OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 52,073
- 114,571
Source TBC Waziri Mkuu achangisha takribani Bil 1.4 kuwasaidia waathirika wa tetemeko la ardhi Kagera - TBC.go.tz
Jumla ya Shilingi Bilioni Moja na Milioni 396 zimeweza kukusanywa ikiwa ni mchango wa kusaidia tetemeko la Ardhi lililotokea September 10,2016 .
Waziri Mkuu KASSIM MAJALIWA amesema taifa limepata hasara kutokana na tetemeko kubwa lililotokea mkoani KAGERA mwishoni mwa wiki iliyopita.
Katika mkutano uliofanyika jijini DSM na mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini na Jumuiya ya wafanyabiashara nchini kwa lengo la kuchangia waliokumbwa na tetemeko Waziri Mkuu MAJALIWA amesema serikali inahangaika kuendelea kutoa misaada kwa waliokumbwa na tetemeko.
Amesema shule nne za sekondari zimeharibika na shule mbili zimefungwa kwa muda ili kuzifanyia marekebisho.
Waziri Mkuu MAJALIWA amesema Kamati ya maafa kwa kushirikiana na mkoa wa KAGERA wanaendelea kupitia maeneo mbalimbali kufanya tathmini ili kubaini kiwango cha hasara.
Amesema Rais JOHN MAGUFULI na serikali kwa ujumla inawashukuru waliojitokeza kutoa misaada mbalimbali na wale walio tayari kuendelea kutoa michango ya hali na mali kwa waliokumbwa na tetemeko.
Mh.Ngeleja akiongea kwa huzuni na hisia katika kuhamasisha watu wajitokeze mechi ya mpira ya wabunge ili kuchangia wahanga
''Wabunge wapenzi wa Simba wanatarajia kuumana wikiendi hii, ikiwa ni mechi mahsusi kwa ajili ya kuchangisha fedha za kusaidia wahanga wa tetemeko la ardhi lililotokea hivi karibuni huko mkoani Kagera.
Mbunge wa Sengerema na Mwenyekiti wa Bunge SC, William Ngeleja ameweka wazi kuwa licha ya wabunge hao kuchangia kiasi cha Sh milioni 85 kupitia posho zao wakiwa bungeni lakini bado wameona kuna msaada zaidi unahitajika kwa ajili ya angalau kurejesha hali ya maisha ya awali ya Kagera ndiyo maana kumeandaliwa mechi hizo.
“Lengo letu ni kukusanya fedha za kuwasaidia ndugu zetu wa kule Kagera, angalau warejewe na hali waliyokuwa nayo awali, tangu awali kule bungeni kupitia posho zetu tulishachanga milioni 85 lakini tunahitaji kuongeza zaidi misaada kwao ndiyo maana tumeandaa mechi hii ili kila Mtanzania kupitia kiingilio alichonacho naye ashiriki kuwakomboa ndugu zetu hawa''
WABUNGE YANGA, SIMBA WAUNGANA KUCHANGIA WALIOKUTWA NA MAAFA YA TETEMEKO LA KAGERA - SALEH JEMBE
DUKUDUKU LANGU
Waziri Mkuu ulikuwa mstari wa mbele kutuchangisha kwa ajili ya kuwasadia wahanga wa tetemeko la Kagera,ukaongea kwa unyenyekevu ukilengwa na chozi huku kwa kutumia kitambaa ukijifuta manyunyu ya machozi, leo hii tunakashifiwa umekaa kimya.
Tukumbushe waziri mkuu ni lini uliwahi kusema tunaichangia serikali kwa ajili ya kujenga miundombinu yake
Mungu nakukabidhi hili jambo utahukumu kwa mapenzi yako kwa wana Kagera
Asubuhi jema