Kheri ya mwaka mpya wana JF wote! Hii ndio habari ya kusikitisha baada ya msanii Young D kusemekana kurudia kubwia unga! Hii ni baada ya meneja wake Max kuonekana akichat na dada fulani kuhusu ishu hiyo kwenye mtandao wa Instagram.
Kwa mujibu wa meneja wa Young Dee, Maximillian Rioba, rapper huyo amerejea tena kwenye matumizi ya dawa za kulevya.
Max anadai amejaribu kila awezalo, lakini sasa ameamua kunawa mikono Amezitoa taarifa hizo Instagram alipokuwa akichat na msichana aitwaye Wendy Eliah.
Kila kifo kinapangwa na Mungu ila hivi vya madawa ya kulevya vinapangwa na shetani, acha wafe tu ili wengine wajifunze, wasiokufa hakuna mtu atakayejifunza kuwa madawa ya kulevya ni hatari.
Hii staili ya kuacha unga ya wasanii ndio uwa inanishangaza.. Unaachaje unga kirahisi hivyo!
Wasanii wetu wakae wakijua unga hauna mjanja.. Unga ata uufiche vipi kuna siku utakuumbua tu... Tunasubiri wajanja kina Mr blue, TID, Babuu, Mox, Majani, Bushoke ,Q chilla nk tuuone mwisho wao .
Btw hivi Tippo wa Zizu yupo wapi? Ana dhambi nyingi sana huyu jamaa.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.