Inakuwaje Makonda anaongea kisomi kuliko "daktari" Mwigulu

Keynez

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2007
Posts
3,620
Reaction score
6,510
Moja ya alama ya mtu yoyote aliyesoma na kuelimika ni uongeaji wake. Hata mtu ambaye hajasoma shule sana ila ni msomaji wa vitabu, ni rahisi kumtambua. Kuanzia upangaji wake wa maneno, akiwa anatoa mawazo yake, nk.

Mwigulu sijawahi kumkubali kwa sababu toka nimeanza kumsikiliza day 1, naona ni mtu anayejaribu kuficha madhaifu yake ya kifikra kwa kuweka sura ya kujiamini na kuchekacheka ila ukimsikiliza vizuri utagundua kabisa si mtu aliyeelimika wala kuwa na ufahamu wa mambo anayopewa majukumu ya kuyasimamia. Ni wale watu wajanja wajanja tu.

Makonda amesemwa kwa mengi. Kuanzia kumkwida Warioba kipindi kile kwenye Bunge la Katiba kama sikosei, utajiri wa ghafla kipindi akiwa Mkuu wa Mkoa, kuhusishwa na tukio la Lissu na mengine ya utekaji kipindi cha Magu, nk. ila jamaa ana kitu mabeberu wanaita yuko "articulate". Yaani anaongea kwa ufasaha. Sijajua ni kipaji au ni mtu ambaye anapenda kujisomea maana wote tunajua hana elimu kuuubwa.

Ukiwasikiliza wote wawili, ungeweza kudhani Makonda ndiyo ana PhD halafu Mwigulu ndiye "Bashite".

Hapa simaanishi Makonda ni mtu msafi, muadilifu au mawazo yake yote ni mazuri au ya kisomi (mfano wazo la juzi kuwanunulia vifaa waandishi binafsi ni wazo la hovyo sana ingawa tunajua nia ni nini) ila ninachotaka kusema hata akiwa anatoa mawazo mabaya bado ana uwezo wa kujielezea kwa ufasaha hata ukajua msingi wa hayo mawazo yake.

Mwigulu anajiumauma tu akidhani tai ya bendera itambeba.
 
Kwa hiyo awe NWM? Halafu Baada ya mda amtoe kabisa?
Ila ni sawa tu hata akituongoza
 
Moja ya alama ya mtu yoyote aliyesoma na kuelimika ni uongeaji wake. Hata mtu ambaye hajasoma shule sana ila ni msomaji wa vitabu, ni rahisi kumtambua. Kuanzia upangaji wake wa maneno, akiwa anatoa mawazo yake, nk.

Mwigulu sijawahi kumkubali kwa sababu toka nimeanza kumsikiliza day 1, naona ni mtu anayejaribu kuficha madhaifu yake ya kifikra kwa kuweka sura ya kujiamini na kuchekacheka ila ukimsikiliza vizuri utagundua kabisa si mtu aliyeelimika wala kuwa na ufahamu wa mambo anayopewa majukumu ya kuyasimamia. Ni wale watu wajanja wajanja tu.

Makonda amesemwa kwa mengi. Kuanzia kumkwida Warioba kipindi kile kwenye Bunge la Katiba kama sikosei, utajiri wa ghafla kipindi akiwa Mkuu wa Mkoa, kuhusishwa na tukio la Lissu na mengine ya utekaji kipindi cha Magu, nk. ila jamaa ana kitu mabeberu wanaita yuko "articulate". Yaani anaongea kwa ufasaha. Sijajua ni kipaji au ni mtu ambaye anapenda kujisomea maana wote tunajua hana elimu kuuubwa.

Ukiwasikiliza wote wawili, ungeweza kudhani Makonda ndiyo ana PhD halafu Mwigulu ndiye "Bashite".

Hapa simaanishi Makonda ni mtu msafi, muadilifu au mawazo yake yote ni mazuri au ya kisomi (mfano wazo la juzi kuwanunulia vifaa waandishi binafsi ni wazo la hovyo sana ingawa tunajua nia ni nini) ila ninachotaka kusema hata akiwa anatoa mawazo mabaya bado ana uwezo wa kujielezea kwa ufasaha hata ukajua msingi wa hayo mawazo yake.

Mwigulu anajiumauma tu akijua tai ya bendera itambeba.
Hata kwenye darasa la vilaza watupu, hakosekani best student!
 
Hakuna cha kuongea kisomi sema umetumwa au unajikomba kwako ili akukumbuke kwenye utawala wa mtu wake spesho. Bashiti na Mkumbo Madelu wote ni mafaaala na machaawa. Ni wasomi kwa wasiojua maana ya usomi.
 
Daaah niko mbali kabisa na mfumo. Sijui ataanzaje kunikumbuka
 
Una hoja, usikilizwe ila kuna wengine nadhani nature yao tu ni kwamba hawana akili.
Ukishakuwa kwenye huu mfumo huu UKITUMIA TU AKILI inakuwa ni offence kwa mamlaka,labda ukae kimya ..angalia warioba anayopitia kuwa na akili timamu na ukazitumia ni unageuka adui ?

ndio maana wanazifungia akili zao kabatini hata maprofesa wa majalalani ...wote wanakuwa mabashite..ili mradi mkono uende kinywani.
 
Uchawa hauna ukaribu au umbali na mfumo bali uzwazwa na uvivu wa kufikiri na kufikiri kuwa akitetea majambazi yatamkumbuka kwenye wizi wao
Daah umenisoma vibaya. Sipo huko kabisa ila haiondoi ukweli kuwa ni muhimu kwa kiongozi kuwa na uwezo wa kujielezea kwa ufasaha.
 
Ukishakuwa kwenye huu mfumo huu UKITUMIA TU AKILI inakuwa ni offence kwa mamlaka,labda ukae kimya ..angalia warioba anayopitia kuwa na akili timamu na ukazitumia ni unageuka adui ?

ndio maana wanazifungia akili zao kabatini hata maprofesa wa majalalani ...wote wanakuwa mabashite..ili mradi mkono uende kinywani.
Sasa inakuwaje ndani ya mfumo huo huo wa hovyo, Makonda anakuwa tofauti na wenzake?

I hope sitaonekana kama nampigia chapuo Makonda maana siyo nia yangu hiyo. Siongelei utendaji wala uadilifu wake, nazungumzia uwezo wake wa kujieleza.
 
wale walio ongea speech zilizonyooka za kujenga na kuponya wanatumbuliwa..(chawene)

.mfumo unataka huo ubashite ndio mana watu wanajitoa ufahamu...sio kwamba eti hawana akili.
Juzi hapa Mwigulu anasema hajaja ili apendwe. Yaani anaiga kauli ya Magufuli bila kutambua muktadha wa kauli ya Magufuli ulikuwa tofauti na wa kwake. Utasema kuna msomi hapo?

Mwigulu kama WF ndiye aliyemshauri Samia kusema deni linaonekana kubwa kwa sababu limetajwa katika shilingi.
 
Back
Top Bottom