Uchaguzi 2020 Inakuwaje viongozi wa dini wanapowasifia watawala wa CCM ionekane sawa, lakini inapotokea wengine wakawasifia Wapinzani wanaonekana wachochezi?

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
14,214
2,000
Kila mara tumekuwa tunamsikia Rais wetu akitamka kuwa Maendeleo hayana chama.

Kwa maana nyingine ni kuwa nchi hii ni ya mfumo wa vyama vingi, kwa hiyo mwananchi yeyote anaruhusiwa kuwa mshabiki wa chama chochote anachokitaka.

Lakini tunashuhudia kutokea "double standard" ya kiongozi wa dini anapowasifu waziwazi viongozi walioko madarakani inaonekana sawasawa kabisa, lakini inapotokea kiongozi wa dini kusifia viongozi wa kisiasa wa upinzani, hususani wa CHADEMA, ionekane wachochezi?

Tumeshuhudia mwezi uliopita Nabii Josephat Mwingira, alipotoa clip akionyesha namna alivyofunuliwa unabii wake alioepewa na Mungu wetu kuwa, Tundu Lissu, ni mshindi tayari.

Walijitokeza viongozi kadhaa wa dini, akiwemo Sheikh mkuu wa Dar, Alhad Mussa, wakishutumu vikali clip hiyo na kusema wazi kuwa kiongozi wa dini hawapaswi wahubiri siasa kwa kuwa wanaleta uchochezi na kama wanataka hivyo basi ni vyema wakavua majoho ya kidini na wakajitumbukiza kwenye siasa.

Lakini tumeshuhudia wiki iliyopita tu, wakati Rais Magufuli akifanya kampeni yake Kawe, akijitokeza Sheikh Mkuu wa Dar, Alhad Mussa, akimnadi waziwazi, Rais Magufuli pamoja na wabunge na madiwani wa CCM na kueleza kuwa wapigiwe kura, kwa kuwa wameleta Maendeleo makubwa.

Sijasikia kiongozi yeyote wa dini, aidha wa kiislam au wa kikristo aliyejitokeza hadharani, kukemea mwenendo huo na kumkanya Sheikh Mkuu huyo, Alhad Mussa, kuwa anachanganya dini na siasa, kwa hiyo hapaswi kufanya hivyo.

Tukamsikia Sheikh Ponda, akiibuka katika mkutano wa kampeni wa jijini Dodoma na kuwasihi waislam wa nchi hii kuwa wampigie kura zote, mgombea wa CHADEMA, Tundu Lissu, kwa kuwa yeye ndiye anahubiri sera ya Uhuru, Haki na Maendeleo ya watu, ambayo ndiyo sera bora zaidi.

Wakaibuka masheikh kadhaa na kuongea na vyombo vya habari, akiwemo Sheikh Jongo, wakilaani vikali msimamo huo wa Sheikh Ponda na kuuelezea kuwa unaweza kutuletea machafuko nchini, kwa kuwa viongozi wa dini hawapaswi kujiingiza kwenye siasa!

Ndipo hapo ninapojiuliza, hivi hawa akina Sheikh Jongo, hawakumuona Sheikh mwenzao wa Mkoa wa Dar, akimnadi waziwazi, Rais Magufuli kwenye viwanja vya Tanganyika Packers, je ni kwanini hawakutoa tamko lao hilo?

Ndipo hapo ninapoona kuwa viongozi wa kidini nchini kuwa wana "double standard" wakiona kiongozi mwenzao wa dini anaibuka na kiwasifu watawala wetu wa CCM, wanashikwa na "kigugumizi" na kutokemea, lakini wanapoona viongozi hao wa dini wakiwasifu viongozi wa kisiasa, hususani wa CHADEMA, ndipo hapo wanapomshukia kama mwewe na kumshambulia vikali mno!

Tujikumbushe kidogo kuwa nchi yetu ni ya mfumo wa vyama vingi na tumekuwa tukimsikia Mara kwa Mara Rais wetu Magufuli akisema kuwa Maendeleo hayana chama na kwa maana nyingine ni ruksa mwananchi yeyote kushabikia chama chochote anachoona huyo mwananchi kuwa kinafaa kushabikiwa, kwa kuwa kwa kufanya hivyo atakuwa hajavunja Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977.
 
Ngongo

JF-Expert Member
Sep 20, 2008
13,960
2,000
Kila mara tumekuwa tunamsikia Rais wetu akitamka kuwa Maendeleo hayana chama.

Kwa maana nyingine ni kuwa nchi hii ni ya mfumo wa vyama vingi, kwa hiyo mwananchi yeyote anaruhusiwa kuwa mshabiki wa chama chochote anachokitaka..

Kuna Sheikh moja alimwomba hadi Yesu na Mtume Mohamad hapakuwa na kelele hata kidogo.

Sheikh Ponda kamnadi Lissu imekuwa taabu kweli kweli.Ukitumia akili kidogo utagundua Viongozi wa dini wengi ni wanafiki sana.

Week mbili zilizopita katika Ibada KKKT usharika wa Kimara Mchg alimpigia debe mgombea ubunge wa Ubungo Kitila Mkumbo na Rais Magufuli katikati ya Ibada hapakuwa na kelele hata kidogo.Nilikuwepo katika ibada hiyo nilikwazika sana,nilitamani kumzaba kelbu Mchg kwa kukiuka taratibu za Ibada.
 
Lombo

JF-Expert Member
Jan 21, 2011
4,209
2,000
Mwaka huu Viongozi wa Dini wamejichanganta kweli.....ndio shida ya unafiki na Uoga....ndio tumedhidi kujifunza maana halisi ya Dini !
 
Ninaweza

JF-Expert Member
Dec 14, 2010
10,542
2,000
Kelele hizo ni wivu wa CCM dhidi ya upinzani, kwani wanaona hata wale walokuwa chini ya imaya yao wanaanza kukata kamba.
 
Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
14,214
2,000
Kuna Sheikh moja alimwomba hadi Yesu na Mtume Mohamad hapakuwa na kelele hata kidogo.

Sheikh Ponda kamnadi Lissu imekuwa taabu kweli kweli.Ukitumia akili kidogo utagundua Viongozi wa dini wengi ni wanafiki sana...
Yaani kwao wao watawala wakisifiwa ni sawa.

Ila wakisifiwa wapinzani, ndiyo inakuja nongwa, hadi kuitwa kuwa ni wasaliti na wachochezi!
 
dolevaby

JF-Expert Member
Aug 25, 2013
11,321
2,000
Kuna Sheikh moja alimwomba hadi Yesu na Mtume Mohamad hapakuwa na kelele hata kidogo.

Sheikh Ponda kamnadi Lissu imekuwa taabu kweli kweli.Ukitumia akili kidogo utagundua Viongozi wa dini wengi ni wanafiki sana.

Week mbili zilizopita katika Ibada KKKT usharika wa Kimara Mchg alimpigia debe mgombea ubunge wa Ubungo Kitila Mkumbo na Rais Magufuli katikati ya Ibada hapakuwa na kelele hata kidogo.Nilikuwepo katika ibada hiyo nilikwazika sana,nilitamani kumzaba kelbu Mchg kwa kukiuka taratibu za Ibada.
Miongoni mwa vitu anazingua Mastai nihiyo kupigia debe jiwe na genge lake matatizo wanayotendewa waumini wake na jiwe kwake sio issue ila tar 28/10 tutaelewana
 
denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
3,058
2,000
Wanatumiwa na CCM 100% wanajidanganya sana kwa kudhani watanzania wa leo ni wale wa mwaka "47

#bampa to bampa
 
Kibe Zamorano

Member
Jan 1, 2017
24
75
Kila mara tumekuwa tunamsikia Rais wetu akitamka kuwa Maendeleo hayana chama.

Kwa maana nyingine ni kuwa nchi hii ni ya mfumo wa vyama vingi, kwa hiyo mwananchi yeyote anaruhusiwa kuwa mshabiki wa chama chochote anachokitaka.

Lakini tunashuhudia kutokea "double standard" ya kiongozi wa dini anapowasifu waziwazi viongozi walioko madarakani inaonekana sawasawa kabisa, lakini inapotokea kiongozi wa dini kusifia viongozi wa kisiasa wa upinzani, hususani wa CHADEMA, ionekane wachochezi?

Tumeshuhudia mwezi uliopita Nabii Josephat Mwingira, alipotoa clip akionyesha namna alivyofunuliwa unabii wake alioepewa na Mungu wetu kuwa, Tundu Lissu, ni mshindi tayari.

Walijitokeza viongozi kadhaa wa dini, akiwemo Sheikh mkuu wa Dar, Alhad Mussa, wakishutumu vikali clip hiyo na kusema wazi kuwa kiongozi wa dini hawapaswi wahubiri siasa kwa kuwa wanaleta uchochezi na kama wanataka hivyo basi ni vyema wakavua majoho ya kidini na wakajitumbukiza kwenye siasa.

Lakini tumeshuhudia wiki iliyopita tu, wakati Rais Magufuli akifanya kampeni yake Kawe, akijitokeza Sheikh Mkuu wa Dar, Alhad Mussa, akimnadi waziwazi, Rais Magufuli pamoja na wabunge na madiwani wa CCM na kueleza kuwa wapigiwe kura, kwa kuwa wameleta Maendeleo makubwa.

Sijasikia kiongozi yeyote wa dini, aidha wa kiislam au wa kikristo aliyejitokeza hadharani, kukemea mwenendo huo na kumkanya Sheikh Mkuu huyo, Alhad Mussa, kuwa anachanganya dini na siasa, kwa hiyo hapaswi kufanya hivyo.

Tukamsikia Sheikh Ponda, akiibuka katika mkutano wa kampeni wa jijini Dodoma na kuwasihi waislam wa nchi hii kuwa wampigie kura zote, mgombea wa CHADEMA, Tundu Lissu, kwa kuwa yeye ndiye anahubiri sera ya Uhuru, Haki na Maendeleo ya watu, ambayo ndiyo sera bora zaidi.

Wakaibuka masheikh kadhaa na kuongea na vyombo vya habari, akiwemo Sheikh Jongo, wakilaani vikali msimamo huo wa Sheikh Ponda na kuuelezea kuwa unaweza kutuletea machafuko nchini, kwa kuwa viongozi wa dini hawapaswi kujiingiza kwenye siasa!

Ndipo hapo ninapojiuliza, hivi hawa akina Sheikh Jongo, hawakumuona Sheikh mwenzao wa Mkoa wa Dar, akimnadi waziwazi, Rais Magufuli kwenye viwanja vya Tanganyika Packers, je ni kwanini hawakutoa tamko lao hilo?

Ndipo hapo ninapoona kuwa viongozi wa kidini nchini kuwa wana "double standard" wakiona kiongozi mwenzao wa dini anaibuka na kiwasifu watawala wetu wa CCM, wanashikwa na "kigugumizi" na kutokemea, lakini wanapoona viongozi hao wa dini wakiwasifu viongozi wa kisiasa, hususani wa CHADEMA, ndipo hapo wanapomshukia kama mwewe na kumshambulia vikali mno!

Tujikumbushe kidogo kuwa nchi yetu ni ya mfumo wa vyama vingi na tumekuwa tukimsikia Mara kwa Mara Rais wetu Magufuli akisema kuwa Maendeleo hayana chama na kwa maana nyingine ni ruksa mwananchi yeyote kushabikia chama chochote anachoona huyo mwananchi kuwa kinafaa kushabikiwa, kwa kuwa kwa kufanya hivyo atakuwa hajavunja Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977.
Inauma sana kaka. Magufuli siyo kiongozi mzuri hata kidogo. Ametugawa sana Watanzania. Magufuli ni mjanja mno: anatumia ile falsafa ya "Divide and Rule".
FB_IMG_1603163131617.jpg
 
nguruka wa kig0ma

JF-Expert Member
Jan 16, 2020
1,303

Miaka ya 60-80,walipokuwe waislam wa bakwata, tuliona ni dini ya mwenyezi mungu, walipoanza kuingia suni tuliwaona ni magaidi.
Sasa tunapata majibu kadiri muda unavyokwenda kuwa suni ndiyo dhehebu la kweli ktk uislam

Bakwata hawamchi Mungu
 
Domhome

JF-Expert Member
Jun 28, 2010
2,739
2,000
Magufuli katuharibia sana hii Nchi yaani ni wa hovyo kabisa tena hafai Msikitini na,hakubaliki Kanisani !
 
T2020cdm

Member
Oct 17, 2020
37
125
Hao viongozi wengine wa Dini wanajua wanachotete huenda wanalipwa kila mwisho wa mwezi na ndiyo maisha yao, tuwaache watoe ujinga wao na sisi tuwasubiri tar 28 tuone watazuia sisi tusipige kura.
 
Babati

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
37,397
2,000
Kuna Sheikh moja alimwomba hadi Yesu na Mtume Mohamad hapakuwa na kelele hata kidogo.

Sheikh Ponda kamnadi Lissu imekuwa taabu kweli kweli.Ukitumia akili kidogo utagundua Viongozi wa dini wengi ni wanafiki sana.

Week mbili zilizopita katika Ibada KKKT usharika wa Kimara Mchg alimpigia debe mgombea ubunge wa Ubungo Kitila Mkumbo na Rais Magufuli katikati ya Ibada hapakuwa na kelele hata kidogo.Nilikuwepo katika ibada hiyo nilikwazika sana,nilitamani kumzaba kelbu Mchg kwa kukiuka taratibu za Ibada.
Wengi ni njaa na kukosa elimu kuna wasumbua hawana lolote siyo hata ni viongozi wa dini ni matapeli ya dini
 
Malcom XX

JF-Expert Member
Sep 12, 2020
432
1,000
Kila mara tumekuwa tunamsikia Rais wetu akitamka kuwa Maendeleo hayana chama.

Kwa maana nyingine ni kuwa nchi hii ni ya mfumo wa vyama vingi, kwa hiyo mwananchi yeyote anaruhusiwa kuwa mshabiki wa chama chochote anachokitaka.

Lakini tunashuhudia kutokea "double standard" ya kiongozi wa dini anapowasifu waziwazi viongozi walioko madarakani inaonekana sawasawa kabisa, lakini inapotokea kiongozi wa dini kusifia viongozi wa kisiasa wa upinzani, hususani wa CHADEMA, ionekane wachochezi?

Tumeshuhudia mwezi uliopita Nabii Josephat Mwingira, alipotoa clip akionyesha namna alivyofunuliwa unabii wake alioepewa na Mungu wetu kuwa, Tundu Lissu, ni mshindi tayari.

Walijitokeza viongozi kadhaa wa dini, akiwemo Sheikh mkuu wa Dar, Alhad Mussa, wakishutumu vikali clip hiyo na kusema wazi kuwa kiongozi wa dini hawapaswi wahubiri siasa kwa kuwa wanaleta uchochezi na kama wanataka hivyo basi ni vyema wakavua majoho ya kidini na wakajitumbukiza kwenye siasa.

Lakini tumeshuhudia wiki iliyopita tu, wakati Rais Magufuli akifanya kampeni yake Kawe, akijitokeza Sheikh Mkuu wa Dar, Alhad Mussa, akimnadi waziwazi, Rais Magufuli pamoja na wabunge na madiwani wa CCM na kueleza kuwa wapigiwe kura, kwa kuwa wameleta Maendeleo makubwa.

Sijasikia kiongozi yeyote wa dini, aidha wa kiislam au wa kikristo aliyejitokeza hadharani, kukemea mwenendo huo na kumkanya Sheikh Mkuu huyo, Alhad Mussa, kuwa anachanganya dini na siasa, kwa hiyo hapaswi kufanya hivyo.

Tukamsikia Sheikh Ponda, akiibuka katika mkutano wa kampeni wa jijini Dodoma na kuwasihi waislam wa nchi hii kuwa wampigie kura zote, mgombea wa CHADEMA, Tundu Lissu, kwa kuwa yeye ndiye anahubiri sera ya Uhuru, Haki na Maendeleo ya watu, ambayo ndiyo sera bora zaidi.

Wakaibuka masheikh kadhaa na kuongea na vyombo vya habari, akiwemo Sheikh Jongo, wakilaani vikali msimamo huo wa Sheikh Ponda na kuuelezea kuwa unaweza kutuletea machafuko nchini, kwa kuwa viongozi wa dini hawapaswi kujiingiza kwenye siasa!

Ndipo hapo ninapojiuliza, hivi hawa akina Sheikh Jongo, hawakumuona Sheikh mwenzao wa Mkoa wa Dar, akimnadi waziwazi, Rais Magufuli kwenye viwanja vya Tanganyika Packers, je ni kwanini hawakutoa tamko lao hilo?

Ndipo hapo ninapoona kuwa viongozi wa kidini nchini kuwa wana "double standard" wakiona kiongozi mwenzao wa dini anaibuka na kiwasifu watawala wetu wa CCM, wanashikwa na "kigugumizi" na kutokemea, lakini wanapoona viongozi hao wa dini wakiwasifu viongozi wa kisiasa, hususani wa CHADEMA, ndipo hapo wanapomshukia kama mwewe na kumshambulia vikali mno!

Tujikumbushe kidogo kuwa nchi yetu ni ya mfumo wa vyama vingi na tumekuwa tukimsikia Mara kwa Mara Rais wetu Magufuli akisema kuwa Maendeleo hayana chama na kwa maana nyingine ni ruksa mwananchi yeyote kushabikia chama chochote anachoona huyo mwananchi kuwa kinafaa kushabikiwa, kwa kuwa kwa kufanya hivyo atakuwa hajavunja Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977.
Mashekh njaa
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom