianze kwa kuwapongeza wote waliotumia muda wao kutoa maoni na kujadili suala la Bunge kukataa kufanya kazi na CAG (Controller & Auditor General-Mthibiti na Mkaguzi mkuu wa serikali) kutokana na kauli yake tata aliyoitoa akiwa Marekani kwa kuita Bunge lina UDHAIFU.

Binafsi nimejiuliza maswali mengi kama wengine walivyo hoji. Kwanza nilijiuliza CAG ni nani hasa mpaka aite Bunge ni dhaifu hasa anapohojiwa kuhusiana na hoja za kigaguzi zinazopelekwa bungeni kutopatiwa majibu?. Je kuna kosa gani kwa yeye kuita Bunge ni dhaifu? Na je ni kweli Bunge ni dhaifu? Na kama ni dhaifu katika lipi? Na kwanini atamke hadharani wakati ana nafasi ya kukosoa ndani? Na kwa nini akatamke nje ya nchi na sio akiwa hapa Tanzania? Na je Bunge kukataa kufanya kazi na CAG ni sawa? Na madhara yake ni nini? Na kama sio kupitia CAG Bunge watasimamiaje serikali? Pia nikajiuliza Bunge na CAG nani mwenye mamlaka ya juu kuliko mwenzake na nani anawajibika kwa nani? Hakika maswali ni mengi lakini sina nia ya kujadili maswali yote haya. Niseme tu katika hili naamini Bunge na CAG wote wakosaji.

Katika kujijibu maswali nikaona nifanye tafakali juu ya CAG Vs Bunge hasa katika kuangalia msingi wa uwepo wao katika katiba ya Tanzania. Kwanza CAG ndio mthibiti na mkaguzi mkuu wa serikali na amepewa madaraka hayo kwa mujibu wa katiba ibara 143 na katiba imeainisha kazi zake kuwa143(2) a) kuhakikisha kwamba fedha zozote zinazokusudiwa kutolewa kutoka mfuko mkuu wa Hazina ya serikali matumizi yake yameidhinishwa na kwamba zitatolewa kwa mujibu wa masharti ya ibara ya 136 ya katiba hii na iwapo atatosheka kwamba masharti hayo yatatekelezwa ipasavyo, basi ataidhinisha fedha hizo zitolewe. Na ibara ya 136 (3) Fedha zilizomo katika mfuko mkuu wa hazina ya serikali hazitatolewa kutoka mfuko huo kwa ajili ya matumizi ila mpaka matumizi hayo yawe yameidhinishwa na Mthibiti na Mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali na pia kwa sharti kwamba fedha hizo ziwe zimetolewa kwa kufuata utaratibu uliowekwa kwa ajili hiyo kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge.

Na Bunge ni mhimili katika JMT. Kwa mujibu wa Katiba ibara ya 63(2) Bunge limepewa madaraka kwa niaba ya wananchi kuisimamia na kuishauri serikali ya JMT na vyombo vyake vyote(akiwemo CAG) katika utekelezaji wa majukumu yake kwa mujibu wa katiba hii.

CAG KAKOSEA NINI?

CAG kakosea kwanza kwa kutotambua wajibu wake wa kikatiba au makusudi. Kwa msingi wa Katiba ni wazi kwamba CAG amepewa wajibu mkubwa sana sio tu wa kukagua mahesabu lakini hasa KUDHIBITI. Na Bunge limepewa wajibu wa kusimamia na kushauri Serikali. CAG ndiye mdhibiti mkuu kutupia lawama Bunge na kuita Bunge dhaifu naona sio sawa ila kinyume chake ni sahihi? Kwa mujibu wa katiba CAG anatakiwa athibiti matumizi ya fedha ya serikali, kama kuna lolote halijaenda sawa kwenye eneo hilo haitoshi yeye kukagua na kuonyesha tu mapungufu bali anatakiwa athibiti hayo yasitokee. Ikiwa katiba inampa CAG wajibu wa kuthibiti fedha isitoke kwenye mfuko wa serikali bila kuanisha matumizi sahihi na kufuata sheria alafu CAG anatuandikia taarifa kwamba kuna fedha 1.5Trn hazionekani zilipo na yeye ndo mthibiti udhaifu hapo unakuwaje wa Bunge?

Sababu ya pili, CAG ni kukosa uungwana tu. Kwasababu hata katika mahusiano ya kawaida ukimtolea ndugu ama rafiki kauli ya maudhi kwake hata kama wewe hukumaanisha kama alivyoelewa yeye na ukaona nduguyo kachukia busara ya kawaida tu inatuongoza kuomba radhi yaishe. Sasa CAG ingetosha tu kutambua kwamba kauli yake imeudhi bunge(chombo cha wananchi) na kuomba samahani yakaisha lakini kuweka msimamo kwamba hajakosea inaweza kuwa kweli kisheria hakukosea lakini ustaarabu wa kawaida tu ingefaa aombe radhi na kusema tu jamani mimi sikumaanisha hivyo mlivyoelewa lakini kwakuwa ndugu zangu mmeudhika na kauli yangu basi naombeni radhi tufanye kazi tusonge mbele. Lakini kukataa kuomba radhi kunazua maswali magumu. CAG katumwa na nani? Anatumika? Anajiamini nini?

Sababu ya Tatu. CAG kutamka mapungufu ya Bunge hadharani tena nje ya nchi. Yeye CAG ana access na Bunge ameshindwa nini kushauri Bunge mapungufu ya Bunge. Tukubali tukatae nje ya mipaka ya Tanzania watu hawajui Ndugai wala Prof Asad bali wanajua Tanzania. Sasa hata kama tuna mapungufu yetu kama taifa na kwa yoyote Yule haifai kutangaza kwa ulimwengu. Na anadhurika sio mtu mmoja au sio Bunge ni sisi wote. Hivyo suala la kujenga utamaduni wa kusemana, kuonyana, kuelekezana na kukemeana ndani ni muhimu sana. Sifurahii mtanzania yeyote wakiwemo akina Lissu kusema mambo ya nchi yetu nje ya nchi. Kwasababu kuna haribu taswira ya Tanzania. Katika hili CAG kakosea tena sana.

Sababu ya Nne: CAG kakosea kutamka Bunge ni dhaifu jumla jumla. Yaani kusema Bunge ni dhaifu bila kusema katika lipi? Hivi ni kweli kwamba mambo yooote yanayo ainishwa na CAG bunge halifanyii kazi? Kama ni hivyo ingewezekana vipi hati chafu zikapungua. Mbona mambo mengi sana yaliyoibuliwa na CAG yanajadiliwa Bungeni na kufanyiwa kazi. Sasa kutamka kauli isiyo na maelezo kama hii hakika ina tatiza. Unapolenga kumkosoa mtu inafaa kumwambia umekosea katika lipi na kama ni udhaifu wa bunge ni katika lipi? Je kutunga sheria? Kushauri serikali? Kusimamia serikali? Au katika lipi?

Kwa maoni yangu haya ndio makosa ya CAG katika hili.

BUNGE LIMEKOSEA NINI?

Bunge Spika naye amekosea katika hili.

Sababu ya Kwanza; Kuita vyombo vya habari na kuutangazia ulimwengu gadhabu yake dhidi ya CAG. Kama nilivyosema CAG ni mtu muhimu kwenye nchi na amefanya mengi mazuri kutoa kauli hii moja ya maudhi isingekuwa lazima kwa spika kuja juu kiasi hicho. Tena sio sawa kwasababu tunajenga tension kwa wengine bila sababu. Hoja kwamba CAG aliongea kwenye vyombo vya habari akihojiwa nje hivyo ajibiwe kwa vyombo habari sio sahihi. Katika hili CAG kakosea lakini spika kakosea zaidi. Ingefaa tu kumuita na kumhoji pengine bila hata media na vitisho. Kuchukia sana huku kunaweza kuthibitisha kauli ya CAG kwasababu mara nyingi watu huchukia wanaposemwa ukweli. Kama Bunge mnajua sio dhaifu kwanini kuchukia sana mnapoitwa dhaifu?

Sababu ya pili: ni kukataa kufanya kazi na CAG. Sasa mkikataa kufanya kazi na CAG wakati mnajua CAG ameshawasilisha taarifa yake kwa Rais mnataka Rais apeleke wapi hiyo taarifa. Na je Rais akiwaletea mtamkatalia?. Je hamuoni kama mnamuweka pabaya ndugu Rais. Na kwa kasi ya kazi ya Rais Ndugu John Joseph Pombe Magufuri hastahili kufanyiwa haya na ninyi nyote Bunge na CAG. Nadhani Bunge ingefaa tu kutoa onyo kwa kuwa CAG ni mara yake ya kwanza kufanya kosa la namna hii. Na hata kama hakuwaomba radhi ingefaa tu kutoa onyo ili akirudia ndio mchukue hatua kama hii. Lakini ndugu Spika umechukua hatua kali sana kwa kosa la kwanza. Na adhabu hii inaleta sintofahamu kubwa sana. Mnamuweka Rais njia panda. Na mpaka hapa tulipofikia watanzania tunasubiri busara za Mhe Rais aamue hatima ya jambo lenyewe.

Hivyo nitoe wito kwa Bunge na CAG kulimaliza hili. Na njia ninazo ziona ni tatu. Mosi Bunge mbadilishe adhabu iwe onyo tu na mtangaze kufanya kazi na CAG ,Pili CAG uombe radhi kwa bunge na wabunge nafsi zao zitulie wafute adhabu, Tatu Rais atumie busara kulimaliza hili kwa kuwa anazo busara nyingi na uzoefu wa kutatua migogoro kama alivyofanya kwa suala la Kikokotoo, Suala la Korosho n.k

Tanzania ni yetu sote tuijenge na kuilinda.

Ahsanteni.
 
Umejaribu kuelezea kadri ya ufahamu wako, ila binafsi nakuona wewe ni mtanzania halisi ila una mapenzi mengi kwa upande wa Ndugai.
1. Kusema/kutumia neno dhaifu ni kawaida sana ktk ukaguzi.
2. Kutamkia nje ya nchi au ndani ya nchi haiondoi maana halisi ya neno lenyewe. Kwa maelezo ya CAG mwenyewe kuwa ameshasema sana udhaifu wa bunge ndani ya nchi, lakini uliona impact yoyote katika hilo?
3. Ndugai ana chuki binafsi na wasema kweli ambao hawapendi kujikomba komba kwa mtu.
4. Kuomba msamaha kwa mharifu ni sawa na kumpatia jambazi bastola akateke familia yako
5. Kama ingekuwepo sheria ya kumng'oa mara moja huyo Ndugai ningeomba ifanye kazi hapa. Maana anataka kutupeleka shimoni.
Usipende kujadili mada moja ukachanganya na wengine, unaweza kudharaulika au kupotezewa kile unachojadili ingawa kina faida.
Kama wewe upo upande wa Ndugai mimi nipo kwa CAG.
 
Kwanza na wewe utuombe radhi watanzania: Hakuna mahali CAG aliposema bunge ni dhaifu.

Alibainisha kabisa kuwa yeye alimaliza kazi yake na ripoti ikapelekwa bungeni na akasema kama wabunge hawakuijadli kw a kini itakuwa ni udhaifu wa Bunge.

Udhaifu wa Bunge kwenye kuijadili hiyo ripoti. Alikua specific kabisa.

Hakusema kuwa Bunge ni dhaifu.

Na ukisema kuwa adhibiti peke yake unakosea. Angedhibiti kama pesa iliyotoka angehusishwa. Lakini imetoka kinyemela.
Anachofanya ni kupeleka kwa bosi wake ili ashughulikie wezi au aangalie namna ya kuweka mfumo wa uwazi zaidi. Na Bosi wake anawapelekea wabunge ili wajadili kwa kina na kuunda tume ya kibunge ikibidi ili ifuatilie kuondoa shaka na kuishauri serikali.

Huo ndio utawala bora. Huenda Hata Rais alisubiri kuona wabunge watamshauri vipi lakini badala yake wakawa wanapongeza tu kila kitu mpaka matumizi ya Tr.1.5 bila idhini yao wakapongeza.

Na mbaya zaidi wakawazuia wale waliotaka kuonyesha udhaifu na kuishauri serikali.
 
Kwa taarifa Yako, Raisi ni sehemu ya Bunge. Hivyo bunge likiwa dhaifu basi na Serikali ni dhaifu. Kwa sababu ya Ego, Hii haiwezekani hata kidogo kua kweli.

CAG anapiga hesabu za Matumizi ya Serikali. Ripoti ile mnayooiita ya CAG sio yake binafsi bali ni ya Serikali. Ni mali halali ya Serikali peke yake.

Serikali yetu tukufu, inao uwezo wa kujitathmini au kutojitathmini kupitia Bunge lake tukufu.

CAG akikabidhi ripoti kwa spika tunaweza kuamua kuijadili au kuchagua kutoijadili. CAG hana cha kufanya.


One More...
CAG ndiye Dhaifu, CAG alikubali mbele ya Raisi kua Trilioni moja nukta tano hazijaibiwa popote na hakuthubutu kufafanua alichosema ndani ya ripoti yake mbele ya Raisi.

Akaenda zake kwenye media kunung'unika kua Bunge ni Dhaifu. Na hii inazidi kumfanya kua dhaifu.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Prof Assad was (and will always be) right all day long.

bunge chini ya Ndugai si tu ni dhaifu bali linaendeshwa kama "shule ya vidudu" - Ndugai akiwa ndiye kama headboy huku ticha akiwa 500 km away na remote mkononi!!
 
Sababu ya Nne: CAG kakosea kutamka Bunge ni dhaifu jumla jumla. Yaani kusema Bunge ni dhaifu bila kusema katika lipi? Hivi ni kweli kwamba mambo yooote yanayo ainishwa na CAG bunge halifanyii kazi? Kama ni hivyo ingewezekana vipi hati chafu zikapungua. Mbona mambo mengi sana yaliyoibuliwa na CAG yanajadiliwa Bungeni na kufanyiwa kazi. Sasa kutamka kauli isiyo na maelezo kama hii hakika ina tatiza. Unapolenga kumkosoa mtu inafaa kumwambia umekosea katika lipi na kama ni udhaifu wa bunge ni katika lipi? Je kutunga sheria? Kushauri serikali? Kusimamia serikali? Au katika lipi?
Kwa maoni yangu haya ndio makosa ya CAG katika hili.
Mkuu Mupirocin, kwanza asante kwa maelezo marefu ya kina, unachambua vizuri, ila nina ushauri mdogo kwako.
Next time ukisikia mtu anashutumiwa ametamka kitu fulani, usiishie kusilikiza watuhumu, bali tafuta na aliyetamka usikie hicho kilichotamkwa ujiridhishe ndipo utoe maoni.

1. Jee ulimsikiliza CAG?.
2. Ulisikia akitamka "Bunge Dhaifu"
3. Ulisikia hakusema ni Dhaifu wapi?.

Ukisikiliza upande mmoja kama upande huo ni upande wa vichwa maji na wewe utakuwa kichwa maji. Kama ni upande wa viazi, na wewe utakuwa kiazi.

Kwa kukusaidia tuu
1. CAG hajasema popote "Bunge Dhaifu"
2. Amesema "Bunge Limeinyesha Udhaifu"
3. Na Akataja maeneo yenye udhaifu.

Mtu ambae hajui tofauti ya "Dhaifu" na "Udhaifu" ni kiazi.

Haya hata mimi yakiwahi kunikuta na niliitwa huko huko Dodoma kuhojiwa.

Niliuliza humu "Jee Bunge Linajipendekeza Kwa Serikali?.

Mbunge mmoja kiazi akasimama na kusema nimelidhalilisha Bunge kwa kuliita "Linajipendekeza Kwa Serikali"

Take time kamsikilize CAG alisema nini, usiwategemee Sana watuhumu wengine ni viazi.

P
 
Jibu sahihi na Kuntu Mimi naona ni kwamba Watanzania wote kwa ujumla Wao / Wetu ni dhaifu.
I like this, haiwezekani wote tujengane understanding kuona Bunge ni dhaifu, the Controller and Auditor General in Controlling alipaswa kufanya KAZI na TAKUKURU katika maeneo yanayofanya mounting of Tsh 1.5tr, ili wote tujue through him as a detector.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
I like this, haiwezekani wote tujengane understanding kuona Bunge ni dhaifu, the Controller and Auditor General in Controlling alipaswa kufanya KAZI na TAKUKURU katika maeneo yanayofanya mounting of Tsh 1.5tr, ili wote tujue through him as a detector.

Sent using Jamii Forums mobile app

Na nairudia kwa Kuisisitiza tena kwamba hapa dhaifu siyo sijui CAG Assad, Bunge na Spika wake au Serikali na Rais wake au wale wanaomtetea CAG Assad na Spika Ndugai na Bunge bali ukweli ni kwamba Watanzania wote ni DHAIFU. Nimemaliza.
 
Tumalize kwa kusema.

Bunge letu sio dhaifu maana tumeona likiiwajibisha serikali kutokana na ripoti ya CAG
 
Huwezi sema imepotea mpak aliye kuwa nayo athibitishe au ashindwe kuionyesha, hivyo CAG alipo ulizwa alikuwa bado upande wa pili hawakutoa maelezo yao

Sent using Jamii Forums mobile app
Aliulizwa imeibiwa? Akasema hapa....report inaonyesha kwamba fedha hizo hazina justufication so hajui zilipotumika. Labwq zimeibwa au labda wamekosea kuweka sawa hesabu zao....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom