IMF yakadiria uchumi wa dunia utakua kwa asilimia 5.5 mwaka huu

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,501
9,280
Ripoti ya Mtazamo wa Uchumi wa Dunia iliyotolewa hivi karibuni na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) imekadiria kuwa, uchumi wa dunia utakua kwa asilimia 5.5 mwaka 2021, ikiwa ni asilimia 0.3 zaidi ya makadirio yaliyotolewa mwezi Oktoba.

Mchumi mwandamizi wa IMF Gita Gopinath amesema, sehemu kubwa kwa sasa inategemea matokeo ya kasi kati ya virusi vinavyobadilika na chanjo ili kumaliza janga la virusi vya Corona, na kwa uwezo wa sera zitakazotoa uungaji mkono mara hilo litakapotokea.

Ripoti hiyo pia imesema, uchumi wa China umekua kwa asilimia 2.3 mwaka jana. Mchumi huyo amesema, China imepata mafanikio katika kudhibiti janga hilo, hatua iliyochukua nafasi kubwa katika kurejesha shughuli za kibiashara mapema.

Mwaka huu, uchumi wa China unakadiriwa kukua kwa asilimia 8.1, na utaongezeka kwa asilimia 5.6 mwaka 2022, huku uchumi wa dunia ukikadiriwa kukua kwa asilimia 4.2 mwaka kesho.
 
Mwanzo hiyo IMF niliona kama IFM. Nilikuwa excited sana....
 
Back
Top Bottom