Inasikitisha sana kuona bado kuna Walimu wapo busy kuadhibu wanafunzi

Madihani

JF-Expert Member
Apr 30, 2015
6,083
6,922
Habari wana jamii.
Pitia link hii
Tanga: Mwalimu ampiga mtoto hadi kupooza

Mwalimu uko busy na mtoto wa mwenzako unamtandika bakora ili upate faida gani?
Halafu mwisho uwekwe kizuizini kwa kosa la kujitakia.
Walimu wote mnaochapa wanafunzi ni wajinga wa kutosha kabisa.

Kazi yako kufundisha tu na kama wanafunzi hawaelewi achana nao,hata ukifanya kazi kwa bidii hakuna wa kukushukuru zaidi ya kudharaulika kwenye jamii.
Walimu acheni kuwa wajinga wa kutosha tafuteni pesa ndio itawapa heshima.

Walimu msitegemee chochote wala msaada wowote pale mnaposababisha matatizo kwa wanafunzi mnaowaadhibu,narudia tena achana nao fanya kazi ya kufundisha tu huwezi kupata matatizo.

Mwl Unyangala.
 
Uko sahihi kabisa, sijui nani aliyewaroga walimu. Serikali yenyewe ndo inazidi kuwaona kama takataka lakini wao wanapoteza muda wao kujipendekeza kufanya kazi zisizo na malipo yoyote kwao. Hivi mtoto akifeli mwalimu anapunguzwa mshahara au anafukuzwa kazi? ya nini kujiletea matatizo hivo? Walimu badilikeni. Kama serikali imeamua kuwapuuza kwa nini na ninyi msijiongeze mkaacha kufanya kazi zisizo za lazima kwenu!
 
Walimu wajinga wachache wanatufanya tuonekane Walimu wote sawa.
Sijui nani amewaroga?
Uko sahihi kabisa, sijui nani aliyewaroga walimu. Serikali yenyewe ndo inazidi kuwaona kama takataka lakini wao wanapoteza muda wao kujipendekeza kufanya kazi zisizo na malipo yoyote kwao. Hivi mtoto akifeli mwalimu anapunguzwa mshahara au anafukuzwa kazi? ya nini kujiletea matatizo hivo? Walimu badilikeni. Kama serikali imeamua kuwapuuza kwa nini na ninyi msijiongeze mkaacha kufanya kazi zisizo za lazima kwenu!
 
Sijakuelewa mkuu.
Mimi nashauri waache kuwaadhibu wanafunzi kwasababu linapotokea tatizo ni lawama za kutosha,na kuwekwa ndani.
Kwa jinsi hali ilivyo sasa kizazi hiki cha nyoka ni ujeuri na viburi vimejaa huku walimu nao wana jazba unategemea nini hapo
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Waachane nao maana wanajipalia mkaa wenye moto,Mwalimu akiwapotezea wanafunzi anakuwa salama zaidi.
Kwa jinsi hali ilivyo sasa kizazi hiki cha nyoka ni ujeuri na viburi vimejaa huku walimu nao wana jazba unategemea nini hapo
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Bora kulaumiwa kwa maneno matupu kuliko kukamatwa na kuwekwa ndani kisa umechapa.

Maneno ni kuyapotezea na kuendelea kupokea mshahara.
Siwezi kukamatwa kwa kosa la wanafunzi kukosa nidhamu bali nitakamatwa kwa kutoa adhabu kwa mwanafunzi.

Niliacha kufuatilia wanafunzi tangu nilipoajiriwa na sioni madhara ya maneno.
Bado watalaumiwa sana hao walimu kwa kushindwa kuwasimamia watoto
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Unaweza kuwa sahihi kwa upande mmoja,lakini kwa upande wa pili mawazo yako ni angamivu,sio tu,kwa taifa lakini pia kwako mwenyewe.

Kuwaacha watovu wa nidhamu (wanafunzi) ni kuharibu taifa,na madhara yake hayatakuacha wewe salama,wanafunzi watukutu wanakera sana,kiasi kwamba kama utakuwa mwalimu dhaifu kwa kuwaacha tu,kesho watakuwa vibaka na watakuibia hata wewe,lakini mbaya zaidi wakiwa wanafunzi wakorofi watakuvizia siku moja wakutwange.

Nadhani,muhimu ni kupaaza sauti adhabu ziruhusiwe kabisa,ila sasa mwalimu usimuadhibu mwanafunzi kama unapiga mbwa mwizi,otherwise awe jeuri kwa kiwango cha kutaka kupigana na waalimu wake,huyo apigwe mpaka ashindwe kutembea,na asipate utetezi popote!!!
 
Hakuna faida yoyote anayopata Mwalimu baada ya kutoa adhabu zaidi ya kulaumiwa,kuwekwa kizuizini na kudharauliwa.

Kwa Mwalimu mwenye akili timamu atafundisha na kufanya yanayomhusu ila sio yanayomletea matatizo.
Unaweza kuwa sahihi kwa upande mmoja,lakini kwa upande wa pili mawazo yako ni angamivu,sio tu,kwa taifa lakini pia kwako mwenyewe.

Kuwaacha watovu wa nidhamu (wanafunzi) ni kuharibu taifa,na madhara yake hayatakuacha wewe salama,wanafunzi watukutu wanakera sana,kiasi kwamba kama utakuwa mwalimu dhaifu kwa kuwaacha tu,kesho watakuwa vibaka na watakuibia hata wewe,lakini mbaya zaidi wakiwa wanafunzi wakorofi watakuvizia siku moja wakutwange.

Nadhani,muhimu ni kupaaza sauti adhabu ziruhusiwe kabisa,ila sasa mwalimu usimuadhibu mwanafunzi kama unapiga mbwa mwizi,otherwise awe jeuri kwa kiwango cha kutaka kupigana na waalimu wake,huyo apigwe mpaka ashindwe kutembea,na asipate utetezi popote!!!
 
ukiona mtu ana ujasiri wa kutukana kundi kubwa la watu kiasi hicho jua fika ana viashiria vyote vya uanahalamu.
na wazazi wake hawakumpatia malez bora hawana maadili.
mm naomba Mungu akusameheme mana hujui ulitendalo.
 
Bora kulaumiwa kwa maneno matupu kuliko kukamatwa na kuwekwa ndani kisa umechapa.

Maneno ni kuyapotezea na kuendelea kupokea mshahara.
Siwezi kukamatwa kwa kosa la wanafunzi kukosa nidhamu bali nitakamatwa kwa kutoa adhabu kwa mwanafunzi.

Niliacha kufuatilia wanafunzi tangu nilipoajiriwa na sioni madhara ya maneno.
Adhabu ilizidi kipimo ni sawa je chanzo cha kisanga hicho ni nini?
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Back
Top Bottom