NIONAVYO MIMI:KUFUATIA UNITED 0-1 EVERTON PALE SHAMBA LA BIBI.
Smalling jana amemfutia aibu sana Nemanja Vidic,Lukaku alikuwa anamgeuza vyovyote anavyotaka na kuelekea golini kwa De Gea then Smalling ana-block mipira ya Lukaku!
Kumchezesha Rooney kama striker pekee ni sawa na Lory kuliwekea lita moja ya mafuta,jana Moyes katumia robo ya nguvu za Rooney.Ni bora Shabaranks angecheza striker,Giggs akaanza kushoto na Rooney akacheza dimba la juu.
Baada ya Vallencia kushindwa kumpita Bryan Oviedo,Moyes alifanya sub nzuri ya kumuingiza Januzaj na alionekana kuleta uhai.Ukiondoa Rooney,RVP na De Gea wachezaji wote wanaobaki ni kama hawaitendei haki united!
United sio mbaya kiivyo,moyes anashindwa kupanga kikosi kutoka na ubora wa timu pinzani.James McCarthy na Gareth Barry walitisha sana jana.
Kumchezesha Giggs dimba inategemea unacheza na timu gani,Giggs angeanza winga ya kushoto,Rooney na Mawigi kwenye dimba.Kagawa na chicharito washambuliaji,Vallencia beki na Januzaji winga.
Asante Roberto Martinez kwa kuandika historia mpya!