Inadaiwa CCM wamekataa kumdhamini Jecha Salim Jecha

Jecha wanamuonea tu nawasihi Wazenj wamdhamini manake millioni moja kuitupa usawa huu ni mbaya sana angekula nayo mapembe miezi mitatu!

Nani alimshauri kuchukua form hali akijua kupata wadhamini ni shida? Wazenj acheni hizo mjazieni form zake; Jecha aliwapeni Rais bora mtulivu na mwenye busara!
 
VIGEZO JE?

Sina uhakika kama Mh. Jecha anatimiza kigezo cha kuwa mwanachama kwa kipindi cha miaka mitano.
 
Sidhani kama huu ni uamuzi wa wanachama wenyewe tu bila maelekezo kutoka juu.
 
Mwenyekiti wa zamani wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar, Jecha Salim Jecha ameshindwa kupata wadhamini 250 kila Mkoa katika Mikoa mitatu ya Zanzibar baada ya Wanachama wa Chama cha Mapinduzi kukataa kumdhamini.

Jecha alichukua fomu ya kuomba ridhaa ya kuwania Urais wa Zanzibar kupitia CCM, uamuzi ambao ulizusha mjadala mkubwa huku wanasiasa na hata wanaharakati walikosoa vikali kitendo hicho.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, Wenyeviti wa CCM wa Mikoa ya Zanzibar wamesema kuwa walipokea maombi ya Jecha apatiwe wadhamini 250, lakini hakuna Mwanachama wa CCM aliyejitokeza kumdhamini.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kaskazini Pemba, Hamad Mbelwa, ameserma kwamba wengi wa wananchama wa CCM hawakuwa tayari kumdhamini Jecha kwas kuwa hawafahamu ni loini alijiunga na CCM.

“Huyu bwana alitoa taarifa ya kuomba wanachama wamdhamini, kama kawaida nasi tukawajulisha wanachama… kwa bahati mbaya hakujitokeza mtu” Alisema Mbelwa.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja, Idd Ali Ame alisema kuwa hadi saa nane mchana ya jana, Jescha Salim hakuweza kupata wanachama wa kumdhamini katika Mkoa wa Kaskazini licha ya tarifa kutolewa na kuwafikia wanachama katika matawi yao.

Katika Mkoa wa Mjini, Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa huo Talib Ali Talib, alisema kuwa udhamini wa Jecha umekuwa mtihani mkubwa kwao kwani wanachama wengi walishughulika na udhamini wa wagombea wengine huku wakimuacha Jecha na fomu zake.

Aidha, hali kama hiyo imejitokeza katika Mikoa karibu yote ya Kichama alipokwenda kuomba wadhamini ambapo baadhi yao walihoji uanachama wake ndani ya CCM.

Katika Tawi la CCM chumbuni inakoaminika kuwa Jecha ni mwanachama katika Tawi hilo, wana CCM walihoji uhalali wa uanachama wake na kutoa maoni tofauti huku wengi wakisema hana sifa za kuwania uongozi ndani ya CCM kwa kuwa hajatimiza vigezo vya kikatiba.

“Katiba yetu iko wazi, inasema ili mwanachama mpya ambaye hakufikisha miaka mitano tangu kuingia CCM, hatoweza kugombea nafasi yoyote ya uongozi… sasa tunamshangaa Jecha kuomba ridhaa ya kuwa mgombea wakati uanachama wake ni wa mashaka” Alisema Masoud Machano kutoka Masumbani Jimbo la Chumbuni.

Habari kutoka Dunga Mkoa wa Kusini Unguja zinasema kuwa licha ya Jecha kukaa kwa muda mrefu Makao Makuu ya CCM Mkoa akisubiri wanachama kumdhamini, hadi jua linatua hakuweza kupata hata mwanachama mmoja.

Kwa mujibu wa utaratibu wa CCM kila mwanachama aliyechukua fomu ya kuomba ridhaa ya kuwa mgombea wa Urais wa Zanzibar kupitia Chama hicho, analazimika kupata wadhamini 250 katika Mikoa mitatu ya Zanzibar.

Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Zanzibar, Idara ya Oganaizesheni, Galos Nyimbo alisema hajapokea taarifa ya Jecha Salim Jecha ya kurejecha fomu.

Mwisho wa kutoa na kupokea fomu kwa wanaotaka ridhaa ya CCM kwa kugombea Urais wa Zanzibar ni Juni 30 mwaka huu.
 
.
1591177430218.jpg
 
Atakuwa raia tu kama sisi haina shida mbona sisi tupo tunadunda.
 
Wanaona aibu wenyewe kuhusu yaliyotokea 2015 huko Zanzibar. Wanajaribu kuziba/kuondoa soo. It's loo little, too late.
CCM acheni kumkataa mwanachama wenu Jecha yaani munamfanya toilet paper aka condom hivi hivi.
 
Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

Mwenyekiti wa zamani wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar, Jecha Salim Jecha ameshindwa kupata wadhamini 250 kila Mkoa katika Mikoa mitatu ya Zanzibar baada ya Wanachama wa Chama cha Mapinduzi kukataa kumdhamini.

Jecha alichukua fomu ya kuomba ridhaa ya kuwania Urais wa Zanzibar kupitia CCM, uamuzi ambao ulizusha mjadala mkubwa huku wanasiasa na hata wanaharakati walikosoa vikali kitendo hicho.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, Wenyeviti wa CCM wa Mikoa ya Zanzibar wamesema kuwa walipokea maombi ya Jecha apatiwe wadhamini 250, lakini hakuna Mwanachama wa CCM aliyejitokeza kumdhamini.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kaskazini Pemba, Hamad Mbelwa, ameserma kwamba wengi wa wananchama wa CCM hawakuwa tayari kumdhamini Jecha kwas kuwa hawafahamu ni loini alijiunga na CCM.

“Huyu bwana alitoa taarifa ya kuomba wanachama wamdhamini, kama kawaida nasi tukawajulisha wanachama… kwa bahati mbaya hakujitokeza mtu” Alisema Mbelwa.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja, Idd Ali Ame alisema kuwa hadi saa nane mchana ya jana, Jescha Salim hakuweza kupata wanachama wa kumdhamini katika Mkoa wa Kaskazini licha ya tarifa kutolewa na kuwafikia wanachama katika matawi yao.

Katika Mkoa wa Mjini, Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa huo Talib Ali Talib, alisema kuwa udhamini wa Jecha umekuwa mtihani mkubwa kwao kwani wanachama wengi walishughulika na udhamini wa wagombea wengine huku wakimuacha Jecha na fomu zake.

Aidha, hali kama hiyo imejitokeza katika Mikoa karibu yote ya Kichama alipokwenda kuomba wadhamini ambapo baadhi yao walihoji uanachama wake ndani ya CCM.

Katika Tawi la CCM chumbuni inakoaminika kuwa Jecha ni mwanachama katika Tawi hilo, wana CCM walihoji uhalali wa uanachama wake na kutoa maoni tofauti huku wengi wakisema hana sifa za kuwania uongozi ndani ya CCM kwa kuwa hajatimiza vigezo vya kikatiba.

“Katiba yetu iko wazi, inasema ili mwanachama mpya ambaye hakufikisha miaka mitano tangu kuingia CCM, hatoweza kugombea nafasi yoyote ya uongozi… sasa tunamshangaa Jecha kuomba ridhaa ya kuwa mgombea wakati uanachama wake ni wa mashaka” Alisema Masoud Machano kutoka Masumbani Jimbo la Chumbuni.

Habari kutoka Dunga Mkoa wa Kusini Unguja zinasema kuwa licha ya Jecha kukaa kwa muda mrefu Makao Makuu ya CCM Mkoa akisubiri wanachama kumdhamini, hadi jua linatua hakuweza kupata hata mwanachama mmoja.

Kwa mujibu wa utaratibu wa CCM kila mwanachama aliyechukua fomu ya kuomba ridhaa ya kuwa mgombea wa Urais wa Zanzibar kupitia Chama hicho, analazimika kupata wadhamini 250 katika Mikoa mitatu ya Zanzibar.

Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Zanzibar, Idara ya Oganaizesheni, Galos Nyimbo alisema hajapokea taarifa ya Jecha Salim Jecha ya kurejecha fomu.

Mwisho wa kutoa na kupokea fomu kwa wanaotaka ridhaa ya CCM kwa kugombea Urais wa Zanzibar ni Juni 30 mwaka huu.
Akale alikopeleka mboga
 
Hahahaha jecha bhana
 
Jecha amejichanganya yani anashtuka usingizini kumekucha yani mwisho ndo anakuja kuchukua fomu ya kugombea! Aya kwa chama kipi sasa maana CCM hakuwa mwanachama CHADEMA ndo vile tena. Harafu upate wadhamini eeh
 
... Jecha kwenda kuchukua fomu sio kwa bahati mbaya bali ni mkakati uliosukwa; ni picha linatengenezwa maabara. Ukisoma hoja zinazotolewa na viongozi wa CCM kukataa kumdhamini ya msingi zaidi ni "uanachama wake una mashaka" au "hawautambui uanachama wake".

Tafsiri yake ni kwamba wanataka kuaminisha umma kwamba hana uanachama wa chama hicho na kama anao ni wa hivi karibu sana sio enzi akiwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar back in 2015! Inataka kujengwa hoja kwamba wajumbe wa NEC-Zanzibar hususan Mwenyekiti ambaye alifanya maamuzi "mazito" 2015 hafungamani na CCM hivyo maamuzi yale yalikuwa free from influence ya chama/CCM.

Narudia tena, Jecha hajachukua fomu kwa bahati mbaya au hakwenda yeye mwenyewe bali ametumwa kuchukua fomu kimkakati kwa ajili ya propaganda!
Haiondoi mantiki kuwa Hadi NEC ma CCM yapo
 
CCM haina shukrani, hata Dr Shein akataa kumsaidia mwenzake kama yeye alivyomsaidia 2015? watumishi wa umma wanalakujifuza kuwa CCM siyo rafiki kwao inawatumia kushika madaraka ikishinda inawageuka, angalia Makamba, Nape na wengine wengi wamebaki kulia lia. shame on them
 
Uchaguzi mkuu wa zanzibar ni sampuli ya pekee kabisa duniani
Sijamuelewa Ndugu Jecha Salum Jecha kuutaka urais kupitia ccm
Alipompa Dr.Shein uraisi wa mezani ikawezekana, naye anajaribu bahati yake ikiwa itatokea ateuliwe bahati kama hiyo inaweza kutokea kwake.

Anafahamu siyo kura zinazomuweka rais ikulu ya Zanzibar bali tume ya uchaguzi Zanzibar ambayo yeye ni mshauri wake mstaafu.
 
Wao waliompa form makao makuu wasijue umashaka wa Jechs,wao wanachama wa CCM mtaani ndio wautils shaka?
 
wamdhamini tu bwana wasimtupe maana aliwafanyia kazi kubwa mno.
 
Back
Top Bottom