estlyjonathan
Member
- May 26, 2016
- 84
- 122
habari zenu wadau, kwa kifupi naishi na mama yangu pamoja na mdogo wangu miaka kama saba (7) mimi ndo nilikuwa nahudumia familia kwa kila kitu, marehemu baba yangu alishakufaga miaka mingi iliyopita na marehemu baba aliacha nyumba yenye wapangaji binafsi sijawahi hata siku moja kumsumbua mama kuhusu ela ya pango maisha yakaendelea akatokeaga mzazi mwenzake mama aliyezaa nae mtoto wa kwanza kwa mama yangu yeye tayari kashaolewa sasa kumbe huyu mzazi mwenzie mama ndo anayekulaga kodi ya nyumba yani naandika kwa masikitiko sana moyo wangu unaniuma sana hata kununua vitu vya ndani kama chakula kunisaidia hakuna kuna siku zingine maisha yanakuwaga magumu mpaka nadiriki kufikiria kurudi kijijini mwisho wa siku mungu ananisaidia maisha yanaendelea imenibidi nimvalie njuga huyu mzee na kumwambia mama atumtaki na atumpendi huyu mzee na asikanyage kuja nyumbani imepita siku 3 maza kanuna aongei, nimeona nshachoka.
naombeni ushauri nifanyaje?
naombeni ushauri nifanyaje?