SECRET AGENT
JF-Expert Member
- Jan 4, 2019
- 254
- 499
Nimeajiriwa katika kampuni (private sector), Nafanya kazi kwa bidii sana mpaka boss mwenyewe anaona kwamba kweli napiga kazi na kazi nazofanya zinaingiza pesa na kusifiwa na wateja pia lakini tangu niajiriwe mshahara haupandi na naona ni mdogo sana ukilinganisha na kipato kinachoingia kupitia bidii zangu, muda mwingine natoka kazini usiku nikimalizia kazi za wateja, lakini Bado boss hagusii kabisa suala la kuongeza mshahara. Mbali na hapo elimu yangu ni level ya shahada, ingekua nina elimu ndogo labda ningesema kwa sababu ya kiwango changu cha elimu ndiyo sababu.
Nimekuwa na mawazo ya kujibana nifungue business yangu kwani Nafanya kazi nikiwa na hasira moyoni mwangu. Hasira hiyo inakuja pale ambapo waajiriwa wengine ambao nawazidi mbali kiujuzi na kitaaluma tupo level moja ya mshahara na wengine wamenizidi. Nina bidii na heshima sijawahi kukwazana na boss.
Je ni busara kuomba kuongezewa mshahara au laa naomba ushauri wenu