D Metakelfin
JF-Expert Member
- Mar 23, 2017
- 3,193
- 3,325
*MAJONZI MAJONZI*
Nawasha yangu kurunzi
Nianze andika utenzi
Moyoni nina majonzi
Mwili wajawa na ganzi
Ghafla nashusha pumzi
Kumshukuru Mwenyezi
*_Ni Msiba Wa Taifa_*
*_Mei Sita Ya Majonzi_*
Ghafla simu nafungua
WhatsApp naingia
Taarifa zimeenea
Picha za Kusisimua
Ajali imetokea
Ni Mlima wa Rhotia
*_Huu Msiba Wa Taifa_*
*_Mei Sita Ya Majonzi_*
Gari limetumbukia
Wanafunzi limeua
Thelathini na kadhaa
Na walimu wao pia
Dereva hajabakia
Tanzia kote Tanzia
*_Huu Msiba Wa Taifa_*
*_Mei Sita Ya Majonzi_*
Hao wanafunzi wetu
Hao ni watoto wetu
Hao ni walimu wetu
Hao wote ndugu zetu
Hao ni Kizazi chetu
Poleni wana Karatu
*_Huu Msiba Wa Taifa_*
*_Mei Sita Ya Majonzi_*
Pole kwa wao wazazi
Walojawa na majonzi
Moyoni tuna Simanzi
Machoni tuna Machozi
Hiyo kazi ya Mwenyezi
Amefanya kwa Mapenzi
*_Huu Msiba Wa Taifa_*
*_Mei Sita Ya Majonzi_*
Kwa pamoja tunalia
Tunalia Tanzania
Hii kwetu ni Tanzia
Huzuni imetujaa
Tuzidi kuwaombea
Peponi pakufikia
*_Huu Msiba Wa Taifa_*
*_Mei Sita Ya Majonzi_*
Tunapita Hii Dunia
Hakuna ato bakia
Wao wametangulia
Sisi tutawafuatia
Kikubwa kujiandaa
Kwa Mungu kutubia
*_Huu Msiba Wa Taifa_*
*_Mei Sita Ya Majonzi_*
Walichanua kama maua
Wamezima kama taa
Kifo ni mlango pia njia
Na sote tutaupitia
Kikubwa kujiandaa
Kwa ibada zenye kufaa
*_Huu Msiba Wa Taifa_*
*_Mei Sita Ya Majonzi_*
Lucky Vicent leo Simanzi
Kuwapoteza wanafunzi
Kwao tuliwapa mapenzi
Pamoja bora malezi
Kuwarudisha Hatuwezi
Tumshukuru Mwenyezi
*_Huu Msiba Wa Taifa_*
*_Mei Sita Ya Majonzi_*
Mwisho nitoe pole
Kwake mkuu wa shule
Wazazi wa watoto wale
Watanzania pia Pole
Njia yetu ni Ile Ile
Hatutaishi milele
*_Huu Msiba Wa Taifa_*
*_Mei Sita Ya Majonzi_*
*_Eee Mwenyezi Tunakuomba Utupe moyo wa subira na Uvumilivu katika kipindi Hiki kigumu, pia Tunakuomba Utupe mwisho mwema_*
*Mwenyezi Mungu Azilaze Roho Za Marehemu Mahali Pema Peponi Aamin*
Nawasha yangu kurunzi
Nianze andika utenzi
Moyoni nina majonzi
Mwili wajawa na ganzi
Ghafla nashusha pumzi
Kumshukuru Mwenyezi
*_Ni Msiba Wa Taifa_*
*_Mei Sita Ya Majonzi_*
Ghafla simu nafungua
WhatsApp naingia
Taarifa zimeenea
Picha za Kusisimua
Ajali imetokea
Ni Mlima wa Rhotia
*_Huu Msiba Wa Taifa_*
*_Mei Sita Ya Majonzi_*
Gari limetumbukia
Wanafunzi limeua
Thelathini na kadhaa
Na walimu wao pia
Dereva hajabakia
Tanzia kote Tanzia
*_Huu Msiba Wa Taifa_*
*_Mei Sita Ya Majonzi_*
Hao wanafunzi wetu
Hao ni watoto wetu
Hao ni walimu wetu
Hao wote ndugu zetu
Hao ni Kizazi chetu
Poleni wana Karatu
*_Huu Msiba Wa Taifa_*
*_Mei Sita Ya Majonzi_*
Pole kwa wao wazazi
Walojawa na majonzi
Moyoni tuna Simanzi
Machoni tuna Machozi
Hiyo kazi ya Mwenyezi
Amefanya kwa Mapenzi
*_Huu Msiba Wa Taifa_*
*_Mei Sita Ya Majonzi_*
Kwa pamoja tunalia
Tunalia Tanzania
Hii kwetu ni Tanzia
Huzuni imetujaa
Tuzidi kuwaombea
Peponi pakufikia
*_Huu Msiba Wa Taifa_*
*_Mei Sita Ya Majonzi_*
Tunapita Hii Dunia
Hakuna ato bakia
Wao wametangulia
Sisi tutawafuatia
Kikubwa kujiandaa
Kwa Mungu kutubia
*_Huu Msiba Wa Taifa_*
*_Mei Sita Ya Majonzi_*
Walichanua kama maua
Wamezima kama taa
Kifo ni mlango pia njia
Na sote tutaupitia
Kikubwa kujiandaa
Kwa ibada zenye kufaa
*_Huu Msiba Wa Taifa_*
*_Mei Sita Ya Majonzi_*
Lucky Vicent leo Simanzi
Kuwapoteza wanafunzi
Kwao tuliwapa mapenzi
Pamoja bora malezi
Kuwarudisha Hatuwezi
Tumshukuru Mwenyezi
*_Huu Msiba Wa Taifa_*
*_Mei Sita Ya Majonzi_*
Mwisho nitoe pole
Kwake mkuu wa shule
Wazazi wa watoto wale
Watanzania pia Pole
Njia yetu ni Ile Ile
Hatutaishi milele
*_Huu Msiba Wa Taifa_*
*_Mei Sita Ya Majonzi_*
*_Eee Mwenyezi Tunakuomba Utupe moyo wa subira na Uvumilivu katika kipindi Hiki kigumu, pia Tunakuomba Utupe mwisho mwema_*
*Mwenyezi Mungu Azilaze Roho Za Marehemu Mahali Pema Peponi Aamin*