Inasikitisha kuona CHADEMA wanawachangisha watu hela Iringa wakati wanapewa hela ya Ruzuku

Status
Not open for further replies.

Chris Lukosi

JF-Expert Member
Aug 23, 2012
4,581
2,937
Ndugu zanguni

Jana kama wote tulivyoona viongozi wa chadema waliamua kama kawaida yao kwenda kufanya mkutano Iringa mkutano ambao toka Msigwa achukue ubunge ni kama wa hamsini sasa. Sikatai msigwa inabidi aendelee na kampeni kwa sasa kwani amekalia kuti kavu hivyo inabidi kila mwezi lazima apige mkutano mmoja au miwili kuwabembeleza wanyalu.

Jambo lililonishangaza ni kuona wakati mkutano unaendelea Dr Slaa alisimama na kuwaomba wananchi wachange hela za mafuta.

Naomba niwaulize maswali yafutayo;

Kama kweli unataka kuwasaidia wananchi inakuwaje unwaomba hela wakati unajua hawana?

Chadema wanachukua ruzuku serikalini hela ambayo ndio ilitakiwa itumike kukijenga chama ziko wapi?

Kama kweli wabunge wana uchungu na wananchi ni kwa nini wasitumie posho zao kununua mafuta?

Kama kweli wabunge wa chadema wana machungu kwa nini wamenunua magari yenye injini kubwa yanayokunywa mafuta mengi? si wange tumia Nissan micra au Toyota Vitz zenye injini ndogo? ili wasiwe wanawaomba omba wanachi hela ambao tayari wao wanahitaji msaada wao?

Chadema kuweni na huruma kwa wananchi, msiwafanye wananchi mitaji. Wananchi walaiwasaidia wakati wa kampeni kwa hiyo sasa ni wakati wa nyinyi kulipa sio kuomba omba miaka yote.
scam.jpg

JITAMBUE!
 
" Please chip $5 to support Obama for 12" ulikuwa ujumbe kwa wamarekani wote hasa (47%) ambao Mitt Romney did give a damn about. Obama alikuwa Rais, anaruka na AirForce One, hizo pesa zilikuwa za nini? Lakini ndizo zilizo run campaign na kumwezesha kushinda tena. Wewe kama business man, you should know umuhimu wa michango to run project. SHAME ON YOU
 
Hii ni moja kati ya mada ambazo they lack all depth
Nikupe mfano hai labda unaweza kupata picha kamili:
Rais Obama na chama chake Democratic katika chaguzi zote zilizopita walipitisha bakuli isivyokawaida kufanikisha uchaguzi. Haikutosha uchaguzi tu, ila hupitisha bakuli kila siku kuomba wenye mapenzi mema kuchangia shughuli mbalimbali za chama na miradi ambayo serikali ya marekani haiwezi kugharimia. Wakati taifa kubwa kama hilo linafanya hivyo iweje kwa taifa maskini kama Tanzania. Fahamu kuwa Democratic ndio chama tawala nchini Marekani na Republican chama cha mabepari na makabaila ni chama za upinzani.

Kwa taarifa yako pamoja na mimi kuwepo Tanzania, bado napata email za Democratic kuniomba nichangie chama. Labda ungeanzisha uzi mwingine, lakini hii ya kuchangia chama umeteleza, nimekujibu hivi ikiwa kama njia ya kukushika mkono kukuinua ulipoteleza na urudi kujipanga upya kuleta mada yenye kujenga maudhui yanayoleta maana nzuri na ya kweli.
 
Yes, kuwa successful business man katika project mbali mbali lazima uwe na kitabu cha mahesabu na ufahamu nini maana ya debit & credit. Kwani hujui wahenga walisema mali bila daftali hupotea bila mwenye mali kuwa na taarifa.

Liko wapi hilo daftali la mali inayochangwa kwa hii project?.

Hata kama ni mradi binafsi, lazima uwe na daftali kama ilivyo kwa Democratic ya President Obama.

Kama isivyojulikana kwa majina kwa wale wanaochangia hii project ya CHADEMA na isiwe ndiyo sababu ya kutokuwa na daftali.

This is just small ask but very important
 
Kuna mada nyingine usipokuwa makini unaweza kujidhalilisha mleta mada mwenyewe na kuonekana upeo wako kuwa wa kiwango cha masafa mafupi mno isivyotegemewa.
Chama cho chote cha siasa ni chama cha wananchi, viongozi wa juu hadi matawini wanawawakilisha wanachama na wananchi na kazi yao kuwaongoza wanachama wao.

Tunachangia serikali kila siku, serikali ni fukara haina pesa hata senti moja, lakini ni tajiri kutokana na michango yetu kupitia kodi mbalimbali. Hata wanapotangaza bajeji huwa hawana pesa isipokuwa makisio ya kodi zinazotazamia kukusanywa.

Chama cha siasa nacho ni mali ya wananchi, na kama chama kinahitaji wananchi wachangie gharama za uendeshaji na pengine hata gharama za kampeni tatizo nini? Kama CCM ina mazoea ya kuiba pesa za serikali kuendeshea shughuli zake hizo ni pesa haramu, waache wananchiwenye moyo wachangie vyama vyao vya siasa.

Mdau mmoja hapo juu nadhani Njele kasema kuhusu Marekani, ni kweli kabisa, hata mimi kwa vile kuna kipindi nilikuwa huko na kabisa kuwa na communication nyingi na idara mbalimbali wakati nafanya kwanye gazeti moja kubwa huko email yangu inajaa maombi ya kuchangia Democratic. Republican hawafanyi hivyo kwa vile ni chama cha matajiri na wana njia zao za kuchngia, lakini chama Cha Obama ni cha walalahoi, hivyo basi walalahoi ndio wenye kukisimamia, kuiendesha na kuchangia gharama za kuendesha chama.

Ndugu yangu hapa huko sahihi kabisa, na kama kuna mtu amekushawishi kufanya hivyo basi siku nyingine fikiria kwanza kabla ya kuweka mada maana hapa unaweza kuonekana ni mtu usiyeweza kuwa na uelewa wa kutosha katika mambo ya mfumo wa serikali na vyama vya siasa katika gharama za uendeshaji wake hali kadhalika vyanzo vya mapato.

Kama kuna wa kukurushia madogo katika mada hii umejitakia mwenyewe, maana hata tu kwa ile kitu inaitwa common sense haiingii akilini kabisa.
 
Usiku wote huo (kwa Tz, maana huku US ni jioni sasa) hujalala unaiwazia CDM. Kweli CDM inawanyima usungizi.

Wewe nawe, bora ujue kama hujui kuliko kuanika ujinga hapa.

Kwa vile wewe uko US basi lazima wengine watakuwa tu Tanzania.

Shule gani hiyo uliyoenda ambayo haikukufungua kufahamu kama dunia siyo Tanzania na US peke yake ukizingatia hata US time zone zinatofautiana kati ya jimbo na jimbo.

Jibu hoja, haya mambo ya time zone niya dalasa la nne kama elimu yako ya awali ulichukulia Tanzania. Kama huna hoja, soma bandiko na kuondoka. Hii nayo ni hekima na busara pia.
 
Yes, kuwa successful business man katika project mbali mbali lazima uwe na kitabu cha mahesabu na ufahamu nini maana ya debit & credit. Kwani hujui wahenga walisema mali bila daftali hupotea bila mwenye mali kuwa na taarifa.

Liko wapi hilo daftali la mali inayochangwa kwa hii project?.

Hata kama ni mradi binafsi, lazima uwe na daftali kama ilivyo kwa Democratic ya President Obama.

Kama isivyojulikana kwa majina kwa wale wanaochangia hii project ya CHADEMA na isiwe ndiyo sababu ya kutokuwa na daftali.

This is just small ask but very important

Miaka 5 iliyopita nilimchangia Obama, lakini sikupewa takwimu za mapato na atumizi ya michango zaidi ya emai na barua ya asante tu. Jaribuni kuangalia mazingira na nafasi ipi maana ni mamilioni ya wananchi, ukitaka kujua mapato na matumizi ya pesa za michango nenda kwa mhasibu wa Chama atakupa taarifa, lakini fanya hivyo tu iwapo we umekuwa ferified mchangia chama.
 
Nadhani wewe TOPIC zako saa NYINGINE ni kama VILE haufikirii na HAUISHI NJE ya NCHI na kuelewa kuwa LABOR party na CONSERVATIVE pamoja na kupata pesa toka serikalini bado wanachangisha Wananchama Wao either kwa DINNER PLATE costs maybe 500 pounds...

Au, OBAMA anawachangisha kina J-Z na BEYONCE kwasababu UCHUMI wa USA na UK sio sawa na wa BONGO hatuna Macebrities kama huko; na Hawalazimishwi..

Wewe unaangalia MIKUTANO ya CCM; Wanatoa VYAKULA; Wanatoa Usafiri ; Wanatoa T;SHIRT KHANGA na PIA wanamleta DIAMOND unadhania hiyo ni RUZUKU ya serikali???? CCM inachota kwingine zaidi...

WEWE ANGALIA MIKUTANO YA CCM ni UFUJAJI wa PESA...

1, Wanapewa USAFIRI kwenda kwenye MIKUTANO na T-shirt za CCM nani anapesa za kuchezea kama sio WIZI?

65106_450487505025763_1721346781_n.jpg

2. Wanachama wa Chama Tawala cha CCM wanalishwa Wali na Maharagwe na Nyama tamu ili tu wasiondoke kwenye MIKUTANO - kwasababu Wamenyonywa VYa kutosha na Serikali tawala... the GAP BTN RICH and POOR imeongezeka VIBAYA scrabs everywhere

934945_450487301692450_419593028_n.jpg

3. CCM inapata pesa wapi kualika Mwanamuziki GHALI kama DIAMOND? Bado haijawalipa Makatibu Kata; Wakulima wa Pamba toka Mwaka Juzi... Ndio hapo bado kila Miradi ni Mikopo toka CHINA

attachment.php
 
CHIS LUKOSI - THIS is HOW CONSERVATIVE PARTY RAISE MONEY....

NEWS

Fury over Tory Party fundraising ball sponsored by mega-rich bankers

30 Jan 2011 00:00A banker is sponsoring David Cameron’s lavish £1,000-a-head Tory ball next week

sm-image-6-313904166.jpg

David Cameron at the Black and White Conservative party Ball 450 (Pic:GoffPhotos)

sm-image-6-313904166.jpg

David Cameron at the Black and White Conservative party Ball 450 (Pic:GoffPhotos)A multi-millionaire banker is sponsoring David Cameron’s lavish £1,000-a-head Tory ball next week.

Howard Shore, whose investment bank made £14.6million last year, has helped bankroll the bash.

He is an “unashamed capitalist” who thinks the public sector is “bloated” and that thousands of jobs should go.

Mr Shore will be one of dozens of super-rich bankers toasting the Government’s failure to make a major dent in their -£7billion -bonuses. The star guests will be Prime Minister David Cameron and -Chancellor George Osborne.

Mayfair-based Shore Capital, founded by Tory donor Mr Shore, is sponsoring The Black and White Party – so-called because guests are supposed to turn up dressed only in black and white.

Details of the celebrity-studded party follow shock figures showing Britain now faces a “double-dip” recession, with the economy shrinking by 0.5 per cent in the final three months of 2010.

And they brought condemnation of the Tories’ -“arrogance” at a time when millions of us are struggling to make ends meet.

Premier tickets for the event cost £1,000 each, or £10,000 for a table. The cheapest seats for less well-heeled Tories are £400 a head or £4,000 a table. Up to 1,200 -people, including regulars Mr Cameron and his wife Samantha, will attend next Monday’s bash in South London, which aims to raise £2million for the Party.

At Prime Minister’s Questions on -Wednesday, Mr Cameron warned the country that it faces a “choppy” ride as it copes with soaring inflation and rocketing fuel and food prices.

Despite this, his friends will glide to the glamorous party in a fleet of limos for drinks ahead of a sumptuous dinner, followed by dancing before their “carriages” arrive at 12.30am.

One of the event’s two chairwomen is Barbara Fink, wife of multi-millionaire hedge fund manager and Tory Treasurer Lord Fink, who has donated more than £1million to the Tories. The party will be held at trendy Battersea Evolution in Battersea Park, which boasts at last year’s event Tories ate “a starter of hand-carved wild Scottish smoked salmon, a main course of thyme roasted fillet of beef, rounded off by a trio of desserts”.

But, aware of the gloom facing the rest of Britain, a senior Tory source insisted: “There will be no champagne. And it’s not a black tie event. People turn up wearing pretty much what they want.”

This year’s party will include the -traditional fundraising auction. At previous events, Tory donors have paid as much as £250,000 to be highest bidder.

This year’s committee members include Dorothy Angest, wife of Swiss banker Henry Angest, -Elizabeth Brooks, wife of investment banker Rory Brooks, and Fiona Cruddas, wife of stockbroker Peter Cruddas.

Film producer Matthew Vaughn and TV personality Trinny Woodall are also on the committee.

Labour MP Michael Dugher -condemned the event. “Now we know why -Cameron and Osborne have reneged on promises to clamp down on bankers’ bonuses,” he said.

“These people caused the global financial crash – it shows how arrogant and out of touch the Tories are.”

[email]vincent.moss@sundaymirror.co.uk
[/EMAIL]

Follow us: @DailyMirror on Twitter | DailyMirror on Facebook
 
Nadhani wewe TOPIC zako saa NYINGINE ni kama VILE haufikirii na HAUISHI NJE ya NCHI na kuelewa kuwa LABOR party na CONSERVATIVE pamoja na kupata pesa toka serikalini bado wanachangisha Wananchama Wao either kwa DINNER PLATE costs maybe 500 pounds...

Au, OBAMA anawachangisha kina J-Z na BEYONCE kwasababu UCHUMI wa USA na UK sio sawa na wa BONGO hatuna Macebrities kama huko; na Hawalazimishwi..

Wewe unaangalia MIKUTANO ya CCM; Wanatoa VYAKULA; Wanatoa Usafiri ; Wanatoa T;SHIRT KHANGA na PIA wanamleta DIAMOND unadhania hiyo ni RUZUKU ya serikali???? CCM inachota kwingine zaidi...

WEWE ANGALIA MIKUTANO YA CCM ni UFUJAJI wa PESA...

1, Wanapewa USAFIRI kwenda kwenye MIKUTANO na T-shirt za CCM nani anapesa za kuchezea kama sio WIZI?

Well explained!
 
Uwezo Likosi katika kufikitia ni mdogo sana, hivi ni nimesahau au lah, kama nimesahau mtanisamehe, hawa CCM si walitoa huduma yao tiwachangie kwa SMS kupitia mitandao ya simu....! Leo Likosi unaiponda CHADEMA kuchangisha fedha kwa wananchi? Usilete mada za kufanya watu wacomment tu na wewe upate umaarufu wa kijinga aisee. Ingekuwa uwezo wangu, mada pumbafu km hizi watu wasicomment. SERUKAMBA.....!
 
Hii ni moja kati ya mada ambazo they lack all depth
Nikupe mfano hai labda unaweza kupata picha kamili:
Rais Obama na chama chake Democratic katika chaguzi zote zilizopita walipitisha bakuli isivyokawaida kufanikisha uchaguzi. Haikutosha uchaguzi tu, ila hupitisha bakuli kila siku kuomba wenye mapenzi mema kuchangia shughuli mbalimbali za chama na miradi ambayo serikali ya marekani haiwezi kugharimia. Wakati taifa kubwa kama hilo linafanya hivyo iweje kwa taifa maskini kama Tanzania. Fahamu kuwa Democratic ndio chama tawala nchini Marekani na Republican chama cha mabepari na makabaila ni chama za upinzani.

Kwa taarifa yako pamoja na mimi kuwepo Tanzania, bado napata email za Democratic kuniomba nichangie chama. Labda ungeanzisha uzi mwingine, lakini hii ya kuchangia chama umeteleza, nimekujibu hivi ikiwa kama njia ya kukushika mkono kukuinua ulipoteleza na urudi kujipanga upya kuleta mada yenye kujenga maudhui yanayoleta maana nzuri na ya kweli.

Njele,
Mpaka leo chama cha Democrat wanaendelea kupitisha bakuli miongoni mwa wale tuliochangia kampeni za Obama. Ingawa kamati ya Obama haiombi tena michango lakini chama, katika mapambano yake na Republicans ambao hawataki kuona Obama akifanikiwa katika sera zake, wanaomba kila kukicha michango angalau hata dola tatu kwa kila aliyechangia kwenye kampeni ya Obama. Kila wiki napata ombi moja au mawili ya kuchangia dola tatu au tano. Nashangaa kuona watu wanashangaa kwamba Chadema inachangisha hela kutoka kwa wafuasi waker. This is democracy at work. And democracy is not cheap. Siyo bure kwamba CCM walikuwa wamezoea kuchota kwenye akaunti zetu bila kurudisha.
 
Lukosi, nilikuambia majuzi kuwa wewe hujui unachokisema (ulifungua thread ya kipuuzi kuhusu maandamano nikakuuliza swali ukasepa). Ingekuwa kina nape wapo makini wangeshakufukuza kwenye chama, you are a liability. Waulize ccm wenzako kama hawachangishi pesa (uliza matembezi ya mshikamano yalikuwa nini na majengo/viwanja vinavyomilikiwa na ccm vilipatikanaje). Ficha ujinga wako kwa kukaa kimya juu ya mambo usiyoyajua!
 
Acheni ushamba, marekani na utajiri wao vyama vyao vinachangisha pesa kwa kingereza inaitws raising money. Marekani ni lazima vyama au mgombea aoneshe ni wspi amepata hela za kampeini ila kwa Tanzania maccm yanachota hela za wizi na kumwaga kwenye campaign zao..so chadema kuchangisha pesa ni sawa sawa kabisa.acheni ushamba na ushabiki wakishamba.
 
Akili za usingizini bhana! Wanavochangisha c.c,m pamoja na ufisadi na vyanzo vyote vya pesa walivo navo huoni,chadema tu ndo unaona,ama kweli 24/7 unaiwaza chadema zaidi hata ya mkeo au nduguzo,no research no right to speak.serukamba
 
Heri ya CDM wanaochangisha wananchi kuliko CCM yako wanaonyang'anya watu kwa nguvu kwani wanawaandikia barua wafanyabiashara ya kuwataka wawape hela kiasi Fulani au wawaharibie biashara zao.Zaidi ya hayo, wanaiba hela za wananchi kwa kutengeneza ufisadi , mfano ule wa EPA ili kugharimia shughuli zao za kisisasa.Hata kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii wanachukua hela lakini kurudisha mmm! hadi mifuko inakaribia kufilisika na hivyokuwacheleweshea malipo wanachama wake. Kama chama chako Lukosi ni mkosi hivi, waambie viongozi wako wajirekebishe na achana na chadema chama kilichokushinda kutokana na kuanzwa kuota magamba kwako.
 
Yes, kuwa successful business man katika project mbali mbali lazima uwe na kitabu cha mahesabu na ufahamu nini maana ya debit & credit. Kwani hujui wahenga walisema mali bila daftali hupotea bila mwenye mali kuwa na taarifa.

Liko wapi hilo daftali la mali inayochangwa kwa hii project?.

Hata kama ni mradi binafsi, lazima uwe na daftali kama ilivyo kwa Democratic ya President Obama.

Kama isivyojulikana kwa majina kwa wale wanaochangia hii project ya CHADEMA na isiwe ndiyo sababu ya kutokuwa na daftali.

This is just small ask but very important

Kama ungekuwa na Akili, ungejiuliza Billion 500 zilizotajwa na Mkaguzi mkuu wa serikali ya CCM, zipo wapi na hayo madaftari yako? Unajua maana ya national debt? Unajua ni kiasi gani sasa hivi? Je unajua kinachangia kiasi gani kurudisha maendeleo ya hao wananchi unaozungumzia? when this UPUMBAVU/UFISADI wa CCM will end ? Hata Mwalimu alichangiwa na wauza maandazi pesa za kwenda UK kudai uhuru, je aliwajua ni mamantilie wangapi? I knew from GEGO, you're smart, but you play FOOL sometime. Please don't get me started
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom