Inashangaza sana hii

BioPsychologist

JF-Expert Member
Aug 23, 2017
724
1,014
Wakuu bila shaka hamjambo! sihitaji kupoteza muda wenu ngoja niende kwenye mada.

Katika kitaa nachokaa kuna mshikaji mmoja ni mtu wa kuchukua sana wadada haijarishi ni aina gani yaani jamaa ni okota okota, sasa majuzi fulani hivi akanambia kuna mdada anawasiliana nae yuko Mbeya anataka kuja, huyo dada walionana mtandaoni FB.

Siku tatu baadae jamaa akapata ajari na kuumia mguu wakati naenda kumcheki akanambia man yule duu anakuja leo yuko safarini naomba uende jioni kumpokea Ubungo. Dah! Nikashangaa kwanza nikamuuliza mlishaonana hata siku moja akajibu No! Basi nikasema sio mbaya nitaenda kumchukua.

Hadi inafika saa 2 usiku akasema wamepoteza mawasiliano so mimi nikaenda zangu getto. Asubuhi ananipigia simu kuwa mgeni kafika sema kweli nimeshangaa sana demu kaja ila ni mkubwa kiumri kuliko mshikaji. Mshikaji kapagawa hatari anavumilia lakini ina muuma vibaya mno.

Demu katulia na furaha za kumwaga, sasa kutokana na kuuguza majeraha jamaa kapata point ya kuto fanya nae sex.

Nimesikitika sana hadi sasa najiuliza huenda watu wa namna hii ni wengi, yaani unatoka Mbeya hadi Dar kwa mtu usiomfahamu na yeye hakufahamu.

Nasikiaga watu wanapotea ghafla na kusahaulika kumbe sometimes huwa ni uzembe, mfano jamaa asingekuwa mtu salama huyu Dada angeishia wapi na hapa Dar hana ndg wala jamaa?

Mnisaidie kutafakari wakuu!
 
We ni mwanasaikolojia then tena unatuuliza sisi kwani hujui tabia za watu..?

Hivyo ndivyo walivyo ndugu kuna watu wanaweza take risk bila kuwa na maswali ya why,when and how!… Lkn pia watu wanamipango ndugu usione tu kiumbe kimetoka kilipotoka ukafikiri ndo hivyo tu! There's dark side which we don't know!.. licha ya kuwa na masimulizi yanayotuonya but hiyo haitoshi kutuzuia personality zetu..

Tabia zina nguvu kushinda elimu.
 
Daah hii story ya jamaa yako nilikuwa na tabia hizo enzi hizo hata whatsapp haijawa mashuhuri, siku moja natokea bahari beach nakaribia kwenye lile bumps la pale jeshini mara simu ikaita kupokea, sauti ya kike sijui anamtafuta nani, nikamwambia aisee utakuwa umekosea namba.

Akaomba radhi akakata, ila alikuwa na sauti nzuri kinoma, baadae akanitumia msg nikachat naye akasema yuko mbeya sijui anafanya kazi CRBD mimi nikamwambia niko dar, mara aksema atakuja dar ila sasa mimi nilikuwa nampotezea potezea maana nilikuwa na mambo mengi.

Ila baada ya muda nikajikuta nachat naye kila siku, basi siku aliyosema atakuja dar ikafika akaomba nikampokee jioni, nikaenda ubungo kumpokea simjui hanijui, niko nashangaa shangaa ananielekeza kwenye simu muda huo usiku saa mbili hivi demu namuona lakini siamini kama ndiye maana nilivyokuwa na muimagine sivyo, demu allikuwa mkubwa zaidi yangu halafu Mungu anisamehe ila hana mvuto yupo kama bibi.

Ila nikafanya uungwana tu nikampokea tukiwa kwenye gari yeey anaongea sana anacheka akataka nipige deep kiss nikakwepesha mdomo, nikampeleka nyumba ya wageni, nikamwambia narudi sikurudi tena kesho yake nikamwambia aisee nina safari ya ghafla nasafiri.

Nilikoma hizo mambo kabisa.
 
Me mbona kuna demu alitoka tanga week jana amekaa siku nne hapa nyumbani nilikua simjui tumeonana tu mtandaoni
Trustworthy sio kawaida kuna kitu kinakuwa kina endesha uhusiano huo ! Hasa wadada wetu hawa gap limebana sana LA kuolewa ndo maana
 
Dunia imebadilika watu kukutana online sio kitu kipya
Muhimu fanya verification ya mtu
Zungumzeni Kwa video call kwanza
 
Nyie endeleeni tu kutafakari...nipo busy na siku ya wanywa bia duniani.
 
We ni mwanasaikolojia then tena unatuuliza sisi kwani hujui tabia za watu..?

Hivyo ndivyo walivyo ndugu kuna watu wanaweza take risk bila kuwa na maswali ya why,when and how!… Lkn pia watu wanamipango ndugu usione tu kiumbe kimetoka kilipotoka ukafikiri ndo hivyo tu! There's dark side which we don't know!.. licha ya kuwa na masimulizi yanayotuonya but hiyo haitoshi kutuzuia personality zetu..

Tabia zina nguvu kushinda elimu.
Kuhusu tabia nafahamu lakini sio kila incidence inaangukia psychological output kuna mengine yanahitaji ujuzi nje na nilionao ndo nithibitishe.
 
Daah hii story ya jamaa yako nilikuwa na tabia hizo enzi hizo hata whatsapp haijawa mashuhuri, siku moja natokea bahari beach nakaribia kwenye lile bumps la pale jeshini mara simu ikaita kupokea, sauti ya kike sijui anamtafuta nani, nikamwambia aisee utakuwa umekosea namba. Akaomba radhi akakata, ila alikuwa na sauti nzuri kinoma, baadae akanitumia msg nikachat naye akasema yuko mbeya sijui anafanya kazi CRBD mimi nikamwambia niko dar, mara aksema atakuja dar ila sasa mimi nilikuwa nampotezea potezea maana nilikuwa na mambo mengi.
Ila baada ya muda nikajikuta nachat naye kila siku, basi siku aliyosema atakuja dar ikafika akaomba nikampokee jioni, nikaenda ubungo kumpokea simjui hanijui, niko nashangaa shangaa ananielekeza kwenye simu muda huo usiku saa mbili hivi demu namuona lakini siamini kama ndiye maana nilivyokuwa na muimagine sivyo, demu allikuwa mkubwa zaidi yangu halafu Mungu anisamehe ila hana mvuto yupo kama bibi.
Ila nikafanya uungwana tu nikampokea tukiwa kwenye gari yeey anaongea sana anacheka akataka nipige deep kiss nikakwepesha mdomo, nikampeleka nyumba ya wageni, nikamwambia narudi sikurudi tena kesho yake nikamwambia aisee nina safari ya ghafla nasafiri.
Nilikoma hizo mambo kabisa.
Hata huyu ni kama mbibi kwa jamaa japo mapenzi hayana umri
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom