Inastaajabisha Sana, sijawahi kumuona akiuza chochote au kumuona mteja akifika dukani kwake

Ipo hivi, nina jirani yangu anauza madela na vitu vingine vya kike, kiukweli sijawahi kumuona akiuza chochote au kumuona mteja yoyote akifika dukani kwake kuulizia au kununua chochote.

Sasa huwa ninajiuliza sana huyu dada anafaidika vipi na biashara yake maana huu ni mwaka wa tatu yupo kwenye fremu hiyo hiyo na hana dalili yoyote ya kuhama.

Halafu kingine hata location siyo nzuri kulingana na biashara yake maana hakuna mizunguko mizunguko ya watu.

Pia hata duka lenyewe siku nyingine anafungua jioni kabisa anakaa kidogo anafunga, siku nyingine hafungui kabisa.

Nitapiga picha duka lake na mazingira ya duka lilipo mjionee kwa kweli.
Mkuu na ww unaishi vipi sasa??? maana inaonekana kila ikifika aubuhi unakaa barazani hapo mpaka usiku ili kujua kama kutwa nzima kuna mteja kafika kwa jirani yako!!!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom