Inauma sana ila maisha yanatulazimisha

Inauma sana ila maisha yanatulazimisha

Wazima jamani!?

Naandika uzi huu nikiwa nabubujikwa na machozi kwa sababu ya maisha yanavyobadilika. Nakumbuka mwaka 2011 dada angu alimaliza chuo cha ualimu na mwaka 2012 akapata ajira. Lakini mimi na vijana wengine wengi tu tumehitimu Vyuo vikuu na bado tunaendelea kufanya kazi zilizo nje ya taaluma yetu.

Ni kawaida sasa kukutana na Degree holders wakichoma mahindi, wakiuza uji, wakifanya vibarua n.k jama hivi kweli serikali haituoni jmn. Katika bajeti ya mwaka 2020/2021 nimeona kutakuwa na ajira 40000! Hivi hizo ajira zinaenda na idadi ya wahitimu waliopo mtaani kweli?

Huwa naumia sana pale ninapokuwa nafanya kazi ambazo zipo nje na taaluma. Mbaya zaidi kuna watu tumesoshwa na serikali kama walijua kuwa hakuna ajira kwanini hawakutupa hiyo pesa tufanyie kazi nyingi?

Sema kweli inauma ila basi maisha tu
Jilipue kama yule jamaa wa Tunisia kama ishara ya kuchoka hali inayokukabili
 
Umekuja na Hoja nzuri sana ila umeiharibu kama siyo Kuinajisi pale tu uliposema kuwa umeshangaa Kuwaona Wenye Shahada zao wakiuza Uji, wakichoma Mahindi na Kufanya Vibarua. Hii ni Dhihaka kama siyo Dharau kwa Watu ambao pengine hawakubahatika kuipata hiyo Elimu ya Chuo Kikuu uliyonayo. Kwa cheap and poor argument yako ya namna hii imeshanionyesha kuwa kumbe Wasomi wengi ( siyo wote ) wa Tanzania huwa mnakwenda tu huko Vyuoni Kusoma na si Kuelimika. Ungeelimika vyema usingendika Kiubaguzi kama siyo Kinyanyapaa hivi. au hujui kuwa kuna Great Thinkers wengi tu japo hawakufika huko Chuo Kikuu na wanafanya hizo Shughuli ulizozidharau hapo katika Uandishi wako? Nachukia sana Binadamu anayedharau Kazi au Fani au Shughuli za Wanadamu wenzie kwakuwa tu Yeye kabahatika kufika University. Binadamu hapimwi kwa Elimu yake bali anapimwa kwa Utu wake pamoja na Ubunifu wake katika Kujikomboa Kimaisha. Badilika upesi tafadhali hujachelewa.
Samahani sana mkuu! Nilivyoandika hivyo sijamaanisha kuwa nadhihaki hizo kazi mkuu lkn sema tunatofautiana kutafsiri kitu. Samahani naonekana nimekukwaza sana. Binafsi napiga kaz za nje na taaluma lkn ukweli n kuwa watu wanatuchykulia kama tumepotea sana tunaopiga hizo kaz na shahada zetu
 
Mkuu soma sana vitabu utaelimika kulaumu serikali sio sahihi. Hata tukikupa urahisi Leo hii hutokaa uweze kufanya hicho unachotaka kufanyiwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu silaum lkn n kazi ya kila serikali kutaftia wananchi ajira. Mimi naweza kuacha kulaum lkn kuna kundi la watu kubwa tu litaendelea kulaumu mkuu. Hata kama n kujiari bas kuwepo na urahisi nadhan unajua mziki uliopo mtaan
 
Dunia nzima watu wanafanya kazi tofauti na walizosomea..
Usikariri lazima uajiriwe Kwa ulichosomea.
Unaweza fanya kingine Kwa ufanisi zaidi..
Hata hao Viongozi hawajasomea Uongozi..
Hakuna kozi ya uraia wala uwaziri .
Asante kwa kunijuza
 
Pole sana...

Hayo yote ni maisha, wewe leo unahaingaika... nawe ipo siku yako itafika...



Cc: mahondaw
 
Samahani sana mkuu! Nilivyoandika hivyo sijamaanisha kuwa nadhihaki hizo kazi mkuu lkn sema tunatofautiana kutafsiri kitu. Samahani naonekana nimekukwaza sana. Binafsi napiga kaz za nje na taaluma lkn ukweli n kuwa watu wanatuchykulia kama tumepotea sana tunaopiga hizo kaz na shahada zetu
kwahy wewe unaangalia wat wanasemaje juu ya ufanyalo kuingz kipato…wew pambn si lazma uajiliwe na serikar,kwan imeandikw wap kwmb mtu aliesoma asichome mahindi na kaz nyngne ulzotaja

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wazima jamani!?

Naandika uzi huu nikiwa nabubujikwa na machozi kwa sababu ya maisha yanavyobadilika. Nakumbuka mwaka 2011 dada angu alimaliza chuo cha ualimu na mwaka 2012 akapata ajira. Lakini mimi na vijana wengine wengi tu tumehitimu Vyuo vikuu na bado tunaendelea kufanya kazi zilizo nje ya taaluma yetu.

Ni kawaida sasa kukutana na Degree holders wakichoma mahindi, wakiuza uji, wakifanya vibarua n.k jama hivi kweli serikali haituoni jmn. Katika bajeti ya mwaka 2020/2021 nimeona kutakuwa na ajira 40000! Hivi hizo ajira zinaenda na idadi ya wahitimu waliopo mtaani kweli?

Huwa naumia sana pale ninapokuwa nafanya kazi ambazo zipo nje na taaluma. Mbaya zaidi kuna watu tumesoshwa na serikali kama walijua kuwa hakuna ajira kwanini hawakutupa hiyo pesa tufanyie kazi nyingi?

Sema kweli inauma ila basi maisha tu
Sasa mzee unataka waajiri kila mtoto na mwalimu wake? Changamoto ni kwamba wahitimu wamekua wengi kuliko nafasi za kazi.... na hii sio Tz pekee bali dunia nzima

Sent using Jamii Forums mobile app
 
maskiniii[emoji22]Polee
Japo mnatunyanyasaga sana na majoho yenu
Malipo ni hapa hapa
karibu tuuze mapuli mkuu Hii ndio dunia kiongozi...Sisi wenyewe tulipenda tusome tuwe na ma_Degree ila ndio hivyo tena Yote unayotaka hayawi inabidi uishi kiubishi ubishi.
 
Wazima jamani!?

Naandika uzi huu nikiwa nabubujikwa na machozi kwa sababu ya maisha yanavyobadilika. Nakumbuka mwaka 2011 dada angu alimaliza chuo cha ualimu na mwaka 2012 akapata ajira. Lakini mimi na vijana wengine wengi tu tumehitimu Vyuo vikuu na bado tunaendelea kufanya kazi zilizo nje ya taaluma yetu.

Ni kawaida sasa kukutana na Degree holders wakichoma mahindi, wakiuza uji, wakifanya vibarua n.k jama hivi kweli serikali haituoni jmn. Katika bajeti ya mwaka 2020/2021 nimeona kutakuwa na ajira 40000! Hivi hizo ajira zinaenda na idadi ya wahitimu waliopo mtaani kweli?

Huwa naumia sana pale ninapokuwa nafanya kazi ambazo zipo nje na taaluma. Mbaya zaidi kuna watu tumesoshwa na serikali kama walijua kuwa hakuna ajira kwanini hawakutupa hiyo pesa tufanyie kazi nyingi?

Sema kweli inauma ila basi maisha tu
Pole sana.

Umesomea nini mkuu?
 
Ndio Mana kibongo bongo wanaotusua ni darasa la saba kushuka chini,wanaojiita wasomi wanakuja ajiliwa na wasioijua shule,
Huu ni upumbavu kabisa wasomi kulialia na kuzunguka na bahasha miaka nenda rudi
 
Jamaa unaandika thread nyingi sana, na hauko consistent kwenye maandishi yako.

Jitathmini.
 
Ndio Mana kibongo bongo wanaotusua ni darasa la saba kushuka chini,wanaojiita wasomi wanakuja ajiliwa na wasioijua shule,
Huu ni upumbavu kabisa wasomi kulialia na kuzunguka na bahasha miaka nenda rudi
Wewe jamaa unasema coz hujui uchungu tu. Afu kama wa darasa la saba ana pesa ya kunilipa aniajiri tu, kwani shida iko wap? Nimesoma ili niajiriwe kujiajiri yawezekana niliona sowez. Lazima kuwepo na watu kufanyia kaz wengine mkuu. Hata kama ww una nasafac ya kiniajiri nakukaribisha tuweke kandaras mkuu
 
Usikate tamaa mkuu !! Endelea kupambana kama ni mafanikio utayapata tu kwa wakati sahihi.
 
Back
Top Bottom