tatizo ama swali langu, kwanini wakioana hawadumu? while ktk urafk wa gf na bf walidumu let say mwaka au zaidi ya mwaka?
Charminggirl, huu uzi ni mzuri. Ingawa sijashuhudia ndoa za muda mfupi ila naweza sema kitu hapa.
Mapenzi ya bf+gf ( urafiki wa kimapenzi/ngono) mara nyingi haujumuishi watu kuishi pamoja, na kutokana na hilo madhaifu mengi huwa yamejifisha, as mnakutana kwa muda mfupi tuu, then kila mtu anaishia kivyake. Hivyo ule muda mfupi wawili hao hujitahidi uwe ni wa furaha na kufarijiana, na ndio maana wote huenjoy.
Sasa tuje kwa wenyendoa, ambao kwa namna moja hulazimika kuishi "under the same roof, same room, same bed" lol. Hapo ndo kivumbi huanza. Kama ni uchafu utaanza kuonekana hapo, kama ni ulevi ndo utauconsider kwa uzito wake, kama ni ulafi nao utauona kwa mapana yake, nao ubahili utaujua. Hatimaye unagundua Aaaah! kumbe huyu mwenzangu yuko hivi? Sasa maisha ya ndoa na kuishi umoja katika wawili, yahitaji uvumilivu na kujitolea, wawili hao wanaposhindwa sasa kuyaishi mapungufu ya "one another" ndo hapo utasikia ooh! mwanamke mwenyewe hata sikumpenda, au mwanaume mwenyewe mlevi?
Hivyo mapenzi ya gf+bf, kwa mtazamo wangu hutawaliwa zaid na LUST na starehe zingine, ndo maana yananoga. Ukiingia kwenye majukumu ya kutoa hela ya mboga daily au kufua nguo za hubby na kumpikia, ndo hapoo sasa!