Inakuwaje tabia hizi kwenye lift ya gari?

Inakuwaje tabia hizi kwenye lift ya gari?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
63,613
Reaction score
127,994
Ukipewa lifti ya gari ukiwa ndani lazima utaonyesha moja ya tabia hizi kubwa mbili.

1. Unakuwa unazungumza sana njia nzima.
2. Unakuwa hujiamini na unajistukia muda wote.

Kisaikolijia hizi hali mbili zinatokana na nini?

Karibuni tupeane uzoefu wa kudoea lifti kwa magari ya watu.
 
Utakuwa umetumia uzoefu wako tuu, mbona mimi sipo hivyo.
 
Ni kwa kuwa mtu unakuwa huyajui mawazo anayokuwazia huyo aliyekupa lift.

1. Kama ni mwanaume amekupa lift mwanaume mwenzio unakuwa hujui anakufikiriaje kwa wewe kutokuwa na gari ama dume zima kupewa lift na dume mwenzio. Unakuwa hujiamini maana unajiona kama mzembe yeye kapataje gari na wewe umeshindwa kupata?

2. Na kama mwanamke amepewa lift na mwanaume anakuwa hajui lengo la mtoa lift. Je anataka kunitongoza? Au naonekana mshamba mbele yake?

3. Na kama mwanamke amempa lift mwanaume kujishitukia kwake ni kama namba 1 hapo juu ila unajumlisha na mfumo dume.
 
Because unakubali na kukubali aliyekupa lifti ana uwezo zaidi yako, incase na wewe humiliki usafiri wa aina hiyo especially gari
 
Mimi nipo tofauti halafu sipendi kuonekana nina shobo shobo hivi.. ..
 
Wanaopewa lift wana maudhi sana.Nilimpa lift jamaa mmoja anayenifahamu. Njia yote alikuwa anasifia uzuri wa mabinti zangu! Nyongo zilinipanda ikabidi nikatishe safari kinamna!
 
Wanaopewa lift wana maudhi sana.Nilimpa lift jamaa mmoja anayenifahamu. Njia yote alikuwa anasifia uzuri wa mabinti zangu! Nyongo zilinipanda ikabidi nikatishe safari kinamna!

Hahahaha ana lake jambo
Ningemshusha na mwisho wa lift ni siku hiyohiyo
 
Siyo wote,mbona tupo tunaojiamini na tukiamua kugonga story,tunagonga;na tukiamau ku-cool,tuna-cool.yaani fool kujiamini hatakm ni gari la lifti.
 
Ukikuta aliyekupa lift haongei, mara nyingi inayokeaga hata uliyepata lift pia upoteze makofidensi, but kuna mtu kukupa lift lakin akawa very chaming, mkuu hapo utaongea mpaka bas na utajiamin as kwamba ni dereva wako tu ama umemkodi.
 
Napenda kuwapa lift hasa co-workers ili nipate kampani na story kwenye foleni, lol. Kukaa kimya kwenye foleni peke yako inakera. Nitakayempa lift aje na story pia.
 
Mimi ukinipa lift, naweka kishoka na ukizubaa napiga hadi honi! Kila ninaemjua lazima nihakikishe kaniona! Na mwisho wa siku wewe ulietoa lift unaonekana dereva wangu!
 
Hahahaha ana lake jambo
Ningemshusha na mwisho wa lift ni siku hiyohiyo

Hata mimi nilijisemea hivyo kimoyomoyo, lakini baada ya muda namwona jamaa anaendesha kamkweche fulani hivi. Sidhani kama atakuwa kwenye kundi la waomba lift tena!
 
Huku mitaa yetu lifti adimu labda za baiskeli wakati wakwenda shambani
 
Back
Top Bottom