Inasemekana Waafrika wawili akiwemo Mtanzania Nemes waliofariki vitani wakipigania upande wa Urusi walikuwa wanafunzi

Troublemaker

JF-Expert Member
Jun 8, 2015
19,905
38,560
Familia ya Mtanzania Nemes Raymond Tarimo (34) ambaye ameripotiwa kufariki wakati akipigana upande wa Jeshi binafsi la Urusi la Wagner Group dhidi ya Ukraine, imesema haifahamu ni nini kimempata Kijana wao hadi kufariki kwakuwa wanachokifahamu wao ni kwamba Nemes alikuwa anasoma Urusi na wameshangaa kuona akiagwa kijeshi.

Video ambayo imesambaa mitandaoni inawaonesha Wapiganaji wanaominika ni kutoka Wagner Group wakimuaga Nemes Tarimo ambapo amepewa pia nishani baada ya kudaiwa kufariki vitani katika shambulio la Bakhmut Mkoa wa Donbas mashariki mwa Ukraine.

Mjomba wa Nemes, Andrew Mwandenuka akiongea nyumbani kwa Familia ya Nemes Dar es salaam leo, amesema Ubalozi wa Tanzania nchini Urusi umeiambia Familia kuwa mwili wa Nemes utakapofikishwa Tanzania wataelezwa ni nini kimempata Kijana wao.

Jitihada za kuupata Ubalozi wa Tanzania katika Shirikisho la Urusi ili kupata taarifa za tukio hili hazijafanikiwa huku Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ukisema unalifanyia kazi suala hilo.

Yapo madai ambayo hayajathibitishwa yanayodai Nemes alifungwa Jela na baadaye alipewa nafasi ya kutoka jela kwa sharti la kujiunga na Jeshi hilo lakini Familia inasema haina taarifa za kwamba Nemes alifungwa wala kujiunga na Jeshi na inachokifahamu ni kwamba alikuwa Mwanafunzi.

chanzo👇
#MillardAyoUPDATES
 
Russian never die in vain. We see their graves in Africa and till today they are well preserved. But where is your great grandmother or grandfather grave?

They die exploiting Africa. They are dyin fucyking the mother land 😔 😔
You mean to say it's Russian's responsibility to preserve our great grandparents graves (tombs)?
 
https://www.tandfonline.com/doi/abs/10.1080/14682740701284157
https://www.ajol.info/index.php/smsajms/article/view/48743/35095
Africa–Soviet Union relations - Wikipedia
Training haina maana ya kupigana hadi kufia vitani. Training nyingi zilikuwa zinafanyikia huko huko Urusi, yaani wapigania Uhuru walikuwa wanakwenda huko kupata mafunzo ya kijeshi.

Halafu USSR ilikuwa ni pamoja na nchi za Urusi, Ukraine, Georgia, Armenia, estnia, latvia, Lithuania, Belarus, Kyrgystan na nchi nyingezo, haikuwa Urusi tu.
 
Training haina maana ya kupigana hadi kufia vitani. Training nyingi zilikuwa zinafanyikia huko huko Urusi, yaani wapigania Uhuru walikuwa wanakwenda huko kupata mafunzo ya kijeshi.

Halafu USSR ilikuwa ni pamoja na nchi za Urusi, Ukraine, Georgia, Armenia, estnia, latvia, Lithuania, Belarus, Kyrgystan na nchi nyingezo, haikuwa Urusi tu.
Mkuu ngoja niishie hapo nilipofikia maana yaonesha hujui mengi yaliyo kuwa yanaendelea wakati huo.
Kusema kufundisha askari ilikuwa lugha nzuri hadharani ili kuwa na ile plausibe deniability just in case .....
Lakini nyuma ya pazia jamaa walikuwa frontline na guerilla fighters wa Namibia na kwingineko, wapo waliofia vitani. Jaribu kutafuta taarifa zaidi kwa faida yako.
 
Back
Top Bottom