Inamaana kweli serikali haina hela ama ni ubinafsi wa viongozi

jiwe angavu

JF-Expert Member
Aug 28, 2015
19,115
35,945
Unakuta mtumishi wa umma anadai madai mengi sana,kama posho za masaa ya kazi,pesa za kujikimu,posho za uhamisho,pesa za likizo,pesa za safari n.k

Ila kila siku ni danadana mara pesa hakuna mara OC imezuiwa,mara mfumo unasumbua,mara uploader hajaapload malipo,mara dokezo halionekani n.k?

Hivi mbona wakuu wa idara/wakurugenzi na viongozi wengine wakipata safari hizo hoja ama changamoto za malipo kwao huwa hazipo maana hela zao hutoka kwa wakati?

Hii inawahusu sana watumishi wa halmashauri hali ni mbaya sana kwa mwendo huu lazima watu wale kwa urefu wa kamba zao,poteleapote.

NB:Kuajiriwa halmashauri ni kukaribisha umasikini maishani mwako.
 
Back
Top Bottom