Habari ndugu zangu!
Nimefanya ziara/survey katika hardware mbalimbali jijini Dar es salaam kwa ajili ya maandalizi ya material ya ujenzi naotarajia kuufanya hivi karibuni!
Nilichogundua asilimia 95% bidhaa za nondo na mbao hazina urefu unaotakiwa!
nilikuwa na tape measure pamoja na Vernier caliper nikaamua kutumia akili yangu ndogo niliyopata enzi za secondary!
Kwa mujibu Wa TBS na standard ya nondo kimataifa zimewekwa kwa unene tofauti tofauti kulingana na uhitaji Zikitakiwa kuwa na Futi 40 ( zipo 4mm,6mm,....8mm,10mm,12mm,16mm......nakuendelea)
Lakini cha ajabu nilichogundua kutoka kwenye hardware karibu zote wana nondo zilizochakachuliwa zenye urefu Wa Futi 37 yaani futi tatu zimeibiwa kwenye kila nondo.
Basi napata mashaka makubwa sana kama mamlaka hizi kama zinasimamia vyema hata ubora Wa maji ya kunywa tunayouziwa kwenye chupa toka kampuni mbalimbali!
Kama bidhaa zetu zinachakachuliwa, Tusishangae Wageni na wachina wakijenga bongo kwa kuagiza bidhaa toka nchini kwao!
****karibuni****
Nimefanya ziara/survey katika hardware mbalimbali jijini Dar es salaam kwa ajili ya maandalizi ya material ya ujenzi naotarajia kuufanya hivi karibuni!
Nilichogundua asilimia 95% bidhaa za nondo na mbao hazina urefu unaotakiwa!
nilikuwa na tape measure pamoja na Vernier caliper nikaamua kutumia akili yangu ndogo niliyopata enzi za secondary!
Kwa mujibu Wa TBS na standard ya nondo kimataifa zimewekwa kwa unene tofauti tofauti kulingana na uhitaji Zikitakiwa kuwa na Futi 40 ( zipo 4mm,6mm,....8mm,10mm,12mm,16mm......nakuendelea)
Lakini cha ajabu nilichogundua kutoka kwenye hardware karibu zote wana nondo zilizochakachuliwa zenye urefu Wa Futi 37 yaani futi tatu zimeibiwa kwenye kila nondo.
- kwa maana hiyo kama nondo moja inaibiwa futi 3 ina maana ukinunua nondo 13 unakuwa umeibiwa nondo moja nzima kwahiyo utakuwa sawa na nondo 12 TU
- Nikaamua kwenda kwenye mbao nazo nI yaleyale; mbao zinazouzwa kuwa ni futi 10 nazo zimechakachuliwa Futi moja haipo, nyingi zina futi tisa tisa tu;
- nikaamua kuangalia unene Wa nondo; kwa mjibu wa vernier caliper yangu nondo za 16mm baadhi hazikutimia zilikuwa pungufu.
- Flat bar na square pipe zote ziko pungufu!
- misumari nayo ni milaini yaani inapinda kirahisi sana.
- Ebu fikilia siku hizi hadi bajaji au vile vigari viyoriyori/kirikuu vinabeba nondo can you imagine urefu wa futi 40, ikikunjwa futi 20 ikabebwe kwenye chombo kama bajaji yenye futi 5? Obviously nondo zimekuwa fupi thus wanabeba!
- Kama TBS wana kitengo cha Inspection viwandani, Je hizo nondo zilizochakachuliwa wao wanashindwaje kuziona ?
- Kama bidhaa feki hizi zimetapakaa namna hii kuna umhimu gani wafanyakazi wa TBS kulipwa mshahara wakati hawaoni?
Basi napata mashaka makubwa sana kama mamlaka hizi kama zinasimamia vyema hata ubora Wa maji ya kunywa tunayouziwa kwenye chupa toka kampuni mbalimbali!
- Bahati mbaya haya yanatokea Wakurugenzi wapo!
- Bahati mbaya haya yanatokea waziri yupo.
- Bahati mbaya haya yanatokea viwanda vipo hapahapa nchini lakini havikaguliwi
- Bahati mbaya haya yanatokea maduka na hardware zote zipo tena mbao na nondo huwa ziko nje lakini hazikaguliwi.
****karibuni****