Inasemekana Waafrika wawili akiwemo Mtanzania Nemes waliofariki vitani wakipigania upande wa Urusi walikuwa wanafunzi

Familia ya Mtanzania Nemes Raymond Tarimo (34) ambaye ameripotiwa kufariki wakati akipigana upande wa Jeshi binafsi la Urusi la Wagner Group dhidi ya Ukraine, imesema haifahamu ni nini kimempata Kijana wao hadi kufariki kwakuwa wanachokifahamu wao ni kwamba Nemes alikuwa anasoma Urusi na wameshangaa kuona akiagwa kijeshi.

Video ambayo imesambaa mitandaoni inawaonesha Wapiganaji wanaominika ni kutoka Wagner Group wakimuaga Nemes Tarimo ambapo amepewa pia nishani baada ya kudaiwa kufariki vitani katika shambulio la Bakhmut Mkoa wa Donbas mashariki mwa Ukraine.

Mjomba wa Nemes, Andrew Mwandenuka akiongea nyumbani kwa Familia ya Nemes Dar es salaam leo, amesema Ubalozi wa Tanzania nchini Urusi umeiambia Familia kuwa mwili wa Nemes utakapofikishwa Tanzania wataelezwa ni nini kimempata Kijana wao.

Jitihada za kuupata Ubalozi wa Tanzania katika Shirikisho la Urusi ili kupata taarifa za tukio hili hazijafanikiwa huku Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ukisema unalifanyia kazi suala hilo.

Yapo madai ambayo hayajathibitishwa yanayodai Nemes alifungwa Jela na baadaye alipewa nafasi ya kutoka jela kwa sharti la kujiunga na Jeshi hilo lakini Familia inasema haina taarifa za kwamba Nemes alifungwa wala kujiunga na Jeshi na inachokifahamu ni kwamba alikuwa Mwanafunzi.

chanzo👇
#MillardAyoUPDATES
Mfungwa
 
Nilikuwa nimeshakomaa wakati wa harakati za uhuru wa kusini mwa Afrika. Wakati Eduardo Mondlane anauwawa tulifunga shule na kwenda kuandamana kupinga ugaidi huo. Siyo mtu wa kusimuliwa ukizingatia kuwa tulikuwa bado ndani ya ujamaa tukiwa tunapinga ubeberu. Tuishafukuza Ubalozi wa Marekani nchini kwetu; kwa hiyo hakukuwa na siri ya majeshi ya Urusi kuwapo nchini yasijulikane.

Ni jeshi la Cuba tu ndilo lilikwenda kumsaidia Neto kupigana na UNITA ambayo ilikuwa inasaidiwa na Marekani. Urusi haijawai kuwa na jeshi lake Afrika. Hata huko Afrika ya Kati miaka ya hivi karibuni walipeleka jeshi la Wagner, siyo jeshi la Urusi lenyewe!
Unampinga bure mkuu, ni kweli warusi walikuwepo na kuna kuna kambi zao bongo pia..niishie hapo utakua umeelewa.
 
Taifa kama Tanzania ili liwe salama lazima liwe na vijana kama huyo na yumkini wapo wengi "undercover" vitani sehemu nyingine duniani.

Kama ubalozi umesema utatoa taarifa kwa familia mwili ukifika inatosha. Familia nayo iwe sikivu kwa ubalozi kijana azikwe na nishani ya ushujaa. Pumzika kwa amani mzalendo wetu.

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
Shujaa kuwa anampigania nani?
 
Back
Top Bottom