Kwanini TCRA hawahakiki ubora wa "Mobile Phone Apps" zinazotumiwa na umma kama ambavyo TFDA na TBS wanavyohakiki bidhaa zingine (tangible products)?

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
15,893
16,317
Shikamooni wakubwa zangu wote wa humu JamiiForums.

Mimi mdogo wenu Infantry Soldier nipo mzima kabisa wa afya.

Thanks to God the Almighty.

Kwanini TCRA hawahakiki ubora wa "Mobile Phone Apps" zinazotumiwa na umma kama ambavyo TFDA na TBS wanavyohakiki bidhaa zingine (tangible products) ingawa nimesikia TBS na TFDA zimeunganishwa na kuwa shirika moja ila sina uhakika mpaka sasa.

Nimeamua kuuliza swali hili kwa maana kwamba katika karne hii ya 21 ya science and technology ni rahisi sana kwa mtu ama kikundi cha watu kuunda hizi Computer/Mobile Phone Apps huku akiaminisha kuwa ni bidhaa njema kwa matumizi ya Mtanzania kumbe akawa na agenda yake ya siri ikiwa ni pamoja na kufanya udukuzi wa taarifa za watu kisha akawa anazituma kwa watu wasio na nia njema na ustawi wa nchi yetu.

Kama TFDA pamoja na TBS wanaweza kufanya ukaguzi wa bidhaa zinazotumiwa na Watanzania (zinazozalishwa ndani pamoja na nje ya nchi) sasa Kwanini TCRA hawakagui hizi "virtual products" ili kuona kama ni sahihi kwa matumizi ya Mtanzania?

===
Schumer wants FBI to investigate FaceApp, DNC warns against using it: Here's what you need to know

People are worried about FaceApp largely because the developer, Yaroslav Goncharov, is based in Russia.

Given Russia’s meddling in the 2016 election, people have a right to be concerned about what it might mean if millions of us are uploading our selfies to foreign servers. After all, pictures are often used for fake profiles or for identity theft.

Still, there’s no evidence yet that Goncharov is anything more than a Russian developer making a fun app. But, even if there is no ill intent, there are very valid fears that photos uploaded to the servers could be shared with foreign governments.

CNBC spoke with FaceApp on Wednesday. The company said the application only uploads the picture you want to edit, and it only holds most pictures for 48 hours. While there’s no proof the photo is actually deleted, security experts like Will Strafach, who goes by Chronic on Twitter, have confirmed that just the picture — and not your whole photo library — is uploaded when you use the app:

Yes, FaceApp owns that photo after you upload it, but other companies, like Snapchat, have similar terms when you post public images and video to its app. But we only have the developer’s word to go by, and there’s no way for consumers to ask that their pictures be deleted permanently.
And that’s what has a lot of people worried.

Source: CNBS

===
Maoni ya wadau
Wenzetu EU wana General Data Protection Act GDPR ambayo ni lazima mtengenezaji afuate masharti yake ya kulinda taarifa za watumiaji ili app/mfumo/huduma yake inayokusanya na/au kuhifadhi taarifa binafsi iweze kutumika ndani ya nchi za Europian Union, au wananchi wa Europian Union popote pale walipo.

Ukiikiuka hiyo na kugundulika kwenye audit zao madhara yake ni bonge la fine au/na kufungiwa kama sikosei.

TCRA wanaweza wakasema waiadopt hiyo kwa hapa Tanzania on top of sheria ya mitandao, but changamoto ya sheria yoyote ile ni kuhakikisha inafuatwa, enforcing it. Sheria kama hizo zipo kwa ajili ya data za financial institutions kama banks ndo maana utasikia every while bank kadhaa zinapigwa fine mfano kwa kutunza data katika server zilizo nje ya ardhi ya Tanzania.

Kukagua huduma zote na apps zote kutahitaji manpower ya kitaalamu kubwa sana na hibyo fedha nyingi sana.

Swali la kujiuliza ni je, TCRA na serikali kwa ujumla inajali usalama wa data binafsi za wananchi zilizomo mikononi mwa watoa huduma za kimtandao kiasi cha kukagua mifumo yao kuhakikisha data hizo hazitumiii vibaya?

Kwa Android Apps hupakuliwa kwenye Google Play Store, or at least ni inatakiwa zipakuliwe kutoka kwenye Google Play Store, yenyewe Play Store ina feature inaitwa Play Protect.

Means kila App ambayo ipo Play Store ni imeonwa na Play Protect kuwa ni inafaa in terms ya privacy mpaka virus.

Ukidownload App kutokea kwenye Website nyingine na huku Play Protect umeiactivate hiyo App haitakaa.

Kwa hapo sioni kama TCRA wana kazi ya kupima 'ubora' wa App.

Na hata tukija kwenye suala ya kwamba kuna Apps zinavujisha data za mtumiaji au zinatunza data zako bila kujua naona TISS na kitengo cha Cyber Crimes cha Polisi kina kazi hiyo zaidi kuliko TCRA.

Ndiyo maana hata screenshot ya huu uzi inaonyesha ni FBI ndiyo wanatakiwa kuchunguza FaceTime App, unless bodi yao ya mawasiliano ipo ndani ya FBI basi nilichoandika kitakuwa ni komedi.
 
Watasemaje App A ni bora kuliko B, kigezo ni kipi? Na wakisema A ni bora tutajuaje kama sio abuse of power ili kuwapigia upatu hao watu.

Users ndio wanachagua kipi ni bora, ukizingatia Apps nyingi ni bure wateja wenyewe ndio wanaamua na kupata kwako wateja au kukosa ni through word of mouth ukileta upupu sokoni utatoka tu kwenye soko wala haiitaji kutolewa na taasisi.

Pia kumbuka hata kina Microsoft huwa wakitoa bidhaa inakuwa na bugs kibao na matatizo ambayo wanaboresha kutokana na muda na feedback ya wateja ndio maana huwa kuna BETA version na versions nyingi nyingi kila baada ya muda.
 
Wakisema A ni bora tutajuaje kama sio abuse of power ili kuwapigia upatu hao watu.
Kuna ushindani mkubwa sana wa kibiashara baina ya Coca Cola na Pepsi hapa Tanzania. Kama TBS haijawahi kupigia upatu moja kati ya pande hizo mbili, kwanini unaamini ya kwamba TCRA wanaweza kiwapigia upatu washindani wa kibiashara wa Mobile Phone Apps?
 
Kwanini wanatumia kigezo kipi kusema ya kwamba soda ya Coca Cola na Pepsi zote zinafaa kwa matumizi ya Watanzania?
Wanapima kama kilichomo ni sumu, sasa idea au kitu kinachosaidia au entertainment utapima kwa kigezo gani? Mfano jembe linalomsaidia mtu anayelima kwa vidole utapima vipi kwamba halifai, hata kama sio bora kama tractor ila linaongeza ufanisi kuliko vidole na huyo anayepima ana ujuzi au ufahamu kuliko mtumiaji au aliyetengeneza? Au mtu anayetunga kitabu cha hadithi ni vipi unaweza kusema hadithi yake haina viwango.
 
Wanapima kama kilichomo ni sumu, sasa idea au kitu kinachosaidia au entertainment utapima kwa kigezo gani?
Mobile App inaweza kuwa ni sumu kwa kifaa cha mawasiliano cha Mtanzania. It might be embedded with malicious programs in the background.
 
Kuna ushindani mkubwa sana wa kibiashara baina ya Coca Cola na Pepsi hapa Tanzania. Kama TBS haijawahi kupigia upatu moja kati ya pande hizo mbili, kwanini unaamini ya kwamba TCRA wanaweza kiwapigia upatu washindani wa kibiashara wa Mobile Phones Apps?
Duh, kazi ipo. kKna soda aina ngapi (na pepsi au coca wakiweka sumu ambazo ni mbovu ni rahisi kujua) ndio maana nikakupa mfano unajua Windows ilivyotoka ilikuwa ina bugs kiasi gani? Je tungesema isiingie sokoni? au freewares na sharewares zikitoka tuseme zisitoke wakati kutoka kwake na watu kutoa feedback ni part of process ya kuboresha.
 
Jembe linalomsaidia mtu anayelima kwa vidole utapima vipi kwamba halifai.
Jembe linapimwa ubora kuona kama materials zilizotumika (chuma) zinaweza kustahimili kupasua udongo kwa muda gani? Au ule mpini (mbao) unafaa kutumiwa na mkulima pasipo kumchubua mikono?
 
Wenzetu EU wana General Data Protection Act GDPR ambayo ni lazima mtengenezaji afuate masharti yake ya kulinda taarifa za watumiaji ili app/mfumo/huduma yake inayokusanya na/au kuhifadhi taarifa binafsi iweze kutumika ndani ya nchi za Europian Union, au wananchi wa Europian Union popote pale walipo.

Ukiikiuka hiyo na kugundulika kwenye audit zao madhara yake ni bonge la fine au/na kufungiwa kama sikosei.

TCRA wanaweza wakasema waiadopt hiyo kwa hapa Tanzania on top of sheria ya mitandao, but changamoto ya sheria yoyote ile ni kuhakikisha inafuatwa, enforcing it. Sheria kama hizo zipo kwa ajili ya data za financial institutions kama banks ndo maana utasikia every while bank kadhaa zinapigwa fine mfano kwa kutunza data katika server zilizo nje ya ardhi ya Tanzania.

Kukagua huduma zote na apps zote kutahitaji manpower ya kitaalamu kubwa sana na hibyo fedha nyingi sana.

Swali la kujiuliza ni je, TCRA na serikali kwa ujumla inajali usalama wa data binafsi za wananchi zilizomo mikononi mwa watoa huduma za kimtandao kiasi cha kukagua mifumo yao kuhakikisha data hizo hazitumii vibaya?
 
Mtu anayetunga kitabu cha hadithi ni vipi unaweza kusema hadithi yake haina viwango.
Absolutely. Kitabu cha hadithi kinaweza kupigwa marufuku kama kinabeba maudhui ya uchochezi ama uvunjifu wa sheria na taratibu za nchi husika
 
Swali la kujiuliza ni je, TCRA na serikali kwa ujumla inajali usalama wa data binafsi za wananchi zilizomo mikononi mwa watoa huduma za kimtandao kiasi cha kukagua mifumo yao kuhakikisha data hizo hazitumii vibaya?
Hili pia ni swali zuri sana mkuu. Thanks so much
 
Wenzetu EU wana General Data Protection Act GDPR ambayo ni lazima mtengenezaji afuate masharti yake ya kulinda taarifa za watumiaji ili app/mfumo/huduma yake inayokusanya na/au kuhifadhi taarifa binafsi iweze kutumika ndani ya nchi za Europian Union, au wananchi wa Europian Union popote pale walipo.

Ukiikiuka hiyo na kugundulika kwenye audit zao madhara yake ni bonge la fine au/na kufungiwa kama sikosei.

TCRA wanaweza wakasema waiadopt hiyo kwa hapa Tanzania on top of sheria ya mitandao, but changamoto ya sheria yoyote ile ni kuhakikisha inafuatwa, enforcing it. Sheria kama hizo zipo kwa ajili ya data za financial institutions kama banks ndo maana utasikia every while bank kadhaa zinapigwa fine mfano kwa kutunza data katika server zilizo nje ya ardhi ya Tanzania.

Kukagua huduma zote na apps zote kutahitaji manpower ya kitaalamu kubwa sana na hibyo fedha nyingi sana.

Swali la kujiuliza ni je, TCRA na serikali kwa ujumla inajali usalama wa data binafsi za wananchi zilizomo mikononi mwa watoa huduma za kimtandao kiasi cha kukagua mifumo yao kuhakikisha data hizo hazitumiii vibaya?
Asante sana kwa ufafanuzi wako mwanana. Hakika umefafanua kwa kina sana
 
Hiyo sio kazi ya TCRA tu bali vyombo vyote vya TISS n.k. as well as some antivirus and anti-trojans companies TCRA pekee haina huo uwezo.
Kwa hiyo unataka TCRA ishirikiane na hizo companies za antivirus ilihali wao ndio washukiwa wakubwa wanaopaswa kidhibitiwa na serikali?
 
Kwa hiyo unataka TCRA ishirikiane na hizo companies za antivirus ilihali wao ndio washukiwa wakubwa wanaopaswa kidhibitiwa na serikali?
Mkuu naona umeamua kupoteza muda wangu, hivi unajua kuna code milioni ngapi kwenye software ndogo tu? Na ndio maana nikakuuliza swali unajua hata kina Microsofts yenye technical na funds za kutengeneza software hata wakitoa kazi yao huwa zina bugs za kutosha (sio kwa kutaka bali kwa ugumu wa kazi).

Na bugs hizo huwa zinarekebishwa kadri mda unavyokwenda, tukija kwenye viruses nk. ndio maana kuna antivirus za kutosha na hapo bado hacking na udukuzi unaendelea mpaka kesho, ndio maana kina HBO walidukuliwa pia (the only way sio kwa kitengo fulani kucheki kila app inayoingia sokoni.., bali ni kuwa na kinga (anti virus n.k.) inayoweza kuzuia vitu kama hivyo, ili mwisho wa siku mtu akiweza kudua wakati una kinga utaweza kumuuliza kwanini imetokea au kumfanya akawa responsible.

Ndio maana watu hutumia condom kukinga magonjwa ya zinaa na sio kwanza kutibu kila prostitute aliyekuwepo ili kuhakikisha kwamba hawapati magonjwa ya zinaa. One is realistic and practical another is just a pipe dream.
 
Back
Top Bottom