Inamaana Clouds TV ndo imekua TV ya taifa?

aliyetegwa

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
312
483
Wadau,

Nimepatwa na kigugumizi leo nilipokua nikiangalia kipindi cha 360 baada ya mkuu wa kaya kupiga simu kuwapogeza kwa kipindi kizuri.

Najiuliza watanzania wote tunatakiwa kuamia Clouds ili tuweze kuwa tunapata habari za kitaifa, ama hii inamaanisha nini kwenu wadau maana mimi nimebaki na maswali mengi bila majibu kiukweli.

Naomba tusaidiane kuliweka ili sawa ikiwezekana Clouds media itangazwe kama chombo cha habari cha taifa.
 
Rais amepiga simu leo clouds akiwapongeza kwa ubunifu wao. Maana walikuwa wanarusha kipindi chao pendwa cha clouds 360 live toka white sands hotel.

Kiukweli Clouds Ni Wabunifu ndiyo maana wanamvutia rais.

Tunasubiria Bahasha Corporation (TBC) amkeni, hii ni aibu.
 
Basi leo Mwalimu na timu nzima ya TBC watakesha ofisini tena (Novena); wakitafakari wanakosea wapi maana ni majuzi tu walikesha wakijenga mikakati ili mkuu wa boma akipiga simu basi iwe TBC! Phd sasa itahakikiwa upya maana imepwaya! Mkulu hajawa impressed!
 
Hayo ni mambo binafsi acha ushambenga.. Uraisi kama anaipenda TP Lindanda Pamba FC wana kawekamo basi hiyo timu iwe ni ya Taifa?
 
Kuna kama clouds hapa mjini?
Leo rais kapiga simu tena kuipongeza sasa sijui wale ant-clouds mtajifungia wapi
Hongereni kwa ubunifu wa vipindi wa vipindi
Ndo maana inakubalika kitaifa na kimataifa
Ubunifu wa vipindi sana tu
Hapa bongo kila kona ni clouds
Viva clouds
Nilisema mwaka huu anti-clouds mtaomba poo
 
Ndiyo,Clouds imefuata masharti yote ya kusajiliwa
kama chombo cha habari hapa nchini,
Mimi nampongeza rais,kwa kutuma salaam
kwa vyombo vingine visivyotaka kujiongeza
kwa kisingizio cha kuitwa...ya taifa.

Kwa sasa kila kitu ni ushindani
hata wauza maandazi hili wanalijua
kama hutaki kujiongezaa maandazi yako yatadoda
kila siku.
Nikikuuliza mleta uzi kama
kweli wewe ni msikilizaji wa vyombo vya habari
vya taifa imekuaje leo ukansikia Mh. clouds?
Si ajabu ni watu wachache wanasikiliza vyombo hivyo.
 
Hawana jipya TV yao na Radio yao wameizuia kutoa habari LIVE walikusudia nini? Waliona watakuwa wanawazuia wabunge was upinzani kuonekana na kusikikika.Hawana jipya.
 
Ndiyo,Clouds imefuata masharti yote ya kusajiliwa
kama chombo cha habari hapa nchini,
Mimi nampongeza rais,kwa kutuma salaam
kwa vyombo vingine visivyotaka kujiongeza
kwa kisingizio cha kuitwa...ya taifa.

Kwa sasa kila kitu ni ushindani
hata wauza maandazi hili wanalijua
kama hutaki kujiongezaa maandazi yako yatadoda
kila siku.
Nikikuuliza mleta uzi kama
kweli wewe ni msikilizaji wa vyombo vya habari
vya taifa imekuaje leo ukansikia Mh. clouds?
Si ajabu ni watu wachache wanasikiliza vyombo hivyo.
hata aibu huoni
 
Kuna kama clouds hapa mjini?
Leo rais kapiga simu tena kuipongeza sasa sijui wale ant-clouds mtajifungia wapi
Hongereni kwa ubunifu wa vipindi wa vipindi
Ndo maana inakubalika kitaifa na kimataifa
Ubunifu wa vipindi sana tu
Hapa bongo kila kona ni clouds
Viva clouds
Nilisema mwaka huu anti-clouds mtaomba poo
 
Ukikaa karibu n nyuki utaambulia asalii tamu tammu na hii ndio kinacho fanywa na clouds media. Tusitegemee hata siku moja wakiongelea changamoto zilizopo kwa namna ya kuikosoa serikalii ila wao kwao itakuwa ni NDIO MZEE NDIO NDIO SAHIHI KABISA
 
Back
Top Bottom