Inasikitisha: Kama Nondo na mbao (Vitu Tangible) vinachakachuliwa na TBS/TFDA wapo, Nina mashaka sana na usalama wa maji ya chupa!

Mkuu dmkali ni kweli kabisa, mimi ni mtumizi wa chuma pia natumia square pipes, ambazo kiurefu zinatakiwa ziwe 600cm, cha ajabu zinakuwa 570cm kwa hiyo tunaibiwa 30cm kila square pipe.
 
wameondoka na futi nzima Astakafilillah
 
Habari ndugu zangu!

Nimefanya ziara/survey katika hardware mbalimbali jijini Dar es salaam kwa ajili ya maandalizi ya material ya ujenzi naotarajia kuufanya hivi karibuni!
Nilichogundua asilimia 95% bidhaa za nondo na mbao hazina urefu unaotakiwa!
nilikuwa na tape measure pamoja na Vernier caliper nikaamua kutumia akili yangu ndogo niliyopata enzi za secondary!
Kwa mujibu Wa TBS na standard ya nondo kimataifa zimewekwa kwa unene tofauti tofauti kulingana na uhitaji Zikitakiwa kuwa na Futi 40 ( zipo 4mm,6mm,....8mm,10mm,12mm,16mm......nakuendelea)

Lakini cha ajabu nilichogundua kutoka kwenye hardware karibu zote wana nondo zenye urefu Wa Futi 37 yaani futi tatu zimeibiwa kwenye kila nondo.
  • kwa maana hiyo kama nondo moja inaibiwa futi 3 ina maana ukinunua nondo 13 unakuwa umeibiwa nondo moja nzima kwahiyo utakuwa sawa na nondo 12 TU
  • Nikaamua kwenda kwenye mbao nazo nI yaleyale; mbao zinazouzwa kuwa ni futi 10 nazo zimechakachuliwa Futi moja haipo, nyingi zina futi tisa tisa tu;
  • nikaamua kuangalia unene Wa nondo; kwa mjibu wa vernier caliper yangu nondo za 16mm baadhi hazikutimia zilikuwa pungufu.
Nimetafakari sana kama Mimi mwananchi Wa kawaida nisiye na utaalamu nimeyaona haya wazi; Hawa TBS na TFDA wanafanya nini hadi bidhaa inatoka kiwandani hadi kufika madukani?
  • Kama TBS wana kitengo cha Inspection viwandani, Je hizo nondo zilizochakachuliwa wao wanashindwaje kuziona ?
  • Kama bidhaa feki hizi zimetapakaa namna hii kuna umhimu gani wafanyakazi wa TBS kulipwa mshahara wakati hawaoni?
Kutokana na hili la Nondo na mbao zinazoonekana kwa macho ya nyama na mikono kushindwa kung'amuliwa na mamlaka tunazozitegemea,

Basi napata mashaka makubwa sana kama mamlaka hizi kama zinasimamia vyema hata ubora Wa maji ya kunywa tunayouziwa kwenye chupa toka kampuni mbalimbali!

  • Bahati mbaya haya yanatokea Wakurugenzi wapo!
  • Bahati mbaya haya yanatokea waziri yupo.
  • Bahati mbaya haya yanatokea viwanda vipo hapahapa nchini lakini havikaguliwi
  • Bahati mbaya haya yanatokea maduka na hardware zote zipo tena mbao na nondo huwa ziko nje lakini hazikaguliwi.
Kama bidhaa zetu zinachakachuliwa, Tusishangae Wageni na wachina wakijenga bongo kwa kuagiza bidhaa toka nchini kwao!

****karibuni****
Sisi tunanunua nondo kwa kilogram na sio kwa urefu. Yani unafika kiwandanibau dukani unawaambia nipe nondo kilo 800.

Hata bomba za GS huwezi kuta yenye 6m net utakuta zenye 5.7 na 5.8m.

Ila kwa uzoefu kidogo... Kama unanunua nondo penda kwenda kiwandani au dealer wa kiwanda husika. Mara nyingi madukan wanauza zile reject materials kutoka kiwandani!!

Mfano, bomba ya PN 10 HDPE ya kiwandan ni tofauti kabisa na za madukani...
 
Nina uzoefu na viwanda vya nondo dar, vinatembelewa na maofisa wa TBS mara kwa mara, cha kusikitisha hua hawaji kukagua ubora/viwango vya nondo bali wao huenda kuchukua pesa na kuondoka.
Hatari sana. .hili taifa ni dampo la rushwa
 
Kwa hiyo Tunaweza kusema kwamba wa tz tunauliwa taratibu?
Thread iliyokwenda sana shule hii.

Mkuu unastahili pongezi za dhati kulifanyia uchunguzi jambo hilo na kubaini uozo uliotamalaki nchini Tz.

Si kwa bidhaa za ujenzi pekee, ni karibia bidhaa zote zinazozalishwa kwenye viwanda vyetu zina figisu mbalimbali!

Ukija kwenye bidhaa za vyakula zinazozalishwa kiwandani ndiyo usiseme!

Mafuta kwenye madumu hupunguzwa ujazo stahiki na sukari kwenye viroba hesabia!

Raia tukipendelea kununua bidhaa import, wanasema hatupendi vya kwetu!

Wakati hayo yakitendeka, waziri pa1 na wasaidizi wake anayeshughulika na viwanda yupo kwenye ofisi za serikali zenye viyoyozi, katinga na miwani mieusi akirotet kwenye viti vya magurudumu, hana mpango!

Jambo hili si geni, linafahamika siku nyingi.

Lakini hakuna hatua yoyote inayochukuliwa, nadhani linaachwa makusudi liendelee kwa ajili ya manufaa binafsi ya wenye viwanda, wafanyabiashara na viongozi ili kunyonya raia.
Zamani hon.
Magufuli alipokuwa akitumbua viongozi 'kabila hiyo' zembe, nilikuwa ninajawa na huruma.

Lakini hivi sasa ninashangilia sana kuona viongozi wa namna hiyo, mumiani wasiojali shida za watu, wakifukuzwa kidhalilishaji hadharani.

.
 
Sisi tunanunua nondo kwa kilogram na sio kwa urefu. Yani unafika kiwandanibau dukani unawaambia nipe nondo kilo 800.

Hata bomba za GS huwezi kuta yenye 6m net utakuta zenye 5.7 na 5.8m.

Ila kwa uzoefu kidogo... Kama unanunua nondo penda kwenda kiwandani au dealer wa kiwanda husika. Mara nyingi madukan wanauza zile reject materials kutoka kiwandani!!

Mfano, bomba ya PN 10 HDPE ya kiwandan ni tofauti kabisa na za madukani...
kwahiyo watanzania wote wakapange foleni kiwandani maduka yafungwe? unazani hizo bodhaa feki hazitoki viwanda hivyohovyo?
Nini maana ya REJECT kupatikana zikiwa dukani?
 
Uzi umeshapata picha au bado?
Jionee bati hiyo inayodaiwa ni futi 10
IMG20190713171141.jpeg
 
Sisi tunanunua nondo kwa kilogram na sio kwa urefu. Yani unafika kiwandanibau dukani unawaambia nipe nondo kilo 800.

Hata bomba za GS huwezi kuta yenye 6m net utakuta zenye 5.7 na 5.8m.

Ila kwa uzoefu kidogo... Kama unanunua nondo penda kwenda kiwandani au dealer wa kiwanda husika. Mara nyingi madukan wanauza zile reject materials kutoka kiwandani!!

Mfano, bomba ya PN 10 HDPE ya kiwandan ni tofauti kabisa na za madukani...
mkuu kwahyo watu wote Tanzania hii tupangane kwenda kiwandani inawezekana kweli? au unadhani wote tunaishi Dar
 
Akili zote zipo CHATO....
Tusubiri 2025 huenda tukaona mabadiliko ya dhati.
 
Habari ndugu zangu!

Nimefanya ziara/survey katika hardware mbalimbali jijini Dar es salaam kwa ajili ya maandalizi ya material ya ujenzi naotarajia kuufanya hivi karibuni!
Nilichogundua asilimia 95% bidhaa za nondo na mbao hazina urefu unaotakiwa!
nilikuwa na tape measure pamoja na Vernier caliper nikaamua kutumia akili yangu ndogo niliyopata enzi za secondary!
Kwa mujibu Wa TBS na standard ya nondo kimataifa zimewekwa kwa unene tofauti tofauti kulingana na uhitaji Zikitakiwa kuwa na Futi 40 ( zipo 4mm,6mm,....8mm,10mm,12mm,16mm......nakuendelea)

Lakini cha ajabu nilichogundua kutoka kwenye hardware karibu zote wana nondo zenye urefu Wa Futi 37 yaani futi tatu zimeibiwa kwenye kila nondo.
  • kwa maana hiyo kama nondo moja inaibiwa futi 3 ina maana ukinunua nondo 13 unakuwa umeibiwa nondo moja nzima kwahiyo utakuwa sawa na nondo 12 TU
  • Nikaamua kwenda kwenye mbao nazo nI yaleyale; mbao zinazouzwa kuwa ni futi 10 nazo zimechakachuliwa Futi moja haipo, nyingi zina futi tisa tisa tu;
  • nikaamua kuangalia unene Wa nondo; kwa mjibu wa vernier caliper yangu nondo za 16mm baadhi hazikutimia zilikuwa pungufu.
Nimetafakari sana kama Mimi mwananchi Wa kawaida nisiye na utaalamu nimeyaona haya wazi; Hawa TBS na TFDA wanafanya nini hadi bidhaa inatoka kiwandani hadi kufika madukani?
  • Kama TBS wana kitengo cha Inspection viwandani, Je hizo nondo zilizochakachuliwa wao wanashindwaje kuziona ?
  • Kama bidhaa feki hizi zimetapakaa namna hii kuna umhimu gani wafanyakazi wa TBS kulipwa mshahara wakati hawaoni?
Kutokana na hili la Nondo na mbao zinazoonekana kwa macho ya nyama na mikono kushindwa kung'amuliwa na mamlaka tunazozitegemea,

Basi napata mashaka makubwa sana kama mamlaka hizi kama zinasimamia vyema hata ubora Wa maji ya kunywa tunayouziwa kwenye chupa toka kampuni mbalimbali!

  • Bahati mbaya haya yanatokea Wakurugenzi wapo!
  • Bahati mbaya haya yanatokea waziri yupo.
  • Bahati mbaya haya yanatokea viwanda vipo hapahapa nchini lakini havikaguliwi
  • Bahati mbaya haya yanatokea maduka na hardware zote zipo tena mbao na nondo huwa ziko nje lakini hazikaguliwi.
Kama bidhaa zetu zinachakachuliwa, Tusishangae Wageni na wachina wakijenga bongo kwa kuagiza bidhaa toka nchini kwao!

****karibuni****
Unaharibia watu mkuu..wanabiashara ndo wanaenjoi hivo wewe hujui
 
Hapo hujaangalia square pipe, flat bar, condult pipe na misumari ndiyo usiseme milaini inapinda kirahisi sana feki tupu
Nimedili na square pipes, flat bars, black pipes, nondo za round nk kwa mda sasa. Ukinunua mfano hizo nondo kutoka kiwandani unapewa specifications ikiwemo urefu na unene wake, zipo nondo za 40ft, lakini pia zipo nondo za 37ft, 38ft. Bei zinatofautiana kwa buku hadi buku tatu. Wanaodanganya ni retailers, wauzaji wa rejareja wanadanganya kuwa nondo, flat bar au Square pipe ina urefu say 20ft kumbe ile Square pipe ina 19'5".

Kwa asilimia kubwa retailers ndio wanasema uongo, ila kiwandani unapewa specifications zote.
 
Back
Top Bottom