Uchaguzi 2020 Inakuwaje viongozi wa dini wanapowasifia watawala wa CCM ionekane sawa, lakini inapotokea wengine wakawasifia Wapinzani wanaonekana wachochezi?

Kila mara tumekuwa tunamsikia Rais wetu akitamka kuwa Maendeleo hayana chama.

Kwa maana nyingine ni kuwa nchi hii ni ya mfumo wa vyama vingi, kwa hiyo mwananchi yeyote anaruhusiwa kuwa mshabiki wa chama chochote anachokitaka.

Lakini tunashuhudia kutokea "double standard" ya kiongozi wa dini anapowasifu waziwazi viongozi walioko madarakani inaonekana sawasawa kabisa, lakini inapotokea kiongozi wa dini kusifia viongozi wa kisiasa wa upinzani, hususani wa CHADEMA, ionekane wachochezi?

Tumeshuhudia mwezi uliopita Nabii Josephat Mwingira, alipotoa clip akionyesha namna alivyofunuliwa unabii wake alioepewa na Mungu wetu kuwa, Tundu Lissu, ni mshindi tayari.

Walijitokeza viongozi kadhaa wa dini, akiwemo Sheikh mkuu wa Dar, Alhad Mussa, wakishutumu vikali clip hiyo na kusema wazi kuwa kiongozi wa dini hawapaswi wahubiri siasa kwa kuwa wanaleta uchochezi na kama wanataka hivyo basi ni vyema wakavua majoho ya kidini na wakajitumbukiza kwenye siasa.

Lakini tumeshuhudia wiki iliyopita tu, wakati Rais Magufuli akifanya kampeni yake Kawe, akijitokeza Sheikh Mkuu wa Dar, Alhad Mussa, akimnadi waziwazi, Rais Magufuli pamoja na wabunge na madiwani wa CCM na kueleza kuwa wapigiwe kura, kwa kuwa wameleta Maendeleo makubwa.

Sijasikia kiongozi yeyote wa dini, aidha wa kiislam au wa kikristo aliyejitokeza hadharani, kukemea mwenendo huo na kumkanya Sheikh Mkuu huyo, Alhad Mussa, kuwa anachanganya dini na siasa, kwa hiyo hapaswi kufanya hivyo.

Tukamsikia Sheikh Ponda, akiibuka katika mkutano wa kampeni wa jijini Dodoma na kuwasihi waislam wa nchi hii kuwa wampigie kura zote, mgombea wa CHADEMA, Tundu Lissu, kwa kuwa yeye ndiye anahubiri sera ya Uhuru, Haki na Maendeleo ya watu, ambayo ndiyo sera bora zaidi.

Wakaibuka masheikh kadhaa na kuongea na vyombo vya habari, akiwemo Sheikh Jongo, wakilaani vikali msimamo huo wa Sheikh Ponda na kuuelezea kuwa unaweza kutuletea machafuko nchini, kwa kuwa viongozi wa dini hawapaswi kujiingiza kwenye siasa!

Ndipo hapo ninapojiuliza, hivi hawa akina Sheikh Jongo, hawakumuona Sheikh mwenzao wa Mkoa wa Dar, akimnadi waziwazi, Rais Magufuli kwenye viwanja vya Tanganyika Packers, je ni kwanini hawakutoa tamko lao hilo?

Ndipo hapo ninapoona kuwa viongozi wa kidini nchini kuwa wana "double standard" wakiona kiongozi mwenzao wa dini anaibuka na kiwasifu watawala wetu wa CCM, wanashikwa na "kigugumizi" na kutokemea, lakini wanapoona viongozi hao wa dini wakiwasifu viongozi wa kisiasa, hususani wa CHADEMA, ndipo hapo wanapomshukia kama mwewe na kumshambulia vikali mno!

Tujikumbushe kidogo kuwa nchi yetu ni ya mfumo wa vyama vingi na tumekuwa tukimsikia Mara kwa Mara Rais wetu Magufuli akisema kuwa Maendeleo hayana chama na kwa maana nyingine ni ruksa mwananchi yeyote kushabikia chama chochote anachoona huyo mwananchi kuwa kinafaa kushabikiwa, kwa kuwa kwa kufanya hivyo atakuwa hajavunja Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977.
Pumbavu huna akili wewe,Mwingira na Ponda wanasemea watanzania kwa mwamvuli wa taasisi gani?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom