usiendesema
Member
- Feb 5, 2019
- 10
- 7
Habari wana jamvi:
leo tena nimekuja na jambo hili linaloniumiza moyo sana lakini sina namna ya kuepukana nalo.
Mimi ni kijana wa kiume,
Nina rafiki yangu wa kiume tuliyodumu katika urafiki wetu huo zaidi ya miaka kumi sasa,
Tulikutana katika maisha ya kawaida yeye akiwa mwalimu wa shule ya awali nami nikiwa mfanyabiashara.
Tulizoeana na baadae tulikubaliana kuwa marafiki na ilikua hivyo kwa muda wa miaka mingi.
Baadae alishindwa kuendesha shule yake na akapitiwa na wakati mgumu kimaisha,
Niliamua kumshirikisha katika biashara nilizokua nikifanya.
Nilithubutu kumpa pesa akafuate mzigo huko nilikokua ninafuata mkoani,
Alifanya uadilifu kipindi hicho kiasi kwamba nilishawishika kumkatia baadhi ya mzigo na nilimpa ili naye aanze kuzungusha kwa mahitaji yake.
Tuliendelea hivyo na baadae nilibuni biashara nyingine iliyohitaji kusafiri nchi jirani na nilimpa pesa akalete mzigo .
Alisafiri tukiwa tunawasiliana muda wote alipokua safarini na hata alipomaliza kukusanya mzigo , na alinifahamisha kuwa anaanza safari ya kurudi kesho yake .
Tangu hapo sikumpata tena zilipita siku nne hivi nisikia simu yangu ikiita nilipoangalia nikaona jina la rafiki yangu.
Nilipopokea nikasikia sauti ya like akaniuliza unamfahamu mwenye simu hii nikamjibu ndiyo akanambia amepata ajali na amezimia leo siku ya tatu.
Niliwaza kumfuata yule nesi alinambia vumilia akizinduka nitakupa uongee naye laa ikishindikana kesho tutampakia kumleta dar muhimbili.
Ilipofika jioni akizinduka na niliongea naye kwa kwa taabu sana walimsafirisha kwa nia ya kumleta dar lakini walipofika shinyanga walimpeleka hsptl kahama na kupitiwa matibabu.
Kilichonishangaza alinambia amevunjika mguu na mkono ila lakini baada ya wiki alikuja dar huku akiwa na p,o,p mguuni na mkononi ila alikua ulikanyaga huku ameshikiria fimbo.
Alinambia mzigo wote umeibiwa nilikubali kwani sikumtilia shaka , baada ya siku chache alisafiri kwao akarudi
baada ya mwezi akiwa mzima wa afya .
Baadae tutaendelea na biashara ya kusafiri ndani ya nchi huko mkoani , mimi nikiwa dar alinipa taarifa kwamba mkoa umezuia kusafirisha biashara hiyo mpaka taratibu zitakapotangazwa upya .
Mpaka wanafika wilaya tuliyohifadhi mzigo wetu kibali na leseni zetu zilikwisha muda wake na mzigo wetu ulitaifishwa pia nilikubali matokeo.
Kinachoniuma zaidi baada ya kufuatilia zaidi niligundua alinifanyia kamchezo na alifanikiwa kunidhurumu.
Si hivyo tu pamoja na maisha yangu kuwa magumu amekua si wa kunijali pamoja na kujua magumu ninayopitia na unafuu alionao kwa sasa .
Na amekuwa akinifanyia mambo ya nguvu zisizoonekana nia yake ikiwa ni kufanya niwe na maisha magumu naye awe juu yangu kiuchumi, na hilo nahisi amelifanikisha kwa kiasi kikubwa.
Pamoja na yeye kuwa na pesa hata nilipomuomba aniazime ili nijikwamue akinijibu hana ila ananitia moyo na kuniambia atajitahidi kuniazimia kwa jamaa zake lakini bila ya mafanikio.
Na badala yake anaponikuta hunipa elfu 20 au 30 kiasi kwamba hakiwezi kukidhi mahitaji yangu nisaidieni wana jamvi nini nifanye niepukane na huyu mtu.