PreGE2025 Inasikitisha: Rais Samia kasahau nchi anafikira chaguzi tu kwasasa?

PreGE2025 Inasikitisha: Rais Samia kasahau nchi anafikira chaguzi tu kwasasa?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Kamundu

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2006
Posts
9,269
Reaction score
13,895
Nitawapa mambo mawili muhimu

Afya: Pamopja na tatizo kubwa ya mfuko wa bima wa taifa sasa kuna watanzania zaidi ya 1.5M wenye virusi vya ukimwi ambao walikuwa wanategemea USAID. Raisi Trump wa USA kafuta hili shirika na kuzuia pesa. Sasa mpaka leo kama Raisi hajaongea lolote na hakuna mpango wowote kwasababu Mama anafikiria chaguzi tu.

Jeshi: Hivi kuna akili gani na sababu gani ya kushidwa vita na Kagame! nchi ambayo ingeweza kuwekewa vikwazo. Raisi kama Amiri jeshi mkuu hakuna hata nusu bendera tuliona vijana wetu walivyokufa huko. Treni yetu inategemea Congo ili kurudisha matrilioni ya mikopo kwa vizazi vijavyo. Sasa jeshi letu kazi yake hasa ni nini kama hata zile sehemu nyeti za uchumi halisaidii.

Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Jeshi limekuwa waoga na kumwachia madini yote Kagame. Huku ni kukosa umakini kama nchi. Tanzania ingetakiwa kuweka nguvu ambayo ingetoa taarifa kwa wakina kagame kwamba Tanzania italinda vitu ambavyo vina faida kwa taifa. Kagame anafanya hivyo sisi Mama yetu anamfikiria Lissu, usalama wa taifa na Polisi kila siku.

Tanzania ni nchi ya kuombewa na wote tuombe huko mbele tupale Raisi Mzalendo ambaye anapenda nchi kuliko cheo na maslahi binafsi.
 
Mama anaupiga mwingi, nani kama mama, mitano Tena Kwa mama! Hii ndio chorus Kwa sasa...
 
Tanzania ni nchi ya kuombewa na wote tuombe huko mbele tupale Raisi Mzalendo ambaye anapenda nchi kuliko cheo na maslahi binafsi.
Anayepanga rais wa Tanzania, sio wewe, sio yeye, wala sio sisi au mtu mwingine yeyote, anayepanga ni YEYE, kama aliyempangia ni YEYE, hii ina maana ni YEYE aliyepangiwa, kumlaumu ni kumuonea bure tuu huyu mama wa watu!. Watanzania, tuunge mkono 2025 ni zamu ya Mwanamke, ila sio lazima awe yeye bali yule aliyepangiwa na 'YEYE', kama ni yeye aliyepangiwa, then ni yeye!
P
 
lini kafikilia inchi yake ya Tanzania???

jambo gani la maana kafanya ambalo ni memorable??

lini amewangalia wanainchi mwenye hali ngumu ?? na trying to improve there life

lini kafanya improvement ya infrastructure yeyote?? reli tu imeshinda.

my comment, she is the same president we had for the past 4 years nothing has changed.

Ni yule yule tu. watu wamesha mzila amna mtu anajua hata anafanya nini in her day to day life except chawa.

mama ana potential ila chawa wanamcost
 
Back
Top Bottom