Inaniuma hasa wanaoenda kwa TB Joshua

Inaniuma hasa wanaoenda kwa TB Joshua

DIKACY

Member
Joined
Oct 7, 2013
Posts
23
Reaction score
7
Habari wapendwa,kuna kitu kinanikera mpaka nimeamua kuongea na inabidi tumuogope Mungu,kuna jamaa mmoja alioa akafukuza mke wake,badae akamrudia mke wake Mungu akawajalia mtoto mmoja,wakati huyo mke ana mimba jamaa akachepuka bahati mbaya mchepuko ukapata ujauzito,jamaa akachanganyikiwa kwa sababu aliuambia mchepuko hana mke yani walishaachana,sasa jamaa akakimbilia nigeria kwa TB Joshua ili aambiwe nani mke kutoka kwa Mungu wakati mke wa kwanza alifunga nae ndoa,baada ya jamaa kurudi akatulia ndani ya miezi 6 huku akimuomba Mungu amuonyeshe,wiki 2 zilizopita kasema Mungu kamuonyesha mchepuko ndio mke wake,ila nigeria hakuambiwa kitu,sasa kwa mke halali hataki kupasikia wala habari za mtoto.
 
Umeamua kumsema tu TB Joshua, sioni uamuzi wa jamaa yako unamhusisha vipi Joshua. Halafu hata kuandika tu unapata shida, au upo kwenye bodaboda katikati ya jiji?
 
TB Joshua hahusiki hapa jamaa mwenyewe ndo kamuomba Mungu wake mimi na wewe hatujui anamwabudu Mungu gani anaetoa mwongozo hadi kwenye michepuko

Umeongea kweli mkuu hata mimi nakuunga mkono.
 
TB Joshua hahusiki hapa jamaa mwenyewe ndo kamuomba Mungu wake mimi na wewe hatujui anamwabudu Mungu gani anaetoa mwongozo hadi kwenye michepuko

Mkuu kula like umempa jibu zuri.Mungu wa kuchagua michepuo atakuwa Mungu ni yule aliepotea na ndege ya malasia kwa maana yeye ni wa fujo.
 
kahabari kakutunga haka.,
anyway,, hapo hakuna cha Tb joshua wala nin! Huyo jamaa ni mzinzi tu.
 
Mkuu kula like umempa jibu zuri.Mungu wa kuchagua michepuo atakuwa Mungu ni yule aliepotea na ndege ya malasia kwa maana yeye ni wa fujo.

hahaha eti mungu wa fujo, ustadhat umenifurasha sana
 
jamaa akakimbilia nigeria kwa TB Joshua ili aambiwe nani mke kutoka kwa Mungu

baada ya jamaa kurudi akatulia ndani ya miezi 6 huku akimuomba Mungu amuonyeshe,

wiki 2 zilizopita kasema Mungu kamuonyesha mchepuko ndio mke wake,ila nigeria hakuambiwa kt

TB Joshua anahusika vipi na maamuzi ya huyo mwanaume?

Kuna watu mnaongea au kuandika Kiswahili kwa kuwa tu mnaishi Tanzania, lakini reasoning zenu ni mbovu hakuna kifani
 
Watu mna mambo jamani,TB joshua kala za macho bila makosa
 
Habari wapendwa,kuna kitu kinanikera mpaka nimeamua kuongea na inabidi tumuogope Mungu,kuna jamaa mmoja alioa akafukuza mke wake,badae akamrudia mke wake Mungu akawajalia mtoto mmoja,wakati huyo mke ana mimba jamaa akachepuka bahati mbaya mchepuko ukapata ujauzito,jamaa akachanganyikiwa kwa sababu aliuambia mchepuko hana mke yani walishaachana,sasa jamaa akakimbilia nigeria kwa TB Joshua ili aambiwe nani mke kutoka kwa Mungu wakati mke wa kwanza alifunga nae ndoa,baada ya jamaa kurudi akatulia ndani ya miezi 6 huku akimuomba Mungu amuonyeshe,wiki 2 zilizopita kasema Mungu kamuonyesha mchepuko ndio mke wake,ila nigeria hakuambiwa kitu,sasa kwa mke halali hataki kupasikia wala habari za mtoto.

Du!kumbe mtu unaweza kujeruhiwa humu ukikosea ukamtaja vibaya TB Joshua.
 
huyo ni muhuni kama wahuni wengine wa buguruni na mazese hana cha ulokole huko kwa TB Joshua alienda kutaliii tu.
 
Jamani sijamlaum TB Joshua,ndio maana nikasema jamaa alivyoenda nigeria hakuambiwa kt na TB Joshua,zaid ya kuombewa kwenye prayer line,sasa nan kasema TB Joshua mkosaji?nimeandika kuonyesha mtu alivyoenda kuombewa kwamba hakua serious na si kumsema vby TB JOSHUA,helewen mada.
 
Hawa ndo walokole wa hiki kizazi. Wanatanguliza tamaa zao baadae wanampachika Mungu, Ni wachafu afadhali hata wasiomjua Mungu,Wanakesha kwenye maombi mpaka sauti zinawakwama lkn ukisikia mambo yao yanatia kichefuchefu mi nawashauri wangefanya mambo yao kwa uhuru tu maana namna hii wanateseka bure eti
 
Back
Top Bottom