Inakuwaje bei ya mafuta Tanzania inakuwa ghali kuliko nchi ambazo zinapitisha bidhaa hiyo bandari ya Tanzania?

Tatizo kubwa ni kuwaacha wafanyabiashara wakubwa kuwa wanasiasa hivyo kusimamia maslahi yao kwanza badala ya wananchi..
 
Wanaupiga mwingi kwenye kodi za mafuta, ndo maana mapiga dili yanapiga vita uwekezaji kwenye vituo vya kujaza gesi kwenye magari, hovyo kabisa.
 
Wakat Mwigulu anasema watu walikuwa bize na petition ya kumdisqualify mondi leo kelele zishaanza
 
Mkuu juzi nilikua Burundi lita1700
Vipi mkuu huko kuna road toll?

Hii bei yetu imebeba mambo mengi sana ambayo yalikuwa kero mno barabarani...trafiki.
-Road license
-Road toll
-nk

Kwangu mimi naona bora hii bei kuliko kupambana na magwanda meupe huko barabarani.
 
Wazanzibari na watu wa pwani ni rojorojo sana.

Sasa magenge ya wauza mafuta wameshakamata nchi wanajiamilia wanavyotaka.

Usikae ukategemea bei ya mafuta itakuja kushuka hii nchi tena.

Leo watu kama Manji wanazurula uraiani huku ana kesi lukuki za kukwepa kodi, kuzurumu taasisi za umma zilizompa pesa azipatie huduma akatokomea na pesa na ushahidi upo lakini anadunda mtaani. TRA kila siku anawawekea court injunction kwa kodi wanazomdai halipi. Halafu anaitwa muwekezaji.
Tumeingia chaka Kwa huyu mama yetu
 
Mwendazake kaenda wewe pambana na hali yako hakuna wa kukusikiliza.
Mafuta yenyewe unakuta yanaingia kwa maghumashi hayapiti kwenye machine utasikia machine imeharibiki wabongo wameichezea.
 
Mwendazake kaenda wewe pambana na hali yako hakuna wa kukusikiliza.
Mafuta yenyewe unakuta yanaingia kwa maghumashi hayapiti kwenye machine utasikia machine imeharibiki wabongo wameichezea.
bahati nzuri hao wanaotobia hayo mabomba asilimia 60% waliwekea na mwendazake. Alipigwa akiwa hai sijui sasa itakuwaje
 
Mafuta mapaka yanafika bandarini Tanzania bei na wastani wa TZS 1,162.00 Kodi inachukua sehemu kubwa mapaka kuyafikisha shs.2,275.00 baada ya hapo ni usafirishaji na faida za wauzaji. So tatizo ni serekali yetu haiwezekani kodi na tozo ziwe karibu 100% ya bei ya CIF.
View attachment 1837383
View attachment 1837382
Kuna shida katika itaratibu wa kutafuta vyanzo vya mapato na ukokotoaji.
Hata uagizaji Gari ni hivyo hivyo bei ya kununulia inalingana na tozo na kodi zinazotozwa na Serikali ya Tanzania.
HII KASORO INAHITAJI MJADALA WA KITAIFA.
Angalia mfano huu:
1.Serikali inataka kodi kwenye bia,Lakini Serikali hiyo hiyo inaziia watu kunywa bia eti mwisho saa 6 usiku!??
2.Serikali inataka kodi kwenye mafuta,lakini Serikali hiyo inaweka kodi na tozo nyingi na kufanya wananchi wengi wasiagize magari.Kumbe tungepunguza kodi na tozo, wengi watumie magari na kodi ipatikane kwenye mafuta.
3.Mkulima analima mazao kwa nguvu zake, lakini wakati wa kuuza Serikali inakataza kuuza mazao nje ya nchi(eti mwananchi atapata njaa,utafikiri Serikali ndio inayomlisha mwananchi).
Ushauri:
Wenye maamuzi katika Serikali wafikirie namna ya kufanya uchumi na fedha iwe na mzunguko endelevu.
 
Ni aibu kama nchi!

Wilayani Ngara mkoa wa Kagera lita ya petroli inauzwa Tsh. 2630 wakati huo huo upande wa Rwanda Wilaya ya Kirehe ambapo hazizidi kilomita 40 ufike petroli lita ni Tsh. 2000.

Kazi kwenu wadau na tumpongeze mama kwa kuupiga
H
Ni aibu kama nchi!

Wilayani Ngara mkoa wa Kagera lita ya petroli inauzwa Tsh. 2630 wakati huo huo upande wa Rwanda Wilaya ya Kirehe ambapo hazizidi kilomita 40 ufike petroli lita ni Tsh. 2000.

Kazi kwenu wadau na tumpongeze mama kwa kuupiga mwingi.
-
Huko pia kwani wanaongozwa na CCM?
 
Back
Top Bottom