Inahitaji ujasiri kumiliki PASSO

Unajua kazi ya thermostat? Endeleeni kusikiliza mafundi wenu wa chini ya miembe.
Kweli mkuu, mafundi wa chini ya mwembe wanapotosha sana. Mimi nilitoa thermostat kweli mlori wangu Hilux DC 2.8 ya 2001. Siku nilipoamua kwenda nayo kwetu nyanda za juu kusini, hata Morogoro sikufika, ikachemsha. Bahati nzuri ile thermostat niliitunza. Baada ya kirudishia sija-experience kuchemsha tena.

Ushauri wa Bure: USITHUBUTU KUTOA THERMOSTAT!
 
Mpaka kufikia hatua ya kumiliki gari aina ya PASSO inapaswa ujitoe ufahamu mbele ya kadamnasi. Gari gani isiyoweza kutembea 200 kms bila kuchemsha?

Nasubiria tamko/katazo la hizi gari toka ngazi za juu.
Hiyo ni passo yako tu, pole me nina passo tangu 2014 mpaka leo na napiga root ndefu zote Tanzania bara. Hakuna cha kutoa thermostat wala nn na hii yangu ni 4p
 
Mpaka kufikia hatua ya kumiliki gari aina ya PASSO inapaswa ujitoe ufahamu mbele ya kadamnasi. Gari gani isiyoweza kutembea 200 kms bila kuchemsha?

Nasubiria tamko/katazo la hizi gari toka ngazi za juu.
Hahahahahaaaa ... mi napita tu!!
 
Wewe umenunua Passo kuu kuu unakuja kulia lia huku... Tangu lini gari imetembea kilometer kama laki mbili ivi ikawa nzima. Nunua angalau ka Passo kametembea KM elfu sabini angalau na wewe uongeze nyingine hamsini hapo kabla hakajaenda kaburini kuchinjwa skreppa...
natumia CORONA ya mwaka 2000, CC 1790 sasa ina KM 248000 kila weekend na tembea zaidi ya KM 500 (Mbeya_Njombe) haijawahi kuchemka! "WATCH IT"
 
Acha uwongo hiyo passo yako itakuwa baiskeli ,pikpiki yenyewe inatembea 250 km bila kuchemka na aina rejeta.
Yaan huyo Jamaa muongo Hatari..
Me naenda Dar- Dodoma 450km na Dar- Tanga 350km na Chombo hakichemshi...
Tena Non Stop na Jiko halizimwi....
kwa uzoefu wangu PASSO ni nzito kwenye Kuchanganya na hii inachangiwa na udogo wa injini yake.
kikubwa ni kuzingatia Service tu...
 
PASSO imekaa kama vile inataka kuchutama bora hata VX (mgongo wa chura) za zamani.
 
Thermostat kazi yake ni kuregulate temperature. Gari ikipata moto sana....inaruhusu coolant ya kutosha iweze kuflow.

Kama vile pasi inavyo fanya kazi... Joto likiongezeka inakatamoto automatic.

Ukitoa thermostat...maana yake Gari hali sensi tena kama joto limeongezeka kwa hiyo haliwezi kucontrol vizuri temperature.

Mwisho wa siku performance inashuka. Passo inahitaji Coolant original., oil nzuri, na service nzuri bila kupitisha muda.

Narudia atakaye kwambia toa thermostat mchape kofi.
 
Ingekuwa amri yangu ningepiga ban gari za kipuuzi zisitumike maeneo ya mjini kabisa labda mikoani huko.Exception ni kama zikiwa kwenye kampuni ya taxi na zisizidi miaka mitatu from manufactured date.

Kwa wote wenye plates za njano nahitaji kuona SUV za maana tu jijini Dar, na executive sedans, series 7 bmw, s class, royal crown, jaguar xf, ls 500 and the like! Zote zitembeazo zisizidi 5 years from manufactured date.

Sio kujaza barabara na mataka taka foleni tu za kijinga. Wasioweza wapande mwendokasi ziwekwe kila route,treni ama wanunue pikipiki!
 
Wewe una gari gani? Usikute hata guta huna
 
Kati ya Suzuki Swift, Toyota Passo, Toyota Vitz/Yaris, Honda Fit na Toyota Starlet. Ni baby walker gani ipo imara zaidi, inaweza kwenda masafa zaidi (considering kuwa hizi zote ni town cars). Sijaweka Toyota IST coz nahisi ipo juu ya hizi zote.
Yaris
 
Back
Top Bottom