Inadaiwa CCM wamekataa kumdhamini Jecha Salim Jecha

dubu

JF-Expert Member
Oct 18, 2011
3,496
3,461
Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

Mwenyekiti wa zamani wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar, Jecha Salim Jecha ameshindwa kupata wadhamini 250 kila Mkoa katika Mikoa mitatu ya Zanzibar baada ya Wanachama wa Chama cha Mapinduzi kukataa kumdhamini.

Jecha alichukua fomu ya kuomba ridhaa ya kuwania Urais wa Zanzibar kupitia CCM, uamuzi ambao ulizusha mjadala mkubwa huku wanasiasa na hata wanaharakati walikosoa vikali kitendo hicho.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, Wenyeviti wa CCM wa Mikoa ya Zanzibar wamesema kuwa walipokea maombi ya Jecha apatiwe wadhamini 250, lakini hakuna Mwanachama wa CCM aliyejitokeza kumdhamini.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kaskazini Pemba, Hamad Mbelwa, ameserma kwamba wengi wa wananchama wa CCM hawakuwa tayari kumdhamini Jecha kwas kuwa hawafahamu ni loini alijiunga na CCM.

“Huyu bwana alitoa taarifa ya kuomba wanachama wamdhamini, kama kawaida nasi tukawajulisha wanachama… kwa bahati mbaya hakujitokeza mtu” Alisema Mbelwa.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja, Idd Ali Ame alisema kuwa hadi saa nane mchana ya jana, Jescha Salim hakuweza kupata wanachama wa kumdhamini katika Mkoa wa Kaskazini licha ya tarifa kutolewa na kuwafikia wanachama katika matawi yao.

Katika Mkoa wa Mjini, Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa huo Talib Ali Talib, alisema kuwa udhamini wa Jecha umekuwa mtihani mkubwa kwao kwani wanachama wengi walishughulika na udhamini wa wagombea wengine huku wakimuacha Jecha na fomu zake.

Aidha, hali kama hiyo imejitokeza katika Mikoa karibu yote ya Kichama alipokwenda kuomba wadhamini ambapo baadhi yao walihoji uanachama wake ndani ya CCM.

Katika Tawi la CCM chumbuni inakoaminika kuwa Jecha ni mwanachama katika Tawi hilo, wana CCM walihoji uhalali wa uanachama wake na kutoa maoni tofauti huku wengi wakisema hana sifa za kuwania uongozi ndani ya CCM kwa kuwa hajatimiza vigezo vya kikatiba.

“Katiba yetu iko wazi, inasema ili mwanachama mpya ambaye hakufikisha miaka mitano tangu kuingia CCM, hatoweza kugombea nafasi yoyote ya uongozi… sasa tunamshangaa Jecha kuomba ridhaa ya kuwa mgombea wakati uanachama wake ni wa mashaka” Alisema Masoud Machano kutoka Masumbani Jimbo la Chumbuni.

Habari kutoka Dunga Mkoa wa Kusini Unguja zinasema kuwa licha ya Jecha kukaa kwa muda mrefu Makao Makuu ya CCM Mkoa akisubiri wanachama kumdhamini, hadi jua linatua hakuweza kupata hata mwanachama mmoja.

Kwa mujibu wa utaratibu wa CCM kila mwanachama aliyechukua fomu ya kuomba ridhaa ya kuwa mgombea wa Urais wa Zanzibar kupitia Chama hicho, analazimika kupata wadhamini 250 katika Mikoa mitatu ya Zanzibar.

Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Zanzibar, Idara ya Oganaizesheni, Galos Nyimbo alisema hajapokea taarifa ya Jecha Salim Jecha ya kurejecha fomu.

Mwisho wa kutoa na kupokea fomu kwa wanaotaka ridhaa ya CCM kwa kugombea Urais wa Zanzibar ni Juni 30 mwaka huu.
 
inanipa funzo kuwa wanaccm wa zanzibar wanamkubali maalim seif!pia Jecha alipewa zawadi ya uraisi kama atafuta uchaguzi!nadhani mkapa alimdanganya jecha!!!Pia wana ccm zanzibar wameshtukia mtego wa jecha kuchukua fomu ya uraisi!huwenda ndio takwa la vigogo wa ccm!!!ngoja nione sarakasi hizi!!!
 
Mi-CCM kwa unafiki Shetani kawatuniku wallah!

Yaani ndo kwamba wanataka kuwadanganya misukule yao kwamba hawakufurahishwa na uhuni wa Jecha, au hawakumdhamini kwa sababu zipi hasa!

Walijiuliza Marehemu Jaji Ramadhani alijiunga lini na CCM?

Walijiuliza yule RPC wa Arusha alijiunga lini CCM?
 
... Jecha kwenda kuchukua fomu sio kwa bahati mbaya bali ni mkakati uliosukwa; ni picha linatengenezwa maabara. Ukisoma hoja zinazotolewa na viongozi wa CCM kukataa kumdhamini ya msingi zaidi ni "uanachama wake una mashaka" au "hawautambui uanachama wake".

Tafsiri yake ni kwamba wanataka kuaminisha umma kwamba hana uanachama wa chama hicho na kama anao ni wa hivi karibu sana sio enzi akiwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar back in 2015! Inataka kujengwa hoja kwamba wajumbe wa NEC-Zanzibar hususan Mwenyekiti ambaye alifanya maamuzi "mazito" 2015 hafungamani na CCM hivyo maamuzi yale yalikuwa free from influence ya chama/CCM.

Narudia tena, Jecha hajachukua fomu kwa bahati mbaya au hakwenda yeye mwenyewe bali ametumwa kuchukua fomu kimkakati kwa ajili ya propaganda!
 
Shukrani ya Punda ni Mateke. Pole sana Mheshimiwa Jecha. Kwisha habari yako. Ni wakati sasa wa kula mafao yako. Ccm ina wenyewe, na kwa bahati mbaya wewe si mmoja wao.
 
Shukrani ya Punda ni Mateke. Pole sana Mheshimiwa Jecha. Kwisha habari yako. Ni wakati sasa wa kula mafao yako. Ccm ina wenyewe, na kwa bahati mbaya wewe si mmoja wao.
... wala usimpe pole; Jecha na waliomtuma wanajua wanachokifanya hahitaji pole maana lao moja. Kuna "filamu" inaandaliwa kufanikisha propaganda.
 
Back
Top Bottom