secret file
JF-Expert Member
- Sep 10, 2019
- 5,843
- 8,609
Hujui online marketing and business......Ipo hivi, nina jirani yangu anauza madela na vitu vingine vya kike, kiukweli sijawahi kumuona akiuza chochote au kumuona mteja yoyote akifika dukani kwake kuulizia au kununua chochote.
Sasa huwa ninajiuliza sana huyu dada anafaidika vipi na biashara yake maana huu ni mwaka wa tatu yupo kwenye fremu hiyo hiyo na hana dalili yoyote ya kuhama.
Halafu kingine hata location siyo nzuri kulingana na biashara yake maana hakuna mizunguko mizunguko ya watu.
Pia hata duka lenyewe siku nyingine anafungua jioni kabisa anakaa kidogo anafunga, siku nyingine hafungui kabisa.
Nitapiga picha duka lake na mazingira ya duka lilipo mjionee kwa kweli.