Hii ina maanisha nini??
Mosi,Wadau wamekuwa wakilalamika sana juu ya TBC kiasi amabacho kumbe content yao hata mkuu wa nchi haifuatilii labda sababu haimvutii mtazamaji ama imekaa kiCCM kiasi analazimika kuangalia vyombo vya habari binafsi ili apate ukweli wa kinachoendelea kwenye jamii. Rejea mtangazaji wa TBC kipind cha kampeni ambaye alithubutu kuruka baadhi ya vichwa vya Magazeti sababu vinamzungumzia Lowassa.
Pili, Naona dalili mbaya ama ishara inatumwa kwa Viongozi wa Media ya Taifa TBC indirectly. Kama viongozi hawa wapo makini inabid wajitathimini kwamba iweje kila siku Raisi apoge simu Clouds tu na sio kwa Chombo cha serikali.
Tatu, Inawezekana kuna Jambo linaendelea ambalo mimi na wewe hatulijui kati ya Raisi(serikali) ndio maana kila mara raisi pamoja na watendaji wengine wa serikali inabid wajlchomoze kupitia clouds aidha kufafanua jambo ama kujibu hoja sinazojitokeza kwa wananchi mbalimbali hata kama wananchi hao wanatokea sehemu ambako clouds TV haipatikani.
Ushauri wangu kwa serikali(Raisi), ianze kupenda vyake kabla ya kuanza kushoboka na vya jirani. Huwezi himiza wananchi wawe wazalendo kwa kupanda pangaboi wakati ww serikali unapanda fastjet.