Inauma sana ila maisha yanatulazimisha

Umomi

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
677
983
Wazima jamani!?

Naandika uzi huu nikiwa nabubujikwa na machozi kwa sababu ya maisha yanavyobadilika. Nakumbuka mwaka 2011 dada angu alimaliza chuo cha ualimu na mwaka 2012 akapata ajira. Lakini mimi na vijana wengine wengi tu tumehitimu Vyuo vikuu na bado tunaendelea kufanya kazi zilizo nje ya taaluma yetu.

Ni kawaida sasa kukutana na Degree holders wakichoma mahindi, wakiuza uji, wakifanya vibarua n.k jama hivi kweli serikali haituoni jmn. Katika bajeti ya mwaka 2020/2021 nimeona kutakuwa na ajira 40000! Hivi hizo ajira zinaenda na idadi ya wahitimu waliopo mtaani kweli?

Huwa naumia sana pale ninapokuwa nafanya kazi ambazo zipo nje na taaluma. Mbaya zaidi kuna watu tumesoshwa na serikali kama walijua kuwa hakuna ajira kwanini hawakutupa hiyo pesa tufanyie kazi nyingi?

Sema kweli inauma ila basi maisha tu
 
Mungu yupo hata sasa atafanya
 
pole sana mdogo wangu,
Kwa hali ilivyo saiv hizo ajira walizotenga kwa walimu ni kama elfu 10 kama sikosei. Kama ni kweli bado ni chache sana kulingana na demand iliyopo mtaani wahitimu wa vyuo vikuu wa kada tofauti hususani walimu ni malaki. Lakini pia hizo nafasi elfu 10 ni kwa walimu wa level zote za msingi na sekondari.

Lakini mbaya zaidi ni upepo huu wa janga la kidunia la korona umedhoofisha sana uchumi wa dunia pamoja na nchi yetu as uzalishaji wa huduma na bidhaa umekuwa halted hivyo serikali hazikusanyi kodi inavyotakiwa ambayo hiyo kodi ndo inatumika kuajiri watumishi nk.
Kwa hoja hiyo sidhani kama kuna serikali yoyote katika nchi zetu za kiafrika inaweza kutekeleza huo mpango wa kuajiri maelfu ya ajira kwa sasa.. je ili ije iwalipe na nini, wakati hata hela ya dharura ya kukabiliana na janga hili tunategemea wahisani watusaidie kwani hali siyo hali.

So mdogo wangu endelea tu kujiandaa kisaikolojia kuwa hali siyo hali kwa sasa
 
Dunia nzima watu wanafanya kazi tofauti na walizosomea..
Usikariri lazima uajiriwe Kwa ulichosomea.
Unaweza fanya kingine Kwa ufanisi zaidi..
Hata hao Viongozi hawajasomea Uongozi..
Hakuna kozi ya uraia wala uwaziri .
 
Ase raia bado tunamisconception kubwa tu, Kuajiri haijawahi kuwa kazi ya serikali. Ila miaka hadi miaka serikali imekuwa ikiitaji wataalamu mbali na kuwaajiri ili iwezeshe utendaji wa shukhuri kadha wa kadha za kuwaudumia raia wake.
 
  • Thanks
Reactions: amu
Wazima jamani!?

Naandika uzi huu nikiwa nabubujikwa na machozi kwa sababu ya maisha yanavyobadilika. Nakumbuka mwaka 2011 dada angu alimaliza chuo cha ualimu na mwaka 2012 akapata ajira. Lakini mimi na vijana wengine wengi tu tumehitimu Vyuo vikuu na bado tunaendelea kufanya kazi zilizo nje ya taaluma yetu.

Ni kawaida sasa kukutana na Degree holders wakichoma mahindi, wakiuza uji, wakifanya vibarua n.k jama hivi kweli serikali haituoni jmn. Katika bajeti ya mwaka 2020/2021 nimeona kutakuwa na ajira 40000! Hivi hizo ajira zinaenda na idadi ya wahitimu waliopo mtaani kweli?

Huwa naumia sana pale ninapokuwa nafanya kazi ambazo zipo nje na taaluma. Mbaya zaidi kuna watu tumesoshwa na serikali kama walijua kuwa hakuna ajira kwanini hawakutupa hiyo pesa tufanyie kazi nyingi?

Sema kweli inauma ila basi maisha tu

Umekuja na Hoja nzuri sana ila umeiharibu kama siyo Kuinajisi pale tu uliposema kuwa umeshangaa Kuwaona Wenye Shahada zao wakiuza Uji, wakichoma Mahindi na Kufanya Vibarua. Hii ni Dhihaka kama siyo Dharau kwa Watu ambao pengine hawakubahatika kuipata hiyo Elimu ya Chuo Kikuu uliyonayo. Kwa cheap and poor argument yako ya namna hii imeshanionyesha kuwa kumbe Wasomi wengi ( siyo wote ) wa Tanzania huwa mnakwenda tu huko Vyuoni Kusoma na si Kuelimika. Ungeelimika vyema usingendika Kiubaguzi kama siyo Kinyanyapaa hivi. au hujui kuwa kuna Great Thinkers wengi tu japo hawakufika huko Chuo Kikuu na wanafanya hizo Shughuli ulizozidharau hapo katika Uandishi wako? Nachukia sana Binadamu anayedharau Kazi au Fani au Shughuli za Wanadamu wenzie kwakuwa tu Yeye kabahatika kufika University. Binadamu hapimwi kwa Elimu yake bali anapimwa kwa Utu wake pamoja na Ubunifu wake katika Kujikomboa Kimaisha. Badilika upesi tafadhali hujachelewa.
 
Back
Top Bottom